settings icon
share icon
Swali

Kuna uhusiano gani kati ya sala na kufunga?

Jibu


Ingawa uhusiano kati ya sala na kufunga haijaelezewa hasa katika maandiko, mfumo wa kawaida ambao huunganisha hizo mbili unaonekana kwa kila tukio lolote la maombi na kufunga ambao umeandikwa katika Biblia. Katika Agano la Kale, inaonekana kwamba kufunga na sala ilikuwa na maana ya haja na utegemezi, na / au kutojiweza katika shida halisi au msiba unaotarajiwa. Maombi na kufunga yamewekwa pamoja katika Agano la Kale katika nyakati za maombolezo, toba, na / au haja ya kina ya kiroho.

sura ya kwanza ya Nehemia inaelezea Nehemia akiomba na kufunga, kwa sababu ya taabu yake ya kina juu ya habari kwamba Yerusalemu ulikuwa ukiwa. Siku zake mingi za maombi zilikuwa na sifa ya machozi, kufunga, kukiri kwa niaba ya watu wake, na malilio kwa Mungu kwa huruma. Hivyo yalikuwa makali yake ya kumwagwa hisia zake takribani isikubalike kuwa angeweza "kuchukua mapumziko" katikati mwa sala kama hizo ili ale na kunywa. Uharibifu ulioipata Yerusalemu pia ulimfanya Danieli kuchukua mtindo huo: "Nikamwelekezea Bwana Mungu uso wangu, ili kutaka kwa maombi, na dua, pomoja na kufunga, na kuvaa nguo za magunia na majivu" (Danieli 9:3). Kama Nehemia, Danieli alifunga na kuomba kwamba Mungu aone huruma juu ya watu, akisema, "Tumefanya dhambi, tumefanya ukaidi, tumetenda maouvu, tumeasi, naam hata kwa kuyaacha maagizo yako na hukumu zako" (mstari wa 5).

Katika matukio kadhaa katika Agano la Kale, kufunga kunahusishwa na maombi ya kuombea. Daudi aliomba na kufunga juu ya mtoto wake mgonjwa (2 Samweli 12:16), akilia kwa bidii mbele za Bwana katika maombezi (vv. 21-22). Esta alimsihi Mordekai na Wayahudi kufunga kwa ajili yake alipokuwa akipanga mbele ya mumewe mfalme (Esta 4:16). Ni wazi, kufunga na kuomba sina uhusiano wa karibu.

Kuna mifano ya sala na kufunga katika Agano Jipya, lakini haijahusishwa na toba au kukiri. Nabii Anna "haondoki katika hekalu, ila huabudu usiku na mchana kwa kufunga na kuomba" (Luka 2:37). Katika umri wa miaka 84, sala yake na kufunga ilikuwa sehemu ya huduma yake kwa Bwana katika hekalu lake alipikuwa akingoja Mwokozi ahadi ya Israeli. Pia katika Agano Jipya, kanisa la Antiokia lilikuwa linafunga kuhusiana na ibada yao wakati Roho Mtakatifu alinena nao kuhusu kuwatia wakuvu Barnaba na Saulo kwa kazi ya Bwana. Katika hatua hiyo, wao waliomba na kufunga, wakawawekea mikono hao wawili na kuwatuma. Hivyo, tunaona mifano hii ya maombi na kufunga kama sehemu ya ibada yao kwa Bwana na kutafuta neema zake. Hakuna mahali popote, hata hivyo, kuna dalili yoyote kwamba Bwana anaweza kujibu maombi kama yameandamana na kufunga. Badala yake, kufunga pamoja na sala kunaonekana kuonyesha ukweli wa watu kuomba na asili muhimu ya hali ambayo wanajikuta.

Jambo moja li wazi: theolojia ya kufunga ni theolojia ya vipaumbele ambayo kwayo waumini hupewa nafasi ya kujieleza katika namna isiyo ya mgawanyiko na ibada ya kina kwa Bwana na kwa matatizo ya maisha ya kiroho. Ibada hii itadhihirishwa kwa kujinyima kwa muda mfupi mambo ya kawaida na mazuri kama chakula na kinywaji, ili kufurahia wakati wa ushirika na Baba yetu bila kukatizwa. "Ujasiri wetu kuingia katika Patakatifu kwa damu ya Yesu" (Waebrania 10:19), ikiwa tunafunga au hatufungi, ni mojapo ya sehemu ya kufurahisha ya hicho "kitu bora" ambacho ni chetu katika Kristo. Maombi na kufunga yasiwe ni mzigo au wajibu, lakini badala maadhimisho ya wema wa Mungu na huruma kwa watoto wake.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Sala na kufunga ni nini?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries