settings icon
share icon
Swali

Je ninaweza kuwa na uakikisho wa wokovu wangu?

Jibu


Je unawezaje kujua hakika umeokolewa? Hubu angalia 1Yohana 5:11-13: “Na huu ndio ushuhuda, ya kwamba Mungu alitupa uzima wa milele; na uzima huu umo katika Mwanawe. Yeye aliye naye Mwana, anao huo uzima; asiye naye Mwana wa Mungu hana huo uzima. Nimewaandikia ninyi mambo hayo, ili mjue ya kuwa mna uzima wa milele, ninyi mnaoliamini Jina la Mwana wa Mungu” Ni nani huyo aliye na Mwana? Ni wale wote ambao wamemwamini na kumkubali Mwana (Yohana 1:12). Ikiwa umempokea Yesu, uko na uzima. Si maisha ya muda bali ya milele.

Mungu anataka tuwe na uakikisho wa wokovu wetu. Hatuwezi kuishi maisha yetu ya Kikristo tukiwa na hofu na shaka kila siku ikiwa kweli tumeokoka. Hiyo ndio sababu Bibilia inafanya mpango wa kuokoka kuwa wazi. Mwamini Yesu na utaokoka (Yohana 3:16; Matendo ya Mitume 16:31). Je unaamini kuwa Yesu ni Mwokozi, na alikufa kuliba deni ya dhambi zako (Warumi 5:8; 2Wakorintho 5:21)? Je unamwamini Yeye mwenyewe kwa wokovu? Kama jibu lako ni ndio, umeokoka! Uakikisho wamaanisha, “kuwekwa mbele zaidi ya shaka.” Kwa kuliweka neno la Mungu kwa moyo wako unaweza, “kuwa juu ya shaka zote” dhana na ukweli wa uzima wako na wokovu wako wa milele.

Yesu mwenyewe anatuakikishia hayo kuhusu wale wote ambao wamemwamini: “Nami nawapa uzima wa milele; wala hawatapotea kamwe; wala hakuna mtu atakayewapokonya katika mkono wangu. Baba yangu aliyenipa hao ni mkuu kuliko wote; wala hakuna mtu awezaye kuwapokonya katika mkono wa Baba yangu” (Yohana 10: 28-29). Uzima wa milele ni uzima wa milele. Hakuna mtu yeyote, hata mmoja, hata wewe mwenyewe anayeweza kuchukua kipawa cha wokovu cha Mungu kilicho ndani ya Yesu.

Twalificha neno la Mungu ndani ya mioyo yetu ili tusi sini kinyume chake (Zaburi 119:11), na hii ni pamoja na dhambi ya kushuku. Kuwa na furaha kwa kila kitu ambayo neno la Mungu lakwambia badala ya kushuku tunaweza kuishi na ujaziri. Tunaweza kuwa na ujaziri katika neno la Kristo pekee, yakuwa wokovu hautakuwa wa maswali. Uakikisho wetu uko katika misingi ya upendo wa Mungu katika Yesu Kristo.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je ninaweza kuwa na uakikisho wa wokovu wangu?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries