settings icon
share icon
Swali

Je, tunapaswa kikamilifu kutafuta kwa mchumba, au kumsubiri Mungu kuleta mchumbae kwetu?

Jibu


Jibu kwa maswali yote ni "naam." Kuna uwiano muhimu kati ya hizo mbili. Hatupaswi kutafuta mchumba kana kwamba inategemea tu juhudi zetu wenyewe. Wala hatupaswi kuwa watazamaji tu, kufikiri kuwa Mungu siku moja atamfanya mke kufika katika mlango wetu. Kama Wakristo, katika wakati Fulani ikiwa tumeamua kwamba tunamtafuta mchumba, tunapaswa kuanza mchakato na maombi. tukijuwazilisha wenyewe kwa mapenzi ya Mungu katika maisha yetu ni hatua ya kwanza. "Nawe utajifurahisha kwa Bwana naye atakupa haja za moyo wako" (Zaburi 37:4). Kujifurahisha katika Bwana ina maana sisi kupata radhi katika kumjua Yeye na kuamini kwamba yeye pia atatufuraha. Yeye ataweka matamanio yake ndani ya mioyo yetu, na katika mazingira ya kutafuta mchumba, kumaanisha tunajitamani mchumba Yeye anatamani tupatemwenye anajua atatuletea furaha. Mithali 3:6 inatuambia, "Katika njia zako zote mkiri yeye, naye atayanyosha mapito yako." Kumtambua Yeye katika kutafuta mchumba inamaanisha kujiwasilisha kwa mapenzi yake tawala na kumwambia kuwa chochote Yeye ataamua ni bora ndicho utataka.

Baada ya kujitoa sisi wenyewe kwa mapenzi ya Mungu, tunapaswa kuwa wazi juu ya tabia ya mume mcha Mungu au mke na tutafute mchumba ambaye amehitimu ngazi ya kiroho. Ni muhimu kuwa na uelewa wa wazi wa sifa hizi kwanza na kisha kutafuta mtu ambaye ako nazo. "Kuingia katika mapenzi" na mtu na kisha kugundua yeye hana sifa za kiroho kumwezesha kuwa mchumba wetu ni kukaribisha maumivu ya moyo na kujiweka katika nafasi ngumu sana.

Tunapoielewa Bibilia na kufahamu kile tunachotakiwa kukitafuta kulingana na maandiko, tutafahamu vyema cha kukitafuta kwa mchumba na kuelewa kwamba Mungu atamleta yeye katika maisha yetu kwa wakati wake mtimilifu na kulingana na mapenzi yake. Tunapoomba, Mungu atatuongoza kwa yule anayetufaa. Ikiwa tutasubiri wakati wake mtimilifu, tutampokea anayetufaa kwa mienendo, matamanio yetu na hata atakayetufaa kiasili. Tunafaa (methali 3:5), hata wakati majira yake si majira yetu. Wakati mwingine Mungu anawaita watu wasioe kwa vyovyote vile (1 Wakorintho 7), lakini katika hali hizo, yeye anaweka wazi kwa kuondoa hamu ya ndoa. Muda wa Mungu ndio kamili, na kwa imani na uvumilivu, sisi hupokea ahadi zake (Waebrania 6:12).

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, tunapaswa kikamilifu kutafuta kwa mchumba, au kumsubiri Mungu kuleta mchumbae kwetu?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries