settings icon
share icon
Swali

Je, Shetani anapaswa kupata kibali cha Mungu kabla ya kutushambulia?

Jibu


Hakuna uthibitisho wowote wa kibiblia kwamba Shetani anahitaji ruhusa ya Mungu ili kuchukua hatua dhidi ya Wakristo kila wakati anapotaka kuwashambulia. Tunajua kwamba Shetani anahitaji ruhusa angalau nyakati fulani. Ayabu 1 inaonyesha kwamba shetani hakuweza kumtesa Ayubu bila ruhusa ya Mungu. Hata hivyo, tafakari hoja ya shetani mbele ya Mungu: “Je, wewe hukumjengea boma pande zote yeye na wa nyumbani mwake pamoja na kila kitu alicho nacho? Kazi za mikono yake umezibariki na hivyo makundi yake ya kondoo na mbuzi pamoja na ya wanyama yameenea katika nchi nzima” (Ayubu 1:10). Ni wazi kwamba shetani anamfahamu Ayubu vizuri na anajua ulinzi wa baraka ya kipekee kwa Ayubu kutoka kwa Mungu. Shetani angewezaje kujua ulinzi wa Ayubu, kama si yeye au wafuasi wake mapepo walikuwa wamejaribu kufanya mapenzi yao ya kinyume dhidi ya Ayubu? Shetani anachoomba hasa ni Mungu aondoe ulinzi kwa Ayubu, bila shaka, kwa kuomba ulinzi uondolewe, Shetani anatafuta kibali cha kumshambulia Ayubu. Je, shetani anafaa atafute kibali hicho kila mara anapotushambulia? Biblia haijasema kuhusu ilo.

Kifungu kingine muhimu ni Luka 22:31-32. Yesu anasema, “Simoni, Simoni, sikiliza, Shetani ameomba kuwapepeta ninyi wote kama ngano. Lakini nimekuombea wewe Simoni ili imani yako isishindwe, nawe ukiisha kunirudia, uwaimarishe ndugu zako.” Ni wazi katika kisa hiki Shetani alikuwa anamwomba Mungu ruhusa ili amjaribu Petro na wale wanafunzi wengine. Yesu anamwambia Petro kuwa amemwombea ili imani yake isitindike na awatie nguvu wale wanafunzi wengine majaribu yatakapoisha. Maana yake ni kwamba Petro na wale wengine wangepepetwa kwa njia yoyote ambayo Shetani alikusudia. Kwa hivyo Mungu aliruhusu wanafunzi wake wateswe kwa kiwango fulani, lakini Alikuwa na kusudu kuu zaidi akilini- kuwatia nguvu wote.

Katika Ayubu 38:11 Mungu anasema kwamba anazuia mawimbi ya bahari: “niliposema, ‘Unaweza kufika mpaka hapa wala si zaidi; hapa ndipo mawimbi yako yenye kiburi yatakapokomea’?.” Vivyo hivyo, inaonekana kwamba kuna mipaka na sheria ambazo Shetani lazima azitii. Anaweza kuenda mbali zaidi lakini si sana. “Mwe na kiasi na kukesha, maana adui yenu ibilisi huzungukazunguka kama simba angurumaye akitafuta mtu ili apate kummeza” (1 Petro 5:8), je anafaa kukoma na kumwomba Mungu ruhusa kwa kila hatua? Au anafaa tu kuomba ruhusa maalum anapojipata kikwazo katika kutekeleza chuki yake? Hata hivyo hakuna uthibitisho wa kweli wa kibiblia. Ayubu na Petro walikuwa wamezungukwa na Bwana, Shetani hangeweza kuwafikia bila Bwana kwanza kuondoa ulinzi wake. Tunajua kwamba Mungu anawajali watoto wake wote, kwa hiyo ni vizuri kufikiria kwamba Mungu ana kiasi fulani cha ulinzi kinachomzunguka kila mmoja wetu. Na tunajua kwamba, hatimaye, Mungu anadhabiti kila kitu katika ulimwengu, akiwemo Shetani. “Nasi tunajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hutenda kazi pamoja na wote wampendao, katika kuwapatia mema, yaani, wale walioitwa kwa kusudi lake” (Warumi 8:28).

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, Shetani anapaswa kupata kibali cha Mungu kabla ya kutushambulia?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries