settings icon
share icon
Swali

Je! Ni kwa nini ninakabiliwa na matokeo ya dhambi ya Adamu na huku sikulila tunda?

Jibu


Biblia inasema, “Kwa hiyo kama vile dhambi ilivyoingia ulimwenguni kupitia kwa mtu mmoja, na kupitia dhambi hii mauti ikawafikia watu wote, kwa sababu wote wamefanya dhambi” (Warumi 5:12). Ilikuwa kupitia Adamu kwamba dhambi iliingia ulimwenguni. Adamu alipofanya dhambi, alikufa mara moja kiroho-uhusiano wake pamoja na Mungu ulivunjika-na pia akaanza kufa kimwili-mwili wake ulianza kuzeeka na kufa. Tangu wakati huo, kila mtu aliyezaliwa amerithi asili ya dhambi ya Adamu na kuteseka kwa matokeo yale yale ya kifo cha kiroho na kimwili.

Tunazaliwa kimwili tukiwa hai lakini wafu kiroho. Hii ndiyo sababu Yesu alimwambia Nikodemo, “huna budi ‘kuzaliwa mara ya pili” (Yohana 3:7). kuzaliwa kimwili hutupatia asili ya dhambi ya kibnadamu; kuzaliwa upya kiroho hutupatia asili mpya, “ ulioumbwa sawasawa na mfano wa Mungu katika haki yote na utakatifu” (Waefeso 4:24).

Huenda isionekane kuwa haki kutwikwa mzigo wa asili ya dhambi ya Adamu, lakini inaambatana na vipengele vingine vya uenezaji wa binadamu. Tunarithi baadhi ya sifa za kimwili kama vile rangi ya macho kutoka kwa wazazi wetu, na pia tunarithi baadhi ya sifa zao za kiroho. Kwa nini kupitishwa kwa sifa za kiroho kunapaswa kuwa tofauti na uenezaji wa tabia za kimwili? Tunaweza kulalamika kuhusu kuwa na macho ya kahawia tulipotaka ya samawati, lakini rangi ya macho yetu ni suala la jeni. Vivyo hivyo, kuwa na asili ya dhambi ni suala la “jeni za kiroho”; ni sehemu ya asili ya maisha.

Hata hivyo, Biblia inasema sisi ni watenda dhambi kwa matendo na vilevile katika asili. Sisi ni wenye dhambi mara mbili: tunatenda dhambi kwa sababu sisi ni wenye dhambi (chaguo la Adamu), na sisi ni wenye dhambi kwa sababu tunatenda dhambi (chaguo letu). “kwa kuwa wote wametenda dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mungu” (Warumi 3:23). Sisi tuna uwezo zaidi wa kutenda dhambi; tunashiriki katika dhambi. “Lakini kila mtu hujaribiwa wakati anapovutwa na kudanganywa na tamaa zake mwenyewe zilizo mbaya” (Yakobo 1:14). Dereva anaona kibao kinachoonyesha kiwango cha mbio; na anaamua kuzidi kiwango hicho; anapata tikiti. Huyo dereva hawezi kumlaumu Adamu kwa kosa hilo.

“Sikula tunda.” Ni kweli, lakini Maandiko yanasema kwamba sisi, kibinafsi na kama jamii ya wanadamu, sote tuliwakilishwa na Adamu. “Katika Adamu watu wote wanakufa” (1 Wakorintho 15:22). Mjumbe/mwanadiplomasia anayezungumza katika Umoja wa Mataifa anaweza kufanya au kusema mambo ambayo wananchi wake wengi hawakubalini nayo, lakini yeye bado ni mjumbe-yeye ndiye mwakilishi anayetambulika rasmi wa nchi hiyo.

Kanuni ya kitheolojia ya mwanamume anayewakilisha wazao wake inaitwa “uongozi wa shirikisho.” Adamu alikuwa mwanadamu wa kwanza kuumbwa. Alisimama kama “kichwa” cha kizazi cha wanadamu. Aliwekwa kwenye bustani ili atende sio kwa ajili yake tu bali kwa ajili ya uzao wake wote. Kila mtu aliyewahi kuzaliwa tayari alikuwa “katika Adamu,” akiwakilishwa naye. Wazo la uongozi wa shirikisho linafunzwa wazi mahali pengine katika Maandiko: “Mtu anaweza hata kusema kwamba Lawi, ambaye hupokea sehemu ya kumi, alitoa hiyo sehemu ya kumi kupitia kwa Abrahamu, kwa sababu Melkizedeki alipokutana na Abrahamu, Lawi alikuwa bado katika viuno vya baba yake wa zamani” (Waebrania 7:9-10). Lawi alizaliwa karne nyingi baada ya Abrahamu kuishi, lakini Lawi alimlipa Melkizedeki sehemu ya kumi “kupitia Abrahamu.” Ibrahimu alikuwa kiongozi wa shirikisho la watu wa Kiyahudi, na matendo yake yaliwakilisha makabila kumi na mawili yajayo na ukuhani wa Walawi.

“Sikula tunda.” Kweli, lakini dhambi zote zina matokeo zaidi ya kosa la mwanzo. “Hakuna mwanadamu anayeweza kuishi pekee yake kama kisiwa,” John Donne aliandika. Ukweli huu unaweza kutumika kiroho. Dhambi ya Daudi na Bathsheba ilimwathiri Daudi, bila shaka, lakini pia ilikuwa na matokeo mabaya ambayo yaliathiri Uria, mtoto wa Daudi ambaye hakuwa amezaliwa, familia yote ya Daudi, taifa zima, na hata maadui wa Israeli (2 Samweli 12:9-14). dhambi daima ina madhara mabaya kwa wale wanaotuzunguka. Mawimbi ya dhambi kuu ya Adamu bado yanashuhudiwa.

“Sikula tunda.” Kweli, haukuwepo kimwili katika Bustani ya Edeni ukiwa na maji ya tunda lililokatazwa yakiacha doa katika pembe za kinywa chako cha hatia. Lakini Biblia yaonekana kuonyesha kwamba, kama ungalikuwa huko badala ya Adamu, ungefanya jambo lilelile alilofanya. Kama vile wanavyosema kuwa tunda la tofaa halianguki mbali na mti wake.

Iwapo tunafikiri kuwa ni “haki” kuhusishwa na dhambi ya Adamu haijalishi. Mungu anasema kwamba tumerithi asili ya dhambi ya Adamu, na sisi ni nani ili kubishana na Mungu? Ziadi ya hayo, sisi ni wenye dhambi kwa haki yetu wenyewe. Dhambi yetu wenyewe labda inamfanya Adamu akilinganishwa aonekane mtakatifu.

Hii ndio habari njema: Mungu anawapenda wenye dhambi. Kwa hakika, amechukua hatua kushinda asili yetu ya dhambi kwa kumtuma Yesu kulipia dhambi zetu na kutupa haki yake (1 Petro 2:24). Yesu alichukua kifo ambacho kilikuwa adhabu yetu juu yake, “ili sisi tupate kufanywa haki ya Mungu kwake yeye” (2 Wakorintho 5:21). Angalia maneno “ndani yake.” Sisi ambao hapo awali tulikuwa ndani ya Adamu tunaweza sasa kuwa ndani ya Kristo kwa imani. Kristo ndiye kichwa chetu kipya, na “katika Kristo wote watafanywa hai” (1 Wakorintho 15:22).

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Ni kwa nini ninakabiliwa na matokeo ya dhambi ya Adamu na huku sikulila tunda?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries