settings icon
share icon
Swali

Je, Roho Mtakatifu milele humuacha muumini?

Jibu


Kwa ufupi, hakuna, Roho Mtakatifu kamwe hamwachi muumini wa kweli. Hii imefunuliwa katika vifungu mbalimbali katika Agano Jipya. Kwa mfano, Warumi 8:9 inatuambia, "... Lakini mtu awaye yote asipokuwa na Roho wa Kristo huyo si wake." Aya hii kwa wazi sana inasema kwamba kama mtu hana makao ya uwepo wa Roho Mtakatifu, basi mtu huyo hajaokolewa. Kwa hivyo, kama Roho Mtakatifu alikuwa anamuacha muumini, huyo mtu angekuwa amepoteza uhusiano wa kuoka na Kristo. Hata hivyo hii ni kinyume na kile ambacho Biblia inafundisha kuhusu usalama wa milele wa Wakristo. Aya nyingine ambayo inasungumzia kudumu kwa Roho Mtakatifu aliye ndani muumini katika maisha ya waumini ni Yohana 14:16. Hapa Yesu anasema kwamba Baba atawapa Msaidizi mwingine "kuwa nanyi milele."

Ukweli kwamba Roho Mtakatifu kamwe hamwachi muumini pia inaonekana katika Waefeso 1:13-14 ambapo waumini wanatiwa 'muhuri' kwa Roho Mtakatifu, "Ndiye aliye arabuni ya urithi wetu, ili kuleta ukombozi wa milki yake, kuwa sifa ya utukufu wake." picha ya kutiwa mhuri na Roho ni mojawapo ya umiliki na mali. Mungu ameahidi uzima wa milele kwa wote wanaoamini katika Kristo, na kama uhakikisho kwamba Yeye atatimiza ahadi yake, ambaye alimtuma Roho Mtakatifu kukaa ndani ya muumini mpaka siku ya ukombozi. Sawa na kuweka amana wakati unanunua gari au nyumba, Mungu amewatolea waumini wote amana ya uhusiano wao wa baadaye pamoja naye kwa kutuma Roho Mtakatifu kukaa ndani yao. Ukweli kwamba waumini wote wametiwa muhuri na Roho pia inaonekana katika 2 Wakorintho 1:22 na Waefeso 4:30.

Kabla ya kifo cha Kristo, ufufuo, na kupaa mbinguni, Roho Mtakatifu alikwisha kuwa "kuja na kwenda" na uhusiano na watu. Roho Mtakatifu alimwingia Mfalme Sauli, lakini kisha akamwondoka (1 Samweli 16:14). Na badala yake, Roho ukamuingia Daudi (1 Samweli 16:13). Baada ya uasherati wake na Bathsheba, Daudi aliogopa kuwa Roho Mtakatifu atachukuliwa kutoka kwake (Zaburi 51:11). Bezaleli alijazwa na Roho Mtakatifu na kumwezesha kuzalisha vitu vilivyohitajika kwa ajili ya hema (Kutoka 31:2-5 ), lakini hii si kama ilivyoelezwa uhusiano wa kudumu. Yote haya yalibadilika baada ya kupaa kwa Yesu mbinguni. Kuanzia siku ya Pentekoste, Roho Mtakatifu alianza kudumu milele ndani ya waumini (Matendo 2). Kupokea uwepo wa kudumu wa Roho Mtakatifu ni kutimiza ahadi ya Mungu kuwa daima atakuwa pamoja nasi na kamwe hatatuacha.

Huku Roho Mtakatifu kamwe kumwondoka muumini, inawezekana kwa ajili ya dhambi zetu na "kumzimisha Roho Mtakatifu" (1 Wathesalonike 5:19) au "kumhuzunisha yule Roho Mtakatifu" (Waefeso 4:30). Dhambi daima ina madhara kwa uhusiano wetu na Mungu. Wakati uhusiano wetu na Mungu ni salama ndani ya Kristo, kuungama dhambi katika maisha yetu tunaweza kuzuia ushirika wetu na Mungu na kwa ufanisi kumzimisha Roho Mtakatifu kufanya kazi katika maisha yetu. Hiyo ndio sababu ni muhimu sana kwa kukiri dhambi zetu kwa sababu Mungu ni "mwaminifu na wa haki na atatusamehe dhambi zetu na kutusafisha na udhalimu wote" (1 Yohana 1:9). Hivyo, wakati Roho Mtakatifu kamwe hatuachi, faida na furaha ya uwepo wake unaweza kwa kweli kutoweka kutoka kwetu.

English
Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, Roho Mtakatifu milele humuacha muumini?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries