settings icon
share icon
Swali

Teolojia marekebisho ni gani?

Jibu


Kiujumla, teolojia marekebisho ni pamoja na mfumo wowote wa imani ambao unafuata athari ya mizizi yake kwa Kiprotestanti ya karne ya 16. Bila shaka, Wageuzi peke yao wenyewe hufuatilia chanzo cha mafundisho yao na maandiko, kama vile imedhihirishwa kwa kumbumbu yao ya "nakala ya maandiko," kwa hivyo teolojia marekebisho sio mfumo "mpya" wa imani lakini ni mmoja ambao unataka kuendeleza mafundisho ya kitume.

Kwa ujumla, teolojia marekebisho inashikilia mamlaka ya Maandiko, Mamlaka ya Mungu, kuokolewa kwa neema kwa njia ya Kristo, na umuhimu wa uinjilisti. Wakati mwingine inaitwa Teolojia Agano kwa sababu ya msisitizo wake juu ya ahadi kati ya Mungu na Adamu na agano jipya ambalo lilikuja kwa njia ya Yesu Kristo (Luka 22:20).

Mamlaka ya Maandiko. Teolojia Marekebisho inafundisha kuwa Biblia ni pumzi na neno la mamlaka la Mungu, latosha katika mambo yote ya imani na mazoezi.

Utukufu wa Mungu. Teolojia Marekebisho inafundisha kuwa Mungu anatawala kwa udhibiti wote juu ya viumbe vyote. Kwa hivyo Yeye ameteua matukio yote na kwa hivyo kamwe hawezi changanyikiwa kutokana na hali. Hii haikomeshi mapenzi ya kiumbe, wala kumfanya Mungu kuwa mwanzilishi wa dhambi.

Wokovu kwa neema. Teolojia Marekebisho inafundisha kuwa Mungu katika neema na huruma zake amechagua kuwakomboa watu kwake mwenyewe, kuwakomboa wao kutoka katika dhambi na kifo. Kanuni geuzi ya wokovu kwa kawaida huwakilishwa na neno la utani TULIP (pia inajulikana kama pointi tano ya Kikalvinisti):

T – Upotovu kamili. Mwanadamu daima ni mnyonge kabisa katika hali yake ya dhambi na ako chini ya hasira ya Mungu na kwa njia yoyote ile hawezi kumfurahisha Mungu. Jumla ya upotovu pia ina maana kwamba mwanadamu kwa kawaida hawezi tafuta kumjua Mungu, mpaka Mungu kwa neema amuweka katika kufanya hivyo (Mwanzo 6:5; Yeremia 17:9, Warumi 3:10-18).

U - uchaguzi bila vikwazo. Mungu, kutoka milele iliyopita, imechagua kuokoa umati mkubwa wa watu wenye dhambi, ambao hakuna mtu angeweza kuhesabu ( Warumi 8:29-30; 9:11; Waefeso 1:4-6,11-12).

L - upatanisho mdogo. Pia huitwa "ukombozi halisi." Kristo alichukua hukumu ya dhambi ya wateule juu yake mwenyewe na hivyo kulipia maisha yao kwa kifo chake. Kwa maneno mengine, hakufanya wokovu "uwezekane," bali aliupata kwa wale aliowachagua (Mathayo 1:21; Yohana 10:11, 17:9, Matendo 20:28, Warumi 8:32; Waefeso 5:25).

I - neema isiyo pingwa. Katika hali yake ya kuanguka, mwanadamu huyapinga mapenzi ya Mungu, ila ni neema ya Mungu hufanya kazi katika moyo wake hufanya yaye atamani kile awali alikuwa anakipinga. Kwamba, neema ya Mungu haiwezi kosa kukamilisha kazi yake ya kuokoa kwa wateule (Yohana 6:37,44; 10:16).

P - uvumilivu wa wateule. Mungu hulinda wateule wake kutokana na kuanguka; hivyo, wokovu ni wa milele (Yohana 10:27-29; Warumi 8:29-30, Waefeso 1:3-14).

Umuhimu wa uinjilisti. Teolojia Marekebisho hufundisha kwamba Wakristo wako katika dunia ili walete tofauti, kiroho kupitia uinjilisti na kijamii kwa njia ya maisha takatifu na ubinadamu.

Mambo mengine ya teolojia marekebisho kwa ujumla ni pamoja na maadhimisho ya sakramenti mbili (ya ubatizo na ushirika), mtasamo wa kikomo cha vipawa vya kiroho (karama bado hazijaachiwa kanisa), ni mtazamo usio wa mfumo wa maandiko. Wanao heshimika sana kwa makanisa ya megeuzi kwa uandishi wao ni pamoja na John Calvin , John Knox, Ulrich Zwingli, na Martin Luther. Kiri la kongamano la Westminster linajumuisha teolojia ya utamaduni zilizorekebishwa. Makanisa ya kisasa katika utamaduni wa mageuzi ni pamoja na Presbyterian Makanisa ya kikongamano (Congregationalist), na baadhi ya Baptisti.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Teolojia marekebisho ni gani?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries