settings icon
share icon
Swali

Je, roho ya dunia ni gani?

Jibu


Kifungu roho ya dunia ni istilahi mtume Paulo alitumia katika 1 Wakorintho 2:12, ambapo anatofautisha kati ya roho ya dunia na Roho wa Mungu: “Basi hatukupokea roho ya dunia bali Roho atokaye kwa Mungu, ili tuweze kuelewa kile kipawa ambacho Mungu ametupatia bure.”

Kinyume na roho ya dunia, Roho Mtakatifu utoa hekima ya ukweli kwa muumini. Roho Mtakatifu hutuwezesha kupokea na kuelewa “hekima ya Mungu ambayo ni siri, tena iliyofichika” (1 Wakorintho 2:7). Ni Roho wa Mungu pekee unaweza dhihirisha ukweli wa kiroho kwa sababu ni Roho Mtakatifu pekee anajua “hata mambo ya ndani sana ya Mungu” (1 Wakorintho2:10).

Roho ya dunia inaweza kueleweka kwa njia moja kati ya hizi tatu. Katika tafsiri moja, roho ya dunia ni roho ya kipepo au pengine Shetani hasa. Mahali pengine katika Maandiko, Shetani anaitwa “mkuu wa ulimwengu” (Yohana Mtakatifu 12:31; 12:30; 16:11) na “mungu wa dunia hii” (2 Wakorintho 4:4). Yeye ni “yule roho atendaye kazi sasa ndani ya wale wasiotii” (Waefeso 2:2).

Wengine wanapekeza kwamba Paulo hakuwa anamaanisha roho mbaya, pekee yake, lakini badala yake mawazo ambayo ni ya kigeni na ya kupinga Roho wa Mungu—ni tabia asili ya dhambi ya kibinadamu, ambayo inaweza kuitwa roho ya kuasi, tamaa, kiburi na yenye uongo. Mtazamo wa tatu ni kwamba roho ya dunia ni hekima ya mwanadamu kwa ujumla au mchakato wa kimsingi wa binadamu wa kuelewa, vile inavyoonyeshwa katika falsafa ya kidunia na hekima ya kiulimwengu.

Mungu anafanya hekima ya kilimwengu kuwa ya upumbavu, kwa vile imechochewa na roho ya dunia: “Yuko wapi mwenye hekima? Yuko wapi msomi? Yuko wapi mwanafalsafa wa nyakati hizi? Je, Mungu hakufanya hekima ya ulimwengu huu kuwa upumbavu? Kwa kuwa katika hekima ya Mungu, ulimwengu kwa hekima yake haukumjua yeye, ilimpendeza Mungu kuwaokoa wale walioamini kwa upuzi wa lile neno lililohubiriwa.” (1 Wakorintho 1:20-21). Kutoka kwa mtazamo wa kibinadamu na kiulimwengu, ni upumbavu kumwani Yesu Kristo kama njia ya wokovu.

Roho ya dunia inaalekeza kwa upumbavu kwa sababu hekima ya binadamu inategemea hekima ya kweli ya Mungu. Hekima ya binadamu inajaribu kujivuna mbele za Mungu; ni yenye kiburi. Hekima ya binadamu inakataa utu na kazi ya Kristo, ambaye ni “ndiye nguvu ya Mungu na pia hekima ya Mungu” (1 Wakorintho 1:24). Hekima ya ukweli kutoka kwa Roho wa Mungu ambaye tumempokea anatambua kwamba wokovu wetu hahustahili kabisa neema ya Mungu: “Lakini Mungu alivichagua vitu vipumbavu vya ulimwengu ili awaaibishe wenye hekima, Mungu alivichagua vitu dhaifu vya ulimwengu ili awaaibishe wenye nguvu. Alivichagua vitu vya chini na vinavyodharauliwa vya dunia hii, vitu ambavyo haviko, ili avibatilishe vile vilivyoko, ili mtu yeyote asijisifu mbele zake. Bali kwa yeye ninyi mmepata kuwa katika Kristo Yesu, aliyefanyika kwetu hekima itokayo kwa Mungu, yaani haki, na utakatifu na ukombozi. Hivyo, kama ilivyoandikwa: “Yeye ajisifuye na ajisifu katika Bwana” (1 Wakorintho 1:27-31).

Ingawa waumini wa Korintho walidai kuwa wakomavu kiroho, walikuwa, kwa hakika, wanaonyesha kutokomaa kwao kupitia majivuno na mgawanyiko. Paulo aliwafundisha kwamba, kuwa wakomavu kwa kweli, wanapazwa kutelekeza hekima ya binadamu (roho ya dunia) kwa hekima safi ya Roho Mtakatifu ya injili. Waumini hawawezi kutambua hazina ya ajabu na ya siri, ambayo wamepokea kutoka kwa Mungu kwa kuangalia na macho yao ya kawaida ya binadamu.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, roho ya dunia ni gani?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries