settings icon
share icon
Swali

Theolojia ya agano jipya ni nini?

Jibu


Theolojia ya agano jipya inaweza elezewa vyema zaidi kama kanuni tafsiri ya Biblia au kigezo cha kutafsiri Biblia ambayo kwayo mtu husoma na kutafsiri Maandiko. Kama kanuni ya kufasiri, inasimama kama kiunganishi kati ya theolojia ya mgao na theolojia ya agano. Hiyo haimaanishi kwamba theolojia ya agano jipya kimakusudi imejiweka kati ya theolojia ya ugawaji na theolojia ya agano, bali kwamba theolojia ya agano jipya ina vipengee ambavyo pia viko katika theolojia ya ugawaji na theolojia ya agano. Kwa hivyo, hatuwezi kufafanua theolojia ya agano jipya bila kutaja theolojia ya ugawaji na theolojia ya agano.

Theolojia ya ugawaji hasa huona Maandiko yakifunuliwa yakifuatana, hasa kwa “matawa” saba. Mgawanyo unaweza kufafanuliwa juu juu kuwa namna ambayo Mungu anatawala hatua yake na mwanadamu na uumbaji. Kwa hivyo, utawala Mungu kwa Adamu ulikuwa tofauti na utawala wake kwa Abrahamu, n.k. Theolojia ya ugawaji inaona ufunuo kuwa wenye kuendelea, yaani, katika kila kipindi, Mungu anafunua zaidi na zaidi mpango Wake wa kiungu wa ukombozi. Hata hivyo, ingawa Maandiko ni ufunuo unaoendelea, kila kipindi kinachofuata kinawakilisha njia mpya ya Mungu ya kushughulikia uumbaji wake. Kwa maneno mengine, kulingana na theolojia ya mgawo, kuna kiwango kikubwa cha kutoendelea miongoni mwa vipindi; kipindi cha zamani kinapoisha na kipya kuanza, ile njia ya “zamani” ya kufanya mambo chini ya enzi ya zamani inaondolewa na enzi mpya. Na kila kipindi kwa kawaida huletwa kwa ufunuo mpya kutoka kwa Mungu.

Jambo la kukumbuka na theolojia ya mgawo ni kwamba kuna tofauti kubwa kati ya Israeli na Kanisa. Hao ni watu wawili tofauti wenye hatima mbili tofauti katika himaya ya Mungu. Kanisa linaonekana kama “limetengwa” na vile Mungu anavyotendea taifa la Israeli. Ufalme uliorejeshwa ambao Isreli iliahidiwa utatimia katika wakati wa Milenia (kipindi cha miaka elfu moja). Hadi wakati huo itakuwa ni kipindi cha Kanisa-wakati wa watu wa Mataifa.

Theolojia ya Agano ni kinyume kabisa cha theolojia ugawo. Huku zote zikikubaliana kwamba Maandiko ni ufunuo unaoendelea, kanuni kuu ya theolojia ya agano ni agano. Theolojia agano inaona maagano mawili ya kitheolojia katika Maandiko-agano la kazi na agano la neema. Agano la kazi lilianzishwa katika Bustani kati ya Mungu na mwanadamu ambapo Mungu aliahidi mwanadamu uzima kwa ajili utiifu na hukumu kwa kutotii. Agano la kazi lilifanywa tena pale mlima Sinai Mungu alipoahidi Israeli maisha marefu na baraka katika nchi ikiwa wangetii Agano la Musa, lakini kufukuzwa na hukumu iwapo wangekosa kutii. Agano la neema lilitekelezwa baada ya dhambi ya Adamu na Hawa na linadhihirisha agano la Mungu lisilo na masharti na mwanadamu ili kukomboa na kuokoa wateule. Maagano yote mbalimbali ya kibiblia (Nuhu, Abrahamu, Musa, Daudi, na lile Jipya) ni utimilifu wa agano la neema ambapo Mungu anatekeleza mpango wake wa ukombozi katika historia ya mwanadamu. Kwa hivyo ambapo theolojia ya ugawo iliona kutokuwa na mwendeleo kati ya vipindi mbalimbali (na hasa kati ya Agano la Kale na Agano Jipya), theolojia ya agano inaona mwendeleo mkubwa.

Hii ni dhahiri hasa katika ukweli kwamba theolojia ya agano haioni tofauti kubwa kati ya Israeli na Kanisa. Zote mbili zinaonekana kuwa kundi moja la watu wa Mungu linaoendelea na walio na hatima moja.

Yote hayo hutumika kama msingi wa kutazama theolojia ya agano jipya. Kama ilivyotajwa hapo mbeleni, theolojia ya agano jipya ni sehemu ya kati kati ya pande zote mbili. Inashiriki mengi na theolojia ya agano ya kawaida, haswa mwendeleo kati ya Kanisa na Israeli kama watu wa Mungu. Hata hivyo, pia inatofautiana na theolojia agano kwamba sio lazima mtu ayatizame Maandiko kama ufunuo wa ukombozi katika agano la kazi/agano la neema. Badala yake inaona Maandiko katika dhana zaidi ya ahadi/utimilifu.

Tofauti kubwa kati ya theolojia ya agano jipya na theolojia ya agano ni jinsi kila moja inavyotizama Sheria ya Musa. Theolojia ya agano inatazama Sheria katika njia tatu: kiraia, sherehe na maadili. mtazamo wa sheria kiraia ulikuwa kwa zile sheria katika agano la Sinai ambalo lilitawala taifa liliongozwa na Mungu la Israeli walipokuwa wakiishi katika Nchi ya Ahadi. Sehemu ya utaratibu rasmi wa Sheria uliongoza ibada ya Mungu kwa Israeli walipokuwa katika nchi hiyo. Mwisho, sehemu ya maadili ya sharia iliyoongoza mwenendo wa watu wa Mungu. Inapaswa kueleweka kwamba Sheria yenyewe inaambatana na ni kamilifu na kwamba Wayahudi hawakueleza kinaganaga kati ya kiraia, utaratibu rasmi, au kiadili; haya ni maneno tu ya kusaidia kutambua nyancha tatu za maisha ya Waisraeli ambayo Sheria ya Musa ilisimamia.

Kulingana na fasihi ya thoeolojia ya agano, Yesu alikuja kutimiza Sheria (Mathayo 5:17). Alifanya hivyo kwa kutosholeza sehemu zote za Sheria, taratibu rasmi, kiraia na maadili. Yesu Kristo ndiye ukweli wa kivuli dhabihu za mfumo wa Agano la Kale na kwa hivyo anatimiza kipengele cha utaratibu rasmi wa Sheria. Yesu Kristo pia alibeba adhabu ambayo dhambi zetu zilistahili na kwa hivyo alitimiza sehemu ya kiraia ya Sheria. Hatimaye, Yesu Kristo aliishi kikamilifu kulingana na kipengee cha madili cha Sheria na kutimiza uadilifu wote inavyohitajika Kisheria.

Sasa, kipengele cha maadili cha Sheria kinawakilisha kiini cha agano la kazi. Kwa hivyo kimepita kazi ya Musa. Kwa maneno mengine, kila mara Mungu amehitaji utakatifu kutoka kwa wanadamu. Agano la matendo halikukataliwa kwa sababu ya anguko, wala halikupuuzwa hata ingawa lilitimizwa katika Kristo. Kipengele cha maadili cha Sheria bado kipo kama kiwango cha maadili kwa wanadamu kwa sababu kinaakisi tabia ya Mungu, na hiyo haibadiliki. Kwa hivyo, theolojia ya agano bado inaona Sheria ya Musa (haswa Amri Kumi) kama maagizo kwa Kanisa, ijapokuwa vipengele vya utaratibu rasmi na uraia hazifai katika Kristo.

Theolojia ya agano jipya inaona Sheria ya Musa kwa ujumla na kuona yote yakitimizwa katika Kristo (hadi sasa inakubaliana na theolojia agano). Hata hivyo, kwa sababu theolojia ya agano jipya inaiona Sheria ya Musa kwa ujumla, vile vile inaona kipengee cha maadili katika Sheria ya Musa kama iliyotimizwa katika Kristo na hakitumiki tena na Wakristo. Badala ya kuwa chini ya kipengele cha maadili ya Sheria ya Musa kama ilivyofupishwa katika Amri Kumi, tuko chini ya sheria ya Kristo (1 Wakorintho 9:21). Sheria ya Kristo itakuwa maagizo ambayo Kristo aliyataja haswa katika Injili (k.m., Mahubiri ya Mlimani). Kwa maneno mengine, sehemu yote ya Sheria ya Musa imetengwa katika theolojia ya agano jipya; haitumiki tena kwa njia yoyote ile kwa Wakristo. Kwa hivyo, huku theolojia agano inaona mwendelezo kati ya Agano la Kale na Jipya kuhusu watu wa Mungu na njia ya wokovu, theolojia ya agano jipya inaweka tofauti kubwa kati ya Agano la Kale katika masuala ya toafuti kati ya agano la kale la Musa na agano jipya lililopatanishwa na Kristo. Agano la kale limepitwa na wakati (ikiwa ni pamoja na kipengele cha maadili cha Sheria ya Musa) na kubadilishwa na agano jipya na sheria ya Kristo kutawala maadili yake.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Theolojia ya agano jipya ni nini?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries