settings icon
share icon
Swali

Teolojia badala ni nini?

Jibu


Theolojia mbadala kimsingi hufundisha kwamba Kanisa la imechukua nafasi ya Israeli katika mpango wa Mungu. Wafuasi wa theolojia badala huamini Wayahudi si wateule wa Mungu tena, na Mungu hana mipango maalum ya baadaye kwa ajili ya taifa hilo la Israeli. Maoni tofauti kuhusu uhusiano kati ya kanisa na Israeli yanaweza kugawanywa katika kambi mbili: aidha kanisa ni muendelezo wa Israeli (badala / theolojia agano ), au kanisa ni tofauti kabisa na tofauti na Israeli.

Teolojia Badala hufundisha kwamba Kanisa li badala ya Israeli na kwamba ahadi nyingi zilizotolewa kwa Israeli katika Biblia zimetimizwa katika kanisa la Kikristo, hata katika Israeli. Hivyo, unabii katika maandiko kuhusu baraka na ukombozi wa Israeli katika Nchi ya Ahadi ni "wa kiroho" au "hadhithi " katika ahadi ya baraka ya Mungu kwa kanisa. Matatizo makubwa huwepo kwa mtazamo huu, kama vile kuendelea kuwepo kwa watu katika karne na hasa hali ya uamsho wa kisasa wa Israeli. Kama Israeli imekuwa na imelaaniwa na Mungu, na hakuna tumaini la baadaye kwa ajili ya taifa la Wayahudi, ni jinsi gani sisi hueleza maisha ya kiajabu ya watu Wayahudi zaidi ya miaka 2000 iliyopita licha ya jitihada nyingi kuwaangamiza? Je, sisi hueleza ni kwa nini na jinsi gani Israeli ilionekana teana kama taifa katika karne ya 20 baada ya kutokuepo kwa miaka 1900?

Mtazamo kwamba Israeli na kanisa ni tofauti kwa wazi unafundishwa katika Agano Jipya. Kuzungumza kibiblia, kanisa ni tofauti kabisa na tofauti la Israeli, na zote mbili kamwe hasifai kuchanganyishwa au kutumika kwa mbadala. Sisi tunafundishwa katika maandiko kwamba kanisa ni kiumbe kipya kabisa ambacho kilikuwa siku ya Pentekoste na kitaendelea mpaka kichukuliwe mbinguni wakati wa kunyakuliwa (Waefeso 1:9-11, 1 Wathesalonike 4:13-17). Kanisa haina uhusiano na laana na baraka kwa Israeli. Ahadi, ahadi na onyo ni halali tu kwa ajili ya Israeli. Israeli imekuwa kwa muda imewekwa kando katika mpango wa Mungu katika kipindi chote cha miaka ya nyuma 2000 ya usambazaji.

Baada ya Unyakuo (1 Wathesalonike 4:13-18), Mungu hurejesha Israeli kama mpango wa lengo lake la msingi. Tukio la kwanza kwa wakati huu ni dhiki (Ufunuo sura ya 6-19). Ulimwengu utahukumiwa kwa kumkataa Kristo, huku Israeli ikitayarishwa kwa njia ya majaribio ya dhiki kubwa kwa ujio wa pili wa Masihi. Kisha, wakati Kristo atakaporudi duniani, katika mwisho wa dhiki, Israeli itakuwa tayari kumpokea. Mzaso wa Israeli ambao ulisalia baada ya dhiki utaokolewa na Bwana ataimarisha ufalme wake katika dunia hii na Yerusalemu kama mji mkuu wake. Pamoja na Kristo kutawala kama Mfalme, Israeli itakuwa taifa la kuongoza, na wawakilishi kutoka mataifa yote watakuja Yerusalemu kwa heshima na kumwabudu Mfalme, Yesu Kristo. Kanisa itarudi pamoja na Kristo na watatawala pamoja naye kwa halisi miaka elfu moja (Ufunuo 20:1-5).

Zote Agano la Kale na Agano Jipya huunga mkono uelewa wa ufalme kabal ya kipindi cha miaka 1000 / mgagwo wa mpango wa Mungu kwa Israeli. Hata hivyo, uungwaji kamili kwa ajili ya ufalme kabal ya kipindi cha miaka 1000 dhahiri hupatikana katika mafundisho ya Ufunuo 20:1-7, ambapo inasema mara sita ufalme wa Kristo utadumu miaka 1000. Baada ya dhiki Bwana atarudi na kuanzisha ufalme wake na taifa la Israeli, Kristo atatawala juu ya dunia yote, na Israeli kuwa kiongozi wa mataifa. Kanisa watatawala pamoja naye kwa halisi miaka elfu moja. Kanisa haicha chukua nafasi ya Israeli katika mpango wa Mungu. Huku Mungu anaweza kuelekeza mawazo yake hasa juu ya kanisa katika kipindi hiki cha neema, Mungu hajaisahau Israeli na siku moja atairejesha Israeli katika majukumu aliyo nuia kama taifa alilolichagua (Warumi 11).

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Teolojia badala ni nini?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries