settings icon
share icon
Swali

Je! Roho saba za Mungu ni gani?

Jibu


"Roho saba za Mungu" zinatajwa katika Ufunuo 1:4; 3:1; 4:5; na 5:6. Roho saba za Mungu hazitambuliki kwa wazi, kwa hivyo haiwezi kutangazwa kama Imani ya kanisa. Ufunuo 1:4 inasema kwamba roho saba ziko mbele ya kiti cha enzi cha Mungu. Ufunuo 3:1 inaonyesha kwamba Yesu Kristo "anashikilia" roho saba za Mungu. Ufunuo 4:5 unaunganisha roho saba za Mungu na taa saba zinazowaka zilizo mbele ya kiti cha enzi cha Mungu. Ufunuo 5:6 hubainisha roho saba na "macho saba" ya Mwanakondoo na inasema kwamba "zimetumwa duniani kote."

Kuna angalau tafsiri tatu zinazowezekana za roho saba za Mungu. Ya kwanza ni kwamba roho saba za Mungu ni ishara ya Roho Mtakatifu. Biblia, na hasa kitabu cha Ufunuo, inatumia namba 7 kutaja ukamilifu na kukamilika. Ikiwa hiyo ndiyo maana ya "saba" katika "roho saba," basi haimaanishi roho saba za Mungu tofauti, lakini badala yake Roho Mtakatifu kamili na mkamilifu. Mtazamo wa pili ni kwamba roho saba za Mungu zinarejelea viumbe saba vya malaika, labda serafi au makerubi. Hii ingekuwa sawa na viumbe wengine wengi wa malaika ambao wanaelezewa katika kitabu cha Ufunuo (Ufunuo 4:6-9, 5:6-14; 19:4-5).

Uwezekano wa tatu umeweka msingi katika Isaya 11:2, ambayo inasema, "Na Roho ya BWANA atakaa juu yake, roho ya hekima na ufahamu, roho ya shauri na uweza, roho ya maarifa na ya kumcha BWANA." Hii labda inaweza kuelezea roho saba za Mungu: (1) Roho ya BWANA, (2) Roho ya hekima, (3) Roho ya ufahamu, (4) Roho ya shauri, (5) Roho ya uweza, (6) Roho ya maarifa, (7) Roho ya kumcha Bwana. Biblia haituambii hasa ni nani/nini roho saba, lakini tafsiri ya kwanza, kwamba ni Roho Mtakatifu, inaonekana ya uwezekano zaidi.

English


Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Roho saba za Mungu ni gani?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries