settings icon
share icon
Swali

Je! Roho Mtakatifu ni Mungu?

Jibu


Jibu fupi kwas wali hili ni, naam, Roho Mtakatifu jinsi alivyoelezewa katika Biblia kikamilifu ni Mungu. Pamoja na Mungu Baba na Mungu Mwana (Yesu Kristo), Mungu Roho ni mshirika wa tatu katika Uungu/Utatu.

Wale ambao wanalipinga hoja ya Roho Mtakatifu ni Mungu wanapendekeza kwamba Roho Mtakatifu inaweza kuwa ni kule kujilazimisha kwa kiwango, chanzo cha nguvu kimedhibitiwa na Mungu na sio kikamilifu kama mtu binafsi. Wengine wanapendekeza kuwa pengine Roho Mtakatfu ni neno linguine la Yesu akiwa katika umbo la roho, mbali na mwili wake.

Kati ya hoja hizi hakuna yenye inaambatana na kile kwa hakika Biblia inasema kuhusu Roho Mtakatifu. Biblia inaelezea Roho Mtakatifu kuwa mtu ambaye amekuwapo pamoja na Baba na Mwana tangu kabla wakati uanze. Roho ni wa muhimu sana katika mambo yote ambayo Mungu anaelezewa kuyafanya katika Biblia.

Roho wa Mungu alikuwako na alihusika katika uumbaji (Mwanzo 1:2; Zaburi 33:6). Roho Mtakatifu aliwaongoza manabii wa Mungu na neno la Mungu (2Petro 1:21). Mili ya wale wako ndani ya Kristo inaelezewa kuwa hekalu la Mungu kwa sababu ya Roho Mtakatifu ako ndani yetu (1 Wakorintho 6:19). Yesu alikuwa wazi kuwa "kuzaliwa mara ya pili," kuwa Mkristo mtu lazima azaliwe kwa "Roho" (Yohana 3:5).

Mojawapo ya kauli ambayo ni ushawishi katika Biblia kuhusu Roho Mtakatifu kuwa Mungu inapatikana katika Matendo 5. Wakati Anania alidanganya kuhusu kipande cha shamba lao, Petro alisema kuwa Shetani alikuwa ameujaza moyo wa Anania "kudanganya Roho Mtakatifu" (Matendo 5:3) na kutamatisha kwa kusema kuwa Anania alikuwa "amemdanganya Mungu" (aya ya 4). Maneno ya Petro yanasawazisha Roho Mtakatifu na Mungu; alizungumza kana kwamba Roho Mungu walikuwa kitu kimoja.

Yesu aliwaambia wanafunzi wake kuwa Roho Mtakatifu, msaidizi, alikuwa tofauti naye. Baba atatuma Msaidizi, ambaye ni Roho wa kweli baada ya Kristo kutoka. Roho atanena kupitia kwao kuhusu Yesu (Yohana 14:25-26; 15:26-27; 16:7-15). Watu wote Yesu anataja ni Mungu huku wakiwa tofauti kutoka kila mmoja katika Utatu.

Wanachama watatu wa Utatu wanajidhihirisha pamoja na huku wakiwa tofauti katika kubatizwa kwa Yesu. Yesu anapotoka kwa maji, Roho akamshukia kama njiwa huku sauti ya Baba ikasikika toka mbinguni ikisema kuwa Huyu ni Mwanangu mpendwa ninayefurahishwa naye.

Mwishowe, biblia inaelezea Roho Mtakatifu kama mtu, sio nguvu. Anaweza huzunishwa (Waefeso 4:30). Ako na nia (1 Wakorintho 12:4-7). Anatumia akili yake kutafuta tafuta mambo ya ndani ya Mungu (1 Wakorintho 2:10). Na ana ushirika na waumini (2 Wakorintho 13:14). Kwa wazi Roho ni nafsi, kama vile Baba na Mwana ni nafsi.

Kwa hakika biblia hii dhahiri kuwa Roho Mtakatifu kwa kweli ni Mungu, jinsi vile Yesu Kristo na Baba ni Mungu.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Roho Mtakatifu ni Mungu?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries