settings icon
share icon
Swali

Je! Sanamu ya mnyama ni gani?

Jibu


Kitabu cha Ufunuo kina maono tabiri ya Wanyama wawili wakiibuka toka baharini na ardhini ili wautawale ulimwengu. Ni katika maono haya (katika Ufunuo 13) ambapo kwamba sanamu ya mnyama imetajwa mara ya kwanza.

Mnyama wa kwanza ni mnyama wa pembe kumi, vichwa saba aliyepewa mamlaka na yule joka (Ufunuo 13:1-2). Mojawapo ya vichwa alikwisha pata jeraha la mauti lakini amepona (Ufunuo 13:3). Mnyama huyo anakufuru dhidi ya Mungu na anawatesa sana watu wa Mungu duniani (Ufunuo 13:5-7). Hatawali dunia tu pekee, bali pia anapokea ibada ya wale wanaoishi duniani (Ufunuo 13:4, 7-8). Mnyama wa kwanza ni mfano taswira wa Mpinga Kristo, na joka ni Shetani (rejelea Ufunuo 12:9).

Mnyama wa pili ni kiumbe mwenye pembe mbili, mwenye tabia danganyifu ambaye anashiriki mamlaka na mnyama wa kwanza (Ufunuo 13:11-12). Jukumu la mnyama wa pili ni kusababisha kila mtu amwabudu mnyama wa kwanza. Mnyama wa pili anapoudanganya ulimwengu na miujiza, anaamurisha kila mtu “wasimamishe sanamu kwa heshima ya yule mnyama aliyekuwa amejeruhiwa kwa upanga lakini akaishi” (Ufunuo 13:14). Pia atahitaji kila mtu apokee alama ya mnyama katika uso na katika mkono wa kuume (Ufunuo 13:16-17). Mnyama wa pili na ishara taswira ya nabii wa uwongo.

Biblia haitoi maelezo ya kina kuhusu sanamu ya mnyama. Hata hivyo, tunajua hili: kwamba nabii wa uwongo atakuwa na ”Akapewa uwezo wa kuipa pumzi ile sanamu ya yule mnyama wa kwanza, ili iweze kusema na kuwasababisha wale wote waliokataa kuiabudu hiyo sanamu kuuawa” (Ufunuo 13:15). Hii sanamu ya mnyanya wa kwanza inayopumua na kuongea basi itadai kuabudiwa. Yeyote atakayekaidi kuiabudu sanamu ya mnyama atauawa. Ufunuo 20:4 inasema kwamba njia ya kuuawa kwa wale watakao kaidi kuiabudu sanamu ya mnyama ni kwamba watakatwa kichwa. Kuna uwezekano kuwa sanamu ya mnyama ni ”chukizo linalo sababisha uharibifu” katika hekalu lililo jengwa upya ambalo limetajwa katika Danieli 9:27 na Mathayo 24:15.

Je! ni nini haswa hali asili kamili ya sanamu ya mnyama? Biblia haisemi chochote. Dhanilo la zamani lilikuwa kwamba, sanamu ya mnyama ni kijisanamu kilichopewa mwonekano wa uhai. Pamoja na kujibuka kwa maarifa ya ufundi (teknolojia) mapya kunaibuka nadharia mpya hii ikiwa ni pamoja na utaalamu wa kubadili chombo na kuwa sura nyingine, kiumbe kilicho na uasili na sehemu sayansi, mseto binadamu-wanyama, au kuumbwa kwa wanadamu bila kujamiana. Vyovyote vile itakavyokuwa, sanamu ya mnyama ndio kitovu cha ibada katika “dini ya mnyama” katika sehemu ya pili ya kipindi cha dhiki. Kusujudia sanamu ya mnyama ni jinsi watu wa uliwengu waliodanganywa watamwabudu “mtu wa kuasi” (2 Wathesalokine 2:3), ambaye atajiinua kuwa mungu katika hekalu la Yerusalemu

Wale wasio iabudu sanamu ya mnyama watapata dhadhabu ya Mpinga Kristo. Lakini kwa watakaoiabudu sanamu ya mnyama watapatwa na ghadhabu ya Mungu, ambayo ni kali mno: “Kama mtu yeyote anamwabudu huyo mnyama na sanamu yake … yeye pia atakunywa mvinyo wa hasira kali ya Mungu ambayo imemiminwa katika kikombe cha ghadhabu yake … Nao moshi wa mateso yao hupanda juu milele na milele. Hakuna mapumziko, mchana wala usiku, kwa wale wamwabuduo huyo mnyama na sanamu yake, au kwa yeyote anayepokea chapa ya jina lake” (Ufunuo 14:9-11). Hukumu ya kwanza ya bakuli la Mungu italenga hasa wale wanaoiabudu sanamu ya mnyama: “Malaika wa kwanza akaenda akalimwaga hilo bakuli lake juu ya nchi. Majipu mabaya yenye maumivu makali yakawapata wale watu wote waliokuwa na chapa ya yule mnyama na walioabudu sanamu yake” (Ufunuo 16:2).

Wale watakaoasi kupiga goti kwa Mpinga Kristo na sanamu ya mnyama wanaweza kuteswa duniani, lakini watatunukiwa mbinguni: “Nikaona kile kilichoonekana kama bahari ya kioo iliyochanganyikana na moto. Kando ya hiyo bahari, walikuwa wamesimama wale watu waliomshinda yule mnyama na sanamu yake pamoja na tarakimu ya jina lake. Mikononi mwao walikuwa wameshika vinubi walivyopewa na Mungu” (Ufunuo 15:2-3). Sanamu ya mnyama ndio ya kwanza na kitengo kuu katika ufalme wa Shetani, lakini haitadumu. Biblilia inasisitiza miezi arobaini na miwili, ama miaka mitatu na nusu, kwamba Mpinga Kristo atakuwa na ushawishi ulimwenguni (Ufunuo 13:5). Baada ya hapo, sanamu ya mnyama itaharibiwa, Minyama hiyo miwili itatupwa katika ziwa la moto (Ufunuo 19:20), Shetani atafungwa (Ufunuo 20:1-3), na Bwana yesu ataanzisha ufalme kamilifu usio na mwisho (Isaya 9:7; Luka 1: 32-33).

English

Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Sanamu ya mnyama ni gani?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries