settings icon
share icon
Swali

Theolojia ya kimuktadha ni gani?

Jibu


Pia inajulikana kama “kuchukua mtindo na tabia za tamaduni nyingine,” theolojia ya muktadha inarejelea jinsi kanisa katika kila majira linabadili mafundisho yake ili kufikia utamaduni ambao linajipata ndani yake. Kuna mifano mingi ya hili, lakini pengine mfano ulio bora zaidi unapatika katika 1 Wakorintho 11:4-7. Mafundisho ya Paulo hapa yanahusiana na kufunika kichwa. Kwa mwanamke katika utamaduni huo kutofunika kichwa chake ilikuwa jambo lisilofikirika kabisa. Utaji au kufunika kichwa cha mwanamke wa muumini wa Korintho kulionyesha kuwa alikuwa chini ya mamlaka ya mumewe, na kwa hivyo kuwa chini ya utii wa Mungu. Katika utamaduni wa Korintho, kwa kawaida wanawake walifunika kichwa kama ishara ya utiivu wao kwa waume zao. Paulo anathibitisha uhalali wa kufuata itifaki hiyo ya kitamaduni-dharau la kufunika kichwa kwa wanawake kungeonyesha ishara mbaya kabisa kwa utamaduni kwa ujumla. Kwa kweli, Paulo anasema kwamba, ikiwa mwanmke Mkristo anakataa kufinika kichwa chake, anaweza pia kunyoa nywele yake- kitendo ambacho kingeleta aibu (aya ya 6). Mwanamke ambaye alikataa kuvaa shela katika utamaduni huo kwa ufupi alikuwa anaesema, “Ninakataa kutii utaratibu wa Mungu.” Fundisho la Mtume Paulo lilikuwa kwamba kuvaa “shela” kwa mwanamke lilikuwa tendo la nje la kuonyesha nia ya moyo wa utiivu kwa Mungu na kwa mamlaka Yake iliyowekwa. Ili kuingiza mafundisho hayo kwa tamaduni nyingine mbalimbali iko chini ya nyancha ya theolojia ya muktadha.

Kwa wazi, mafundisho kutoka kwa Biblia yanapaswa kutafsiriwa kwa muktadha wa utamaduni. Hata hivyo, kanuni za msingi za neno la Mungu bado ni zilezile hii leo jinsi zilivyokuwa zilipoandikwa. Kanuni katika kifungu cha 1 Wakorintho ni kwamba Kristo ni kuchwa juu ya mume, na mme ni kichwa cha mke, ambaye anapaswa kujitiisha kwa kuonyesha unyenykevu wake kwa njia zinazofaa kitamaduni.

Theolojia ya muktadha hutumia kanuni kutoka kwa Biblia na kuichuja kupitia kwa mtazamo wa marejeleo ya kisasa. Katika kuunda mfumo huo wa kitheolojia, mtu lazima azingatie mambo ya kiisimu, kijamii-kisiasa, kitamaduni na kiitikadi. Matokeo yake wakati mwingine ni mchanganyiko wa imani. “Kumfuata Yesu” katika utamaduni na muktadha mmoja kunaweza kuonekana tofauti na “kumfuata Yesu” katika utamaduni mwingine katika upande mwingine wa dunia- na unaweza kuonekana kuwa si Ukristo hata kidogo. Ni wazi theolojia ya muktadha inapaswa kutumika kwa uangalifu. Daima kuna hatari katika kuafiki ukweli kwa utamaduni fulani, ukweli umelegezwa na injili inapotezwa katika kutafsiri.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Theolojia ya kimuktadha ni gani?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries