settings icon
share icon
Swali

Je! Roho Mtakatifu huwepo wakati wa majonzi?

Jibu


Swali la Roho Mtakatifu kutokuwepo wakati wa majonzi hutokana na kutoilewa 2 Wathesalonike 2:7 ambayo inasoma, "Maana ile siri ya kuasi hivi sasa inatenda kazi; lakini yuko azuiaye sasa, hata atakapoondolewa." Hivi sasa, kabla ya mateso, huduma moja ya Roho Mtakatifu ni kuzuia maovu. Katika aya ya 8 na 9, tunajifunza kuwa nguvu ya kuzuia ya Roho Mtakatifu humzuia "yule mwovu" (mpinga Kristo) na kwa hivyo hadhihirishi kabla ya Mungu kutaka. Kifungu kinasema kuwa Roho Mtakatifu sasa hatuzia ongezeko la uovu, lakini hii haimanishi kuwa hatukuwa na huduma kamwe.

Katika Matendo 1:4-5, Yesu aliahidi wanafunzi wake kuwa kwa muda mfupi "watabatizwa kwa Roho Mtakatifu." Katika Matendo 2 ahadi ya Yesu imetimizwa. Katika aya ya 38 na 39 imeandikiwa "Petro akawajibu, "Tubuni, mkabatizwe kila mmoja wenu kwa jina la Yesu Kristo, ili mpate kusamehewa dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu. Kwa kuwa ahadi hii ni kwa ajili yenu na watoto wenu, na kwa wote walio mbali, na kila mtu ambaye Bwana Mungu wetu atamwita amjie.'"

Kila muumini ambaye amezaliwa mara ya pili amehakikishwa kujazwa na Roho Mtakatifu, na hakuna mahali katika Maandiko ahadi hiyo imevunjwa. Kuhuishwa upya ni kazi ya Roho; bila Yeye hakuna yeyote anaweza okolewa. Roho asingalikuwapo wakati wa majonzi, hakuna mtu angeweza kuokolewa. Lakini ukweli ni kwamba umati ambao hakuna awezaye kuuhesabu umeokolewa katika kipindi cha mateso (Ufunuo 7:9-14). Kwa hivyo, wale wanaokuja kwa Yesu wakati wa kipindi cha mateso pia watajazwa na Roho Mtakatifu. Mpe Mungu utukufu kwa kupeana nafasi hiyo, kwa sababu watakatifu wanaoteseka watahitaji uongozo wa Roho wakati wa kipindi cha mateso.

Sababu nyingine muhimu ya Roho kuwapo wakati wa majonzi ni kwamba Yeye yuko kila mahali. Jinsi Yeye yuko kila mahali wakati wote, lazima awe ulimwenguni wakait wa kipindi cha mateso.

Katika wakati mmoja-ni Mungu pekee anajua- ushawishi wa kuzuiliwa wa Roho Mtakatifu utaondolewa, na Mpinga Kristo atadhihirishwa kwa ulimwengu usio na habari na ufahamu, na hapo mateso yataanza.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Roho Mtakatifu huwepo wakati wa majonzi?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries