settings icon
share icon
Swali

Ni nini maana ya silaha zote za Mungu?

Jibu


Kifungu "silaha zote za Mungu " kinatokana na Waefeso 6:13-17: "Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya ouvu, na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama. Basi simameni, hali mmejifunga kweli viunoni, na kuvaa dirii ya haki kifuani,, na kufungiwa miguu utayari tupatao kwa Injili ya amani; zaidi ya yote mkiitwaa ngao ya imani, ambayo kwa hiyo mtaweza kuizima mishale yote yenye moto ya yule mwovu. Tena ipokeeni chapeo ya wokovu, na upanga wa Roho ambo ni neno la."

Waefeso 6:12 inaonyesha wazi kwamba vita na Shetani ni vya kiroho, na kwa hiyo hakuna silaha inayoonekana kutumika kwa ufanisi hidi yake na marafiki zake. Sisi hatupewi orodha ya mbinu maalum Shetani atatumia. Hata hivyo, kifungu ki wazi kabisa kwamba wakati tunafuata maelekezo yote kwa uaminifu, sisi huwa na uwezo wa kusimama, na tutakuwa na ushindi bila kujali mkakati wa Shetani.

Sehemu ya kwanza ya silaha yetu ni ukweli (mstari wa 14). Hii ni rahisi kuelewa, tangu Shetani ananenwa kuwa "baba wa uongo" (Yohana 8:44). Udanganyifu uu wa kwanza katika orodha ya mambo ambayo Mungu anaona kuwa chukizo. " ulimi unenao uongo" ni mojawapo ya mambo Anayaeleza kuwa "chukizo kwake" (Mithali 6:16-17). Kwa hivyo sisi tunahimizwa kuweka mbele ukweli kwa ajili ya utakazo wetu wenyewe na ukombozi, vile vile na kwa ajili ya manufaa ya wale ambao tunawashuhudia.

Pia katika mstari wa 14, tunaambiwa kuvaa dirii ya haki kifuani. Ngao humkinga shujaa sehemu ya kiungu muhimu kutokana na makonde ambayo pengine yanaweza kuwa hatari. Haki hii si matendo ya haki hufanywa na wanadamu. Badala yake, hii ni haki ya Kristo, imewekwa na Mungu na kupokewa kwa imani, ambayo inalinda mioyo yetu dhidi ya shutuma na madai ya Shetani na usalama wa maisha yetu ya ndani kutokana na mashambulizi yake.

Mstari wa 15 anasungumzia maandalizi ya miguu kwa vita vya kiroho. Katika vita, wakati mwingine adui anaweka vizuizi hatari katika njia ya askari anayemfukuza. Wazo la maandalizi ya injili ya amani kama viatu unaonyesha kuwa tunahitaji kwenenda katika himaya ya Shetani, tukifahamu kuwa kutakuwa na mitego, na ujumbe wa neema ukiwa wa umuhimu mno kwa kushinda nafsi kwa Kristo. Shetani ana vizuizi vingi vimewekwa njiani ili vigeuze uenezaji wa injili.

Ngao ya imani inayosungumziwa katika mstari wa 16 hufanya shauku ya Shetani kwa waumini wa Mungu na neno lake kuwa bila ufanisi. Imani yetu - ambayo Kristo ndiye "mwanzilishi na mdumishaji " (Waebrania 12:2) - ni kama ngao ya dhahabu, thamani , imara, na dhabiti.

Chapeo la wokovu katika mstari wa 17 ni ulinzi kwa ajili ya kichwa, kutunza sehemu muhimu za mwili. Tunaweza kusema kwamba njia yetu ya kufikiri inahitaji kuhifadhi. Kichwa ni kiti cha akili, ambayo, wakati kimemiliki uhakika wa injili ya matumaini ya uzima wa milele, hakiwezi kupokea mafundisho ya uongo au kupisha njia ya majaribu ya Shetani. Mtu ambaye hajaokoka hana tumaini la kuzuilia mbali makonde ya mafundisho ya uongo kwa sababu yeye hana chapeo la wokovu na akili yake haina uwezo wa kutambua kati ya ukweli wa kiroho na udanganyifu wa kiroho.

Mstari wa 17 hujitafsiri wenyewe kama wa maana ya Upanga wa Roho -ni neno la Mungu. Wakati vipande vingine vyote vya silaha za kiroho ni wa kujihami katika asili, Upanga wa Roho ndio silaha ya kinga pekee katika silaha zote za Mungu. Inazungumzia utakatifu na nguvu ya neno la Mungu. Silaha za kiroho kuu hasiwezi wazika. Katika majaribu ya Yesu jangwani, neno la Mungu mara zote lilikua jibu la kishindo kwa Shetani. Ni baraka ya aina gani kwamba neno hilo linapatakina kwa ajili yetu!

Katika aya ya 18, tunaambiwa kuomba katika Roho (yaani, kwa nia ya Kristo, na moyo wake na vipaumbele vyake) kwa kuongeza amevaa silaha zote za Mungu. Hatuwezi kupuuzwa sala, kwa vile ni njia ambayo sisi hupata nguvu za kiroho kutoka kwa Mungu. Bila maombi, bila kumtegemea Mungu, juhudi zetu katika vita vya kiroho ni tupu na potovu. Silaha zote za Mungu -ukweli , haki, injili, imani, wokovu, neno la Mungu, na sala ni zana Mungu ametupa, kwa njia ambayo tunaweza kuwa na ushindi kiroho, na kushinda mashambulizi na majaribu ya Shetani.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Ni nini maana ya silaha zote za Mungu?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries