settings icon
share icon
Swali

Je, Siku ya Bwana ni nini?

Jibu


Siku ya Bwana (jinsi ilivyotajwa kutoka siku ya Bwana) ni Jumapili. Neno Siku ya Bwana limetumiwa mara moja tu katika Maandiko. Ufunuo 1:10 inasema, "Nalikuwa katika Roho, siku ya Bwana; nikasikia sauti kuu nyuma yangu, kama sauti ya baragumu." Kwa kuwa mtume Yohana hafafanui maana ya "Siku ya Bwana," tunaweza kuchukulia kwamba aliowalenga, Wakristo wa karne ya kwanza, tayari walikuwa wamefahamu maneno hayo.

Wengine wamefikiri kwamba siku ya Bwana ni sawa na Sabato katika Agano Jipya. Siku ya sabato ilianzishwa na Mungu kwa ajili ya taifa la Isiraeli kuwakumbusha ukombozi wake kutoka Misri (Kumbukumbu la Torati 5:15). Sabato ilianza Ijumaa wakati wa jua kuzama na ikamalizika Jumamosi wakati wa jua kuzama na ilipaswa kuwa siku ya mapumziko kamili kutokana na kazi zote, ikiashiria mfano wa kupumzika kwa Muumba siku ya saba (Mwanzo 2: 2-3, Kutoka 20:11, 23:12). Sabato ilikuwa ishara maalum kwa Waisraeli kwamba walikuwa wameteuliwa kuwa wafuasi wa Mungu Mkuu. Kwa kuzingatia Sabato kuliwasaidia kutofautishwa kutoka kwa mataifa yaliyowazunguka. Hata hivyo, hakuna mahali popote katika Maandiko Sabato imerejelewa kuwa siku ya Bwana. Jina Sabato lilikuwa bado linatumika miongoni mwa jamii ya Wayahudi katika nyakati za Agano Jipya na limerejelewa hivyo na Yesu na mitume (Mathayo 12: 5; Yohana 7:23; Wakolosai 2:16).

Jumapili ilikuwa siku ambayo Yesu Kristo alifufuka kutoka kwa wafu, kitendo ambacho milele kiliutenganisha Ukristo na dini nyingine yoyote (Yohana 20: 1). Tangu wakati huo, waumini wamekusanyika siku ya kwanza ya juma kusherehekea ushindi wake juu ya dhambi na kifo (Matendo 20: 7; 1 Wakorintho 16: 2). Ingawa siku ya sabato ilichaguliwa na Mungu kama siku takatifu, Yesu alionyesha kuwa alikuwa Bwana wa Sabato (Mathayo 12: 8). Yesu alisema kuwa hakukuja kukomesha bali kutimiza Sheria yote. Kulinda na kufuata sheria hakuwezi takaza mtu yeyote; tu kwa njia ya Yesu, mwanadamu mwenye dhambi atasemwa kuwa mwenye haki (Warumi 3:28). Paulo anasisitiza ukweli huu katika Wakolosai 2: 16-17 anapoandika, "Basi, mtu asiwahukumu ninyi katika vyakula au vinywaji, au kwa sababu ya sikukuu au mwandamo wa mwezi, au sabato; mambo hayo ni kivuli cha mambo yajayo; bali mwili ni wa Kristo."

Siku ya Bwana hakika inafikiriwa kuwa Jumapili, lakini sio sawasawa moja kwa moja na Sabato ya Kiyahudi — kumaanisha, Jumapili sio "Sabato ya Kikristo." Ingawa tunapaswa kutenga siku ya kupumzika na kumheshimu Bwana aliyekufa na kufufuka kwa ajili yetu, hatuko chini ya Sheria (Warumi 6: 14-15). Kama wafuasi wa Yesu waliookoka, tuko huru kumwabudu Yeye siku yoyote ambayo dhamiri yetu huamua. Warumi 14 inatoa ufafanuzi wazi wa jinsi Wakristo wanapaswa kuendesha maeneo hayo tata ya utumishi. Mistari ya 5 na 6 inasema, "Mtu mmoja afanya tofauti kati ya siku na siku, mwingine aona siku zote kuwa sawasawa. Kila mtu na athibitike katika akili zake mwenyewe. Yeye aadhimishaye siku, huiadhimisha kwa Bwana; naye alaye, hula kwa Bwana, kwa maana amshukuru Mungu; tena asiyekula, hali kwa Bwana, naye pia amshukuru Mungu. "

Baadhi ya Wayahudi wa Kimasihi wanataka kuendelea na siku ya sabato kama takatifu kwa sababu ya urithi wao wa Kiyahudi. Wakristo wengine wa Mataifa hujiunga na ndugu zao na dada zao wa Kiyahudi katika kutunza Sabato kama njia ya kumheshimu Mungu. Kumuabudu Mungu siku ya sabato kumekubaliwa-tena, siku ya juma si suala muhimu zaidi-lakini moyo wa motisha nyuma ya uamuzi huo ni muhimu. Ikiwa uhalali au kuzingatia na kufuata sheria huhamasisha uamuzi wa kuzingatia Sabato, basi uamuzi huo haufanywi kutoka kwa moyo ulio msafi (Wagalatia 5: 4). Wakati mioyo yetu ni safi mbele ya Bwana, tuko huru kumwabudu siku ya Jumamosi (Sabato) au Jumapili (siku ya Bwana). Mungu anapendezwa sawa na siku zote mbili.

Yesu alionya dhidi ya uhalali wakati alipomnukuu Isaya nabii: "Watu hawa wananiheshimu kwa midomo yao, lakini mioyo yao iko mbali nami. Wananiabudu bure; mafundisho yao ni sheria za kibinadamu tu "(Mathayo 15: 8-9; tazama Isaya 29:13). Mungu hajali nia ya kutunza mila, sheria, au mahitaji. Anataka mioyo iliyo moto na upendo wake na neema siku ya Sabato, siku ya Bwana, na kila siku nyingine (Waebrania 12: 28-29, Zaburi 51: 15-17).

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, Siku ya Bwana ni nini?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries