Swali
Ni kwa jinsi gani saikolojia inafanya kazi na ushauri nasaha wa Biblia?
Jibu
saikolojia ya kiduniai msingi wake ni kwa mafundisho ya wanasaikolojia wadadisi kama vile Sigmund Freud, Carl Jung, na Carl Rogers. Kibiblia, au nautetiki, ushauri nasaha, kwa upande mwingine, msingi wake kimraba uko katika neon la Mungu lililofunuliwa. Ushauri nasaha wa Biblia unaona maandiko kama ya kutosha kwa kuandaa mtoto wa Mungu kwa kila kazi njema (2 Timotheo 3:17). Washauri wa kibiblia hufundisha kwamba tatizo la kimsingi la mtu ni la kiroho kwa asili; Kwa hiyo, wanasaikolojia wanaomkana Mungu, ambao ni waliokufa kiroho wenyewe, hawana ufahamu halisi katika hali ya binadamu.
Katika hali ya kuhusiana, kwa kawaida kinachoitwa"ushauri nasaha wa Kikristo" ni tofauti na "ushauri nasaha wa Biblia" katika huo ushauri wa kikiristo mara nyingi unatumia saikolojia ya kidunia kuongezea kwa Biblia. Hii si kusema kwamba mshauri Mkristo si pia mshauri wa Biblia, lakini mara nyingi washauri wakristo ni Wakristo ambao huunganisha saikolojia ya kidunia katika ushauri nasaha wao. Washauri wa Biblia au nautetiki hukataa saikolojia ya kidunia jumla.
Saikolojia nyingi ni ya kibinadamu kiasili.ubinadamu wa Kidunia hukuza wanadamu kama kiwango cha juu cha ukweli na maadili na kukataa imani, isiyo ya dunia, na Biblia. Kwa hivyo, saikolojia ya kidunia ni jaribio la mtu kuelewa na kukarabati upande wa kiroho wa mtu bila kushauriana na au utambuzi wa kiroho.
Biblia inatangaza kwamba mwanadamu ni kiumbe cha kipekee cha Mungu, aliyefanya katika mfano wa Mungu (Mwanzo 1:26, 2: 7). Biblia waziwazi inahusika na uroho wa mtu, ikiwa pamoja na kuanguka kwake katika dhambi, matokeo ya dhambi, na mahusiano ya sasa ya mwanadamu na Mungu.
Saikolojia ya kidunia kwa msingi iko kwa mawazo kwamba mtu kimsingi ni mzuri na kwamba majibu kwa matatizo yake yako nafsini mwake mwenyewe . Biblia inajenga picha tofauti sana ya hali ya mtu. Mtu "kimsingi si mzuri"; yeye ni "mfu katika makosa na dhambi" (Waefeso 2: 1), na moyo huwa mdanganyifu kuliko vitu vyote, una ugonjwa wa kufisha; nani awezaye kuujua." (Yeremia 17: 9). Kwa hivyo, mshauri wa kibiblia kwa haraka anachukua mbinu tofauti: badala ya kutafuta ufumbuzi wa matatizo ya kiroho ndani ya akili ya mtu mwenyewe, yeye anatafuta ili kukabiliana na dhambi, kupata hekima kutoka juu (James 3:17), na kulitumia neon la Mungu kwa hali hiyo.
Washauri wa kibiblia, kama ilivyo kinyume na wanasaikolojia na baadhi ya washauri wakristo, wanaangalia Biblia pekee kama chanzo cha mbinu ya maelezo ya kina kwa ushauri nasaha (2 Timotheo 3: 15-17; 2 Petro 1: 4). Ushauri nasaha wa kibiblia una msimamo kwa kuruhusu Mungu ajisemee mwenyewe kupitia kwa neno lake. Ushauri nasaha wa kibiblia unatafuta kuhudumu upendo wa kweli wa Mungu aliye hai, upendo ambao unashughulikia dhambi na unazalisha utiifu.
Matibabu ya kisaikolojia ni mahitaji ya msingi. Mahitaji ya kujithamini, upendo na kukubalika, na umuhimu huelekea kutawala. Kama mahitaji haya yanaafikiwa , inaaminika, watu watakuwa na furaha, wapole, na waadilifu; kama mahitaji haya hayajaafikiwa, watu watakuwa wenye taabu,wenye chuki, na wabaya. Ushauri nasaha wa kibiblia unafundisha kwamba kuridhika kwa kweli na furaha kunaweza tu kupatikana katika uhusiano na Mungu na ukimbizaji wa kumcha Mungu. Hakuna kiasi cha matibabu ya kisaikolojia kinachoweza kumfanya mtu mchoyo asiwe mchoyo, kwa mfano, lakini mtumishi mtiifu wa Mungu ataridhika katika kutoa kwa furaha bila uchoyo (2 Wakorintho 9: 7).
Hivyo, jinsi gani saikolojia inafanya kazi na ushauri nasaha wa Biblia? Kwa kifupi, haufanyi. Saikolojia ya kidunia inaanza na kuishia kwa mtu na mawazo yake. Ushauri wa kweli wa Biblia unaelekeza wateja kwa Kristo na Neno la Mungu. Ushauri nasaha wa kibiblia ni shughuli ya wachungaji,zao la zawadi ya kiroho ya kutia moyo, na lengo lake si kujithamini balis utakaso.
English
Ni kwa jinsi gani saikolojia inafanya kazi na ushauri nasaha wa Biblia?