settings icon
share icon
Swali

Je, tamaa asili ya ngono ni dhambi?

Jibu


Ujinsia na uzazi ni sehemu za msingi za kuwa hai. Viumbe vyote vilivyo hai vina aina fulani ya misukumo ya uzazi kwa sababu Mungu aliamuru kujamiiana kuwa njia ambayo viumbe vingi vingedumisha aina mbalimbali za viumbe. Kwa wanyama, hamu ya ngono ni misikumo ya kimwili kama njaa au kiu. Lakini kwa wanadamu, kujamiiana pia kunahusisha uhusiano wa kihisia, kiroho, kujidhibiti, na urafiki wa kisaikolojia. Ujinsia wetu ni sehemu muhimu ya kile tulicho, lakini haitufafanui. Sisi tu zaidi ya ujinsia wetu, na Mungu anatutazamia kuutawala, tusiuruhusu ututawale. Kwa kuwa tamaa za ngono zimeundwa na Mungu, si dhambi ya asili. Ni nzuri, lakini inapaswa kudhibitiwa na kuletwa chini ya sheria ya maadili ya Mungu (1 Wakorintho 7:8-9).

Hatuwezi kutenganisha utambulisho wetu na ujinsia yetu, jinsia yetu, au matamanio yetu. Ujinsia ni sehemu ya msingi ya utu wetu; hata hivyo, kujamiiana sio sawia na utu wetu. Sisi sio watu wa ujinsia tu, jinsia yetu, au tamaa zetu. Hizo ni baadhi ya vipengele vya utu wetu, lakini sio ufafanuzi wa utu wetu.

Tiliumbwa kwa mfano wa Mungu, na hatuwezi kujielewa isipokuwa tuanze na ukweli huu (Mwanzo 1:27). Wakiwa wameumbwa kwa mfano wa Mungu, wanadamu wana tafauti na wanyama na mimea, wao wana roho ya milele kama vile Mungu anavyo. Tulikusudiwa kuishi katika ushirika wa daima pamoja naye katika roho zetu, lakini ili kufanya hivyo, ni lazima tuweke miili yetu ya kimwili chini ya roho hiyo (1 Wakorintho 9:27). Tunaporuhusu tamaa za ngono ziamue mtindo wetu wa maisha au kutawala tabia zetu, tunaishi kama Wanyama badala ya uumbaji wa juu zaidi wa Mungu duniani. Tamaa za ngono zinapowekwa huru, tunaishi kana kwamba hatukuwa na mfano wa Mungu.

Tamaa za ngono, ingawa si dhambi zenyewe, huwa dhambi zinapotoka nje ya mipaka ambayo Mungu aliwawekea. Mungu aliposema, “Si vyema huyu mtu awe peke yake. Nitamfanyia msaidizi wa kumfaa” (Mwanzo 2:18), Alianzisha ngono ya ndoa kama sehemu ya mpango Wake mzuri (Mwanzo 1:31). Mpango wa Mungu kwa ajili ya kujamiiana kwa binadamu ulikuwa kwamba ungekuwa utimilifu wa kimwili na kiroho wa mwanamume na mwanamke kuwa “mwili mmoja” katika agano la maisha yote (Mwanzo 2:21-24). Yesu alirudia dhana hii alipoulizwa kuhusu talaka. Akajibu, “Kwa sababu hii mwanaume atamwacha baba yake na mama yake, naye ataambatana na mkewe, na hao wawili watakuwa mwili mmoja’? Hivyo si wawili tena, bali mwili mmoja. Kwa hiyo alichokiunganisha Mungu, mwanadamu asikitenganishe” (Mathayo 19:5-6).

Shetani amepotosha kila anachoumba Mungu kuwa chema. Ujinsia ni eneo ambalo amepata mafanikio makubwa kwa kuwashawishi mamilioni ya watu kwamba tamaa zao za ngono zinapaswa kuamua mwenendo wa maisha yao. Yule mwovu anapata udhibiti wa ujinsia wetu kupitia njia mbalimbali, na anatumia ubinafsi ulio katika kila moyo wa mwanadamu. Kwa kuptosha zawadi nzuri ya Mungu ya ngono, Shetani hupotosha tamaa zetu nzuri za ngono kuwa kitu chafu, mbaya, au chenye kudhuru. Tunaposikiliza mapendekezo yake badala ya kushikamana na mpango wa Mungu, tunaanguka katika mojawapo ya mitego yake. Kazi ya Shetani inaonekana katika kuenea kwa ushoga, unyanyasaji wa watoto, biashara ya ngono, ubkaji, uavyaji mimba, ngono na wanyama, migogoro ya utambulisho wa kijinsia, na imani ya ngono kupita kiasi. Matatizo hayo yote ni upotovu wa matamanio ya asili ya ngono.

Tunaweza kulinganisha tamaa ya ngono na umeme. Umeme ni ugunduzi wa ajabu, na unapotumiwa kwa usahihi na kuelekezwa, umeme hufaidisha sana ubinadamu. Lakini nguvu ya umeme lazima itumike kwa usahihi, au inaweza kuharibu. Wakati nyaya za umeme zimechomeka kwenye seheu iliyo na msingi mzuri, matokeo mazuri. Lakini ikiwa tutaweka kijiko-uma kwenye sehemu hiyo hiyo maafa hutokea. Ndivyo ilivyo kwa jinsia. Tunapopunguza tamaa zetu za asili za ngono kwa njia zile ambazo Mungu alitayarisha kwa ajili yao, matokeo yatakuwa mazuri. Lakini tunapokiuka mpango Wake kupitia uasherati, uzinzi, au usemi fulani potovu wa kujamiiana, uharibifu hutokea. Karama za Mungu huja na maagizo. Tunapofuata maagizo hayo, tunapata yale mema aliyokusudia kwa ajili yetu.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, tamaa asili ya ngono ni dhambi?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries