settings icon
share icon
Swali

Je! Inamaanisha nini kuwa si vyema mwanaume kuwa peke yake (Mwanzo 2:18)?

Jibu


Mwanzo 1:27 inasimulia kwamba Mungu aliumba wanadamu wakiwa na jinsia mbili; mwanamume na mwanamke. Mwishoni mwa juma la uumbaji, Mungu anatangaza kwamba uumbaji wake wote ulikuwa mzuri sana (Mwanzo 1:31). Kwa sababu Mungu alibuni umoja wa kijinsia na kwa sababu Aliuita kuwa mzuri sana, ni wazi kutoka kwa simulizi ya Mwanzo kwamba tofauti kati ya mwanamume na mwanamke ni muhimu. Lakini huenda tusitambue ni muhimu kiasi gani hadi tusome maelezo zaidi, yaliyoletwa karibu katika simulisi ya jinsi Mungu hasa alivyomuumba mwanamume na mwanamke wa kwanza katika Mwanzo 2. Ni katika muktadha huo ambapo Mungu anatangaza si vyema kwamba mwanamume awe peke yake (Mwanzo 2:18). Hii ni mara ya kwanza kwa jambo lolote kusemwa kuwa si zuri. Jambo baya la kwanza kuwahi kurekodiwa ni kwamba mwanamke hakuwa kwenye eneo la tukio bado! Hilo laonyesha wazi jinsi mwanamke alivyo wa maana katika mpango wa Mungu.

Mwanzo 2:7 inaeleza jinsi Mungu alivyomuumba Adamu kutoka katika mavumbi ya ardhi na kumpulizia pumzi ya uhai, na kumfanya Adamu kuwa hai. Baada ya Adamu kuumbwa, Mungu alimweka katika bustani ya Edeni yenye majani mengi (Mwanzo 2:15). Mungu alikuwa amepanga kwamba Adamu angelima na kuitunza bustani hiyo. Kufikia hapo, Adamu bado alikuwa mwanadamu pekee aliyekuwepo, na kazi ya uumbaji ya Mungu ilikuwa bado haijakamilika. Mungu anakubali kutokamilika kwa kazi—ingawa Alikuwa Ameumba vyote isipokuwa kitu kimoja, upungufu uliosalia ulikuwa mkubwa. Mungu anasema kwamba haikuwa vyema kwa mtu huyo kuwa peke yake (Mwanzo 2:18).

Hapo awali, Mungu alikuwa amesema kwamba angewaumba wanadamu na kwamba wangetawala viumbe vyake vingine (Mwanzo 1:26). Mungu alitumia kiwakilishi cha wingi (wao), kumaanisha kwamba kungekuwa na zaidi ya mtu mmoja tu. Katika mpango ambao Mungu alikuwa amepanga, mtu mmoja hangeweza kufanya kazi hiyo. Baada ya kuumbwa kwa Adamu Mungu alisema kwamba Adamu hakutosha. Haikuwa vyema—haikutimiza mpango Wake—kwa Adamu kuwa peke yake. Katika Mwanzo 1:27, Mungu alipoumba wanadamu aliwaumba wawe mwanamume na mwanamke.

Katikati ya mradi huo, katika siku ya sita, Mungu anabainisha kuwa kazi hiyo ilikuwa haijakamilika, na kilichotakiwa kukamilika ili kuhakikisha kazi hiyo ilikuwa nzuri ni kwamba Mungu atengeneze kinyume chake ambacho kingeweza kumsaidia Adamu kutimiza nia ya Mungu kwa wanadamu (Mwanzo 2:18). Mwanaume moja hakuweza kufanya hivyo peke yake. Lakini kabla Mungu hajakutana na hitaji la Adamu la mwanamke, alimwonyesha Adamu kwamba kila aina ya mnyama alikuwa na mwenzake—kulikuwa na dume na jike katika ulimwengu wa wanyama pia (mwanzo 2:20), lakini hadi hapo Adamu alikuwa bado peke yake. Simulizi la Mwanzo halituambii ni kwa nini Mungu alimwonyesha Adamu upungufu kabla ya kuutatua, lakini ingekuwa na maana kwamba Adamu alihitaji kuelewa jinsi mwanamke mwezake angekuwa muhimu—bila yeye, mpango mzima wa Mungu kwa ajili ya kazi ya wanadamu ungeshindwa. Hakungekuwa na “wao” wa kutawala uumbaji jinsi Mungu alivyokuwa amekusudia.

Kwa hiyo Mungu alimfanya Adamu kulala na kumfanyia upasuaji wa aina yake, akatoa ubavu wake mmoja na kuponya kidonda (Mwanzo 2:21). Kutoka kwa ubavu huo Mungu aliumba mwanamke wa kwanza (Mwanzo 2:22). Mungu alipomleta kwa Adamu, Adamu alitambua thamani yake (labda kwa sababu alionyeshwa kwanza kwamba alikuwa peke yake). Adamu alielewa kwamba alitoka kwake na kwamba walikuwa wameunganishwa kwa njia ya kipekee (Mwanzo 2:23). Ingawa walikuwa sawa kwa thamani, walikuwa tofauti katika muundo. Mungu alikuwa amekamilisha kazi Yake ya uumbaji, mwanamke akiwa ndiye kipigo cha mwisho, na viambato vya kimsingi vya jinsia, kujamiiana, na ndoa vilianzishwa (Mwanzo 2:24-25). Mungu alikuwa amepanga mwanamume na mwanamke wawe sawa nab ado wawe tofauti sana. Kwa namna Fulani walikuwa kinyume, na wote wawili walihitajika ili kutimiza mpango Wake.

Simulizi ya Mwanzo ya asili ya mwanamume na mwanamke ni sahihi kihistoria kulingana na waandishi wengine wa Biblia (kwa mfano, Paulo anajadili sana Adamu na Hawa na athari zao kwa wale ambao wangekuja baada yao katika vifungu kama Warumi 5 na 1 Timotheo 2). Katika siku za hivi majuzi, hata hivyo, historia na kwa hivyo athari za muundo wa wiki ya uumbaji zimezidi kutiliwa shaka. Jamii zinapozidi kuacha kumtambua Mungu kuwa Muumba wao, wao pia huacha kutambua ubunifu wa Mbunifu. Moja ya matokeo ya kuondoka huko ni kuongezeka kwa mkanganyiko wa kijinsia. Kadri tunavyozidi kuzoea asili na muundo wetu, tunaweza kusahau utambulisho wetu na kutafuta kutengeneza njia yetu wenyewe badala ya kutimiza mpango Wake kwa ajili yetu. Ingawa aina hiyo ya kutomtegemea Mungu huenda ikasikika kuwa yenye kupendeza kwa njia fulani, katika kutafuta kijitegemea bila Muumba wetu na mpango Wake tunaweza kupoteza kabisa uwezo wa kutambua Yeye alituumba na kile Alichotuumba tufanye. Ni bora zaidi kutambua uzuri wa uumbaji Wake na kufuata mpango Wake kwa ajili yetu—kufuata utimilifu katika kuwa vile Alituumba kuwa na kukumbatia mpango Wake.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Inamaanisha nini kuwa si vyema mwanaume kuwa peke yake (Mwanzo 2:18)?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries