settings icon
share icon
Swali

Je, Sheria nne za kiroho ni zipi?

Jibu


Sheria nne za kiroho ni njia au mfumo wa kumshuhudia jirani yako habari njema ya wokovu upatikanao kwa kumwamini Yesu Kristo. Ni mfumo mwepesi unao pangilia vidokezo muhimu vya injili katika sehemu kuu nne.

Kidokezo cha kwanza kati ya sheria hizi nne za kiroho ni, ‘Mungu anakupenda na ana mpango mwema juu ya maisha yako.’ Yohana 3:16 yatwambia, “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele” (TMP). Yohana 10:10 yatupa sababu ya kuja kwake Yesu, “Mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele” (TMP). Lakini je, ni kitu gani kinachotutenga na upendo wa Mungu? Ni kitu gani kinacho tupinga kupata uzima ulio tele?

Kidokezo cha pili kati ya sheria hizi nne za kiroho ni, ‘Wanadamu wote wamenajisika kwasababu ya dhambi na hivyo basi kutengwa na Mungu. Kwa sababu hiyo, hatuwezi kamwe kuufahamu huo mpango mwema alio nao Mungu juu ya maisha yetu.’ Warumi 3:23 inatuhakikishia habari hii, “Kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu” (TMP). Warumi 6:23 inatupatia madhara ya dhambi, “Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti” (TMP). Mungu alituumba ili tupate kuwa na ushirika naye. Lakini, mwanadamu alileta dhambi ulimwenguni, na kusababisha atengwe na Mungu. Tumevuruga ushirika wetu na Mungu ambao Yeye alikusudia tuwe nao. Lakini je, suluhisho letu ni nini?

Kidokezo cha tatu kati ya sheria hizi nne za Kiroho ni, ‘Yesu Kristo pekee ndiye ondoleo letu la dhambi mbele za Mungu. Kupitia kwa Yesu Kristo, tunaweza kusamehewa dhambi zetu na kurudisha ushirika mkamilifu mbele za Mungu.’ Warumi 5:8 yasema, “Bali Mungu aonyesha pendo lake yeye mwenyewe kwetu sisi, kwa kuwa Kristo alikufa kwa ajili yetu, tulipokuwa tungali wenye dhambi” (TMP). 1 Wakorintho 15:3-4 inatufahamisha kinachotupasa kujua na kuamini ili tupate kuokoka, “……ya kuwa Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu, kama yanenavyo maandiko, yakuwa alizikwa; ya kuwa alifufuka siku ya tatu, kama yanenavyo maandiko….” (TMP). Yesu mwenyewe akiri ya kwamba yeye ndiye njia ya pekee ya wokovu katika Yohana 14:6, “Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi” (TMP). Lakini je, ninawezaje kupata zawadi hii kuu ya wokovu?

Kidokezo cha nne kati ya sheria hizi nne za kiroho ni, ‘Ni sharti tuweke imani yetu ndani ya Yesu Kristo kama mwokozi ili tukaweze kupokea zawadi hii ya wokovu na tupate kujua huo mpango mwema wa Mungu juu ya maisha yetu’. Yohana 1:12 inatuelezea hivi, “Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu“ (TMP). Matendo 16:31 inazungumzia kwa ufasaha zaidi, “Mwamini Bwana Yesu nawe utaokoka!” (TMP). Twaweza okolewa kwa neema peke yake, kwa njia ya imani pekee, ndani ya Yesu Kristo pekee (Waefeso 2:8-9).

Ukiwa unataka kumwamini Yesu Kristo kama mwokozi wako, sema maneno yafuatayo kwa Mungu. Kusema maneno haya hayatakuokoa, lakini itawezekana kwa kumwamini Kristo! Ombi hili ni njia ya kumwelezea Mungu imani yako kwake na kumshukuru kwa kukupea wokovu. “Mungu, ninajua yakwamba nimefanya dhambi kinyume chako na ninastahili adhabu. Lakini Yesu Kristo akaichukua adhabu niliyo stahili ili kwa kumwamini yeye, nipate kusamehewa. Naweka imani yangu Kwako pekee ili niokolewe. Ahsante kwa neema yako kuu na kwa msamaha-zawadi ya uzima wa milele! Amina!”

Je, umefanya uamuzi kwa Kristo kwa kile ulicho soma hapa? kama ndiyo, tafadhali bonyeza kwa “Nime mkubali Kristo hivi leo” hapo chini.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, Sheria nne za kiroho ni zipi?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries