settings icon
share icon
Swali

Uasherati ni nini?

Jibu


Katika Agano Jipya, neno linalotasfsiriwa mara nyingi zaidi “uasherati” ni porneia.Neno hili pia linatafsiriwa kama “ukahaba,” “uasherati,” na “uzinzi.” ina maana ya “kujitoa kwa usafi wa kingono,”na hutumiwa hasa kwa mahusiano ya ngono kabla ndoa. Kutoka kwa neno hili la Kigiriki tunapata neno la Kiingereza ponografia, linalotokana na dhana ya “kuuza.” Uasherati ni “kuuza” usafi wa kingono na unahusisha aina yoyote ya kujieleza kingono iliyo nje kulingana na mipaka ya uhusiano wa ndoa uliolezwa katika Biblia (Mathayo 19:4-5).

Uhusiano kati ya uasherati na uzinzi unaeleweka vyema katika muktadha wa 1 Wakorintho 6:18, ambayo inasema, “Ikimbieni zinaa. Kila dhambi aitendayo mwanadamu ni nje ya mwili wake; ila yeye afanyaye zinaa hutenda dhambi juu ya mwili wake mwenyewe.” Miili ya waumini ni “hekalu la Roho Mtakatifu” (1 Wakorintho 6:19-20). Ibada ya sanamu za wasioamini mara nyingi ilihusisha vitendo viovu na vya uasherati vilivyofanywa katika hekalu la miungu za uongo. Tunapoitumia miili yetu kwa madhumuni mabaya, tunaiga ibada ya wasioamini kwa kukufuru hekalu takatifu la Mungu kwa vitendo anavyoviona kuwa chukizo (1 Wakorintho 6:9-11).

Marafuku ya Biblia dhidi ya uasherati mara nyingi huambatana na maonyo dhidi ya “uchafu” (Warumi 1:24; Wagalatia 5:19; Waefeso 4:19). Neno hili kwa Kigiriki ni akatharsia, linalomaanisha “najisi, mchafu, asiyefaa kwa sherehe.” Linaashiria vitendo vinavyomfanya mtu asifae kuingia katika uwepo wa Mungu. Wale wanaoshikilia uasherati na uchafu usio na toba hawawezi kuja mbele za Mungu. Yesu alisema, “Heri walio safi wa moyo, maana watamwona Mungu” (Mathayo 5:8; linganisha, Zaburi 24:3-4). Haiwezekani kudumisha urafiki wenye afya na Mungu wakati miili na roho zetu zinatumikia uchafu wa aina yoyote.

Ujinsia ni mpango wa Mungu. Yeye mwenyewe anaweza kufafanua vigezo vya matumizi yake. Biblia inasema wazi kuwa ngono iliumbwa ili ifurahiwe kati ya mwanaume mmoja na mwanamke mmoja ambao wako katika ndoa ya agano mpaka mmoja wao afe (Mathayo 19:6). Ujinsia ni zawadi yake takatifu ya harusi kwa wanadamu. Usemi wowote wa nje ya vigezo hivyo huunda unyanyasaji wa zawadi ya Mungu. Unyanyasaji ni utumiaji wa watu au vitu kwa njia ambazo hazikukusudiwa kutumiwa. Biblia hutaja hii kuwa dhambi. Uzinzi, ngono kabla ya ndoa, ponografia, na mahusiano ya jinsia moja yote yako nje ya mpango wa Mungu, ambayo huyafanya kuwa dhambi.

Yafuatayo ni baadhi ya pingamizi za kawaida kwa amri za Mungu dhidhi ya uasherati:
1. Sio vibaya ikiwa tunapendana. Biblia haitofautishi kati ya mahusiano ya kimapenzi “yenye upendo” na “yasiyo na upendo”. Tofauti pekee ya kibiblia ni kati ya watu waliofunga ndoa na wasiofunga ndoa. Ngono ndani ya ndoa imebarikiwa (Mwanzo 1:28); ngono nje ya ndoa ni “ukahaba” au “uasherati” (1 Wakorintho 7:2-5).
2. Nyakati zimebadilika, na kile kilichokuwa kibaya katika nyakati za Biblia hakionekani tena kuwa dhambi. Maandiko mengi yanayolaani uasherati pia yanajumuisha maovu kama vile uchoyo, tamaa, wizi, nk (1 Wakorintho 6:9-10; Wagalatia 5:19-21). Hatuna tatizo kuelewa kwamba mambo haya mengine bado ni dhambi. Tabia ya Mungu haibadiliki na maoni ya utamaduni ( Malaki 3:6; Hesabu 23:19; Waebrania 13:8).
3 Tuko kwenye ndoa mbele za macho za Mungu. Hoja hii inamaaanisha kuwa Mungu ana macho yaliyopotoka. Upotoshaji wa wazo hili ni kwamba Mungu aliyeumba ndoa mwanzoni angemaliza amri yake mwenyewe ili kukidhi kile alichokiita dhambi. Mungu alitangaza ndoa kuwa mwanaume mmoja na mwanamke mmoja walioungana kwa maisha (Marko 10:6-9). Biblia mara nyingi hutumia picha ya harusi na ndoa ya agano kama sitiari kufundisha ukweli wa kiroho (Mathayo 22:2; Ufunuo 19:9). Mungu huchukulia ndoa kwa uzito sana, na “macho” yake huona uasherati jinsi ulivyo, bila kujali jinsi tulivyoufafanua upya kwa ustadi.
4 . Bado naweza kuwa na uhusiano mzuri na Mungu kwa sababu ananielewa. Mithali 28:9 inasema, ”Yeye aligeuzaye sikio lake asiisikie sheria, Hata sala yake ni chukizo.” Tunajidanganya tunapoamini kwamba tunaweza kuchagua dhambi kwa ukaidi na Mungu Asijali. Waraka wa Kwanza wa Yohana 2:3-4 ina changamoto kubwa kwa wale wanaodumu katika mstari huu wa kufikiri: “Basi katika hili twajua ya kuwa tumemjua, tukizishika amri zake. 4 Mtu yeyote asemaye kuwa, “Ninamjua,” lakini hazishiki amri zake, ni mwongo, wala ndani ya mtu huyo hamna kweli.”

Waebrania 13:4 inafanya matarajio ya Mungu kwa wana Wake kuwa wazi kabisa: “Ndoa na iheshimiwe na watu wote, na malazi yawe safi; kwa maana waasherati na wazinzi Mungu atawahukumia adhabu.” Uasherati ni mbaya. Damu ya Yesu inaweza kututakasa kutoka kwa kila aina ya uchafu tunapotubu na kupokea msamaha wake (1 Yohana 1:7-9). Lakini usafi huo unamaanisha kwamba asili yetu ya zamani, pamoja na uasherati, imeuawa (Warumi 6:12-14; 8:13). Waefeso 5:3 inasema, “Lakini uasherati, usitajwe miongoni mwenu, wala uchafu wa aina yoyote, wala tamaa, kwa sababu mambo haya hayastahili miongoni mwa watakatifu.”

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Uasherati ni nini?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries