settings icon
share icon
Swali

Je! Biblia inasema nini kuhusu kuoa tena ikiwa talaka ilitokea kabla ya kuokoka?

Jibu


Hili ni swali gumu sana, la kuvutia, na lenye changamoto. Wengine wangesema kwamba kwa kuwa waaminio katika Kristo ni “viumbe vipya” na “yote yamekuwa mapya” (2 Wakorintho 5:17), dhambi na matokeo ya talaka huoshwa, na hivyo kumruhusu mtu ambaye aliachwa kabla ya kuwa muumini kuolewa tena. Wengine wangesema kwamba ingawa dhambi ya talaka ilipatanishwa na Kristo, matokeo ya dhambi hayakupatanishwa, na kwa hivyo mtu ambaye ametaliki kabla ya kuwa muumini hawezi kuoa tena.

Kwa kufanya swali hili kuwa gumu zaidi ni ukweli kwamba kuna maoni yanayotofautiana kuhusu ikiwa Wakristo wanaweza kuoa au kuolewa tena. Tafadhali soma nakala zifuatazo kwenye tovuti yetu:

“Biblia inasema nini kuhusu talaka na koa teana?”
“Nimetalikiwa. Je! ninaweza kuoa tena kulingana na Biblia?”
„Je! Kuoa tena baada ya talaka siku zote ni uzinzi?”
“Je! Unyanyasaji ni sababu inayokubalika ya talaka?”
“Ni sababu gani za kibiblia za talaka?”

Wakati Biblia inazungumza kuhusu ndoa, haizungumzi kwa Wakristo/waumini wanaofunga ndoa. Kanuni za kibiblia juu ya ndoa ni za ulimwengu wote. Ikiwa mwanamume na mwanake ambaye ataolewa, mbele za Mungu, wao wameoana kama vile Mkristo mume na mke ambao wameoana. Bado wao ni mwili mmoja (Mwanzo 2:24). Mungu bado anachukia talaka (Malaki 2:16). Mungu bado amewaunganisha pamoja, na hataki watenganishwe (Matahyo 19). Ingawa dhambi zetu zote—za kale, za sasa, na zijazo—husamehewa tunapookolewa, wokovu haufuti matokeo yote ya dhambi tulizotedna kabla hatujamwamini Kristo au dhambi tunazoendelea kutenda. Yesu alilipa adhabu ya dhambi zetu, lakini dhambi bado ina matokeo hasi halisi. Basi ni matumaini yetu kwamba, iwe ni kabla ya wokovu au baada ya wokovu, ikiwa talaka ilikuwa kwa sababu zisizo za kibiblia hakuna sababu za kuoa tena.

Walakini, kama vile nakala zilozoorodheshwa hapo juu zinaonyesha, tunaaamini katika kifungu cha kipekee. Ikiwa talaka ilitokea kwa sababu ya kutotubu, uzinzi ulioendelea, tunaamini kwamba mtu asiye na hatia anaweza kuoa tena. Hii ni kweli vile vile ikiwa mhusika asiye na hatia alikuwa muumini au asiyeamini wakati talaka ilipotokea. Kwa hivyo jibu kwaa Swali hili litategemea hali ya talaka. Ni hoja yetu kwamba iwe talaka ilitokea kabla au baada ya wokovu sio sababu kuu ya uamuzi. Haijalishi mtazamo mtu anaweza kuchukua kwa suala hili, ni muhimu kuelewa kwamba wokovu hautukomboi au kutusamehe kutokana na maamuzi yote ya kipimbavu na ya dhambi tuliyofanya kabla ya kumwamini Kristo.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Biblia inasema nini kuhusu kuoa tena ikiwa talaka ilitokea kabla ya kuokoka?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries