settings icon
share icon
Swali

Je! Tutakuwa na sura gani Mbinguni?

Jibu


Katika kitabu cha 1 Wakorintho, sura ya 15, Paulo anazungumza kuhusu ufufuo na mwili uliofufuliwa. Katika mstari wa 35 na ule unaofuata, asema kwamba miili yetu ya mbinguni itakuwa tofauti na miili yetu ya asili, kukiwa na tofauti nyingi sana. Ingawa miili yetu ya kidunia inakabiliwa na kifo, miili yetu iliyofufuliwa itakuwa na sifa ya kutokufa (haiwezi kukabiliwa na kifo). Vivyo hivyo, wakati miili yetu ya kidunia inaweza kuharibika, itakuwa ile isyoharibika (1 Wakorintho 15:53). Pia, huku miili yetu ya asili inakabiliwa na udhaifu, miili yetu iliyofufuliwa itakuwa na sifa ya nguvu (mstari wa 43).

Ulinganisho mwingine ni kwamba sasa tuna mwili wa asili, lakini baadaye tutakuwa na mwili wa kiroho. Labda hii haimaanishi kuwa tutakuwa kama mizimu isiyo na mwili hata kidogo na inayoelea bila kuingiliana na vitu vinavyotuzunguka. Baada ya yote, mstari wa 49 unasema kwamba tutakuwa na mwili kama mwili wa Yesu uliofufuka (ona pia 1 Yohana 3:2). Na Yesu, baada ya kufufuka kwake, aliwaambia wamguze na wamtazame akila, akionyesha kwamba yeye hakuwa roho tu (Luka 24:37-43). Badala yake, kuna uwezekano zaidi kwamba kama vile mwili wa asili unavyofaa kwa ajili ya maisha haya ya sasa katika ulimwengu wetu wa kimwili, mwili wa kiroho utakuwa ule ambao utatufaa zaidi kwa ajili ya kuwepo milele ambako tumekusudiwa katika makao yetu ya milele. Mwili wa Yesu aluofufuka ulikuwa na uwezo wa kuingia vyumba vilivyofungwa kwa hiari yake (Yohana 20:19). Mwili wetu wa kidunia hutuwekea mipaka kwa njia (na vipimo) ambazo mwili wetu wa kiroho hautafanya.

Wakorintho wa Kwanza 15:43 pia inaelezea mabadiliko kutoka kwa “kupandwa katika aibu” hadi “kufufuliwa katika utukufu.” Wafilipi 3:21 inasema kwamba Yesu “ataubadili mwili wetu wa unyonge, ili upate kufanana na mwili wake wa utukufu.” Miili yetu inayooza inaelezewa kwa neno aibu kwa sababu ina alama ya matokeo ya dhambi. Wakati fulani miili yetu inaharibiwa kwa sababu ya dhambi zetu wenyewe, za kibinafsi, kama vile ubongo ambao hauwezi tena kuunda mawazo kamili kwa sababu ya matumizi mabaya ya dawa za kulevya. Wakati mwingine miili yetu ina alama ya dhambi za wengine, kama vile kovu kutoka kwa mtu anayetutendea kwa jeuri. Lakini hizo sio alama pekee za kimwili za dhambi. Kwa maneno ya jumla zaidi, mwili wa nyama unaoharibika ni matokeo ya moja kwa moja ya kuanguka kwa wanadamu katika dhambi. Kusingekuwa na dhambi, kusingekuwa na uozo na kifo (1 Wakorintho 15:56). Lakini Mungu, kwa njia ya nguvu ya Kristo igeuzayo, anaweza kuwainua watoto wake kwa miili mipya ya utukufu, iliyo huru kabisa na uharibifu wa dhambi na kumiliki utukufu wa Kristo badala yake.

Kwa muhtasari, hatuambiwi hasa jinsi tutakavyoonekana katika maisha yajayo, tutaonekana kuwa na umri gani, au ikiwa tutaonekana wambamba au wanono. Lakini, ingawa wengi wanaamini kwamba tutafanana kwa kiasi fulani na jinsi tunavyoonekana sasa, tunajua kwamba kwa njia zozote sura au afya yetu imebadilishwa kwa sababu ya dhambi (iwe kwa sababu ya uchaguzi mbaya wa afya, ulemavu wa kurithi, majereaha, kuzeeka, n.k.), sifa hizi hazikuwa katika mwonekano wetu katika maisha yajayo. Muhimu zaidi, asili ya dhambi, iliyorithiwa kutoka kwa Adamu (Warumi 5:12) haitakuwa nasi tena, kwa maana tutafanywa kuwa utakatifu wa Kristo (1 Yohana 3:2).

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Tutakuwa na sura gani Mbinguni?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries