settings icon
share icon
Swali

Nguvu ya Roho Mtakatifu ni gani?

Jibu


Nguvu za Roho Mtakatifu ni nguvu za Mungu. Roho, Mtu wa tatu wa Utatu, ameonekana katika Maandiko kama kiumbe na ambaye kupitia kwake kazi kubwa za nguvu zinadhihirishwa. Nguvu yake ilionekana kwanza katika tendo la uumbaji, kwa maana ilikuwa kwa Nguvu Yake ulimwengu ulikuwepo (Mwanzo 1: 1-2; Ayubu 26:13). Roho Mtakatifu pia aliwawezesha watu katika Agano la Kale kuleta mapenzi ya Mungu: "Basi Samweli akachukua pembe wake wenye mafuta akammiminia Daudi mafuta mbele ya kaka zake. Mara roho ya Mwenyezi-Mungu ikamjia Daudi kwa nguvu" (1 Samweli 16:13; tazama pia Kutoka 31: 2-5; Hesabu 27:18). Ingawa Roho hakuwa na watu wa Mungu katika Agano la Kale, alifanya kazi kupitia nao na kuwapa uwezo wa kufikia mambo ambayo hawangeweza kukamilisha wao wenyewe. Nguvu zote za nguvu za Samsoni zinahusishwa moja kwa moja na Roho kuja juu yake (Waamuzi 14: 6, 19; 15:14).

Yesu aliahidi Roho kuwa mwongozo wa kudumu, mwalimu, muhuri wa wokovu, na mtetezi kwa waumini (Yohana 14: 16-18). Pia aliahidi kuwa nguvu ya Roho Mtakatifu itawasaidia wafuasi Wake kueneza ujumbe wa injili ulimwenguni kote: "Lakini wakati Roho Mtakatifu atakapowashukieni nyinyi, mtapokea nguvu na mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, katika nchi yote ya Yudea na Samaria, n ahata miisho ya dunia" (Matendo 1: 8). Wokovu wa roho ni kazi isiyo ya kawaida tu inayowezekana kwa uwezo wa Roho Mtakatifu katika kazi duniani.

Wakati Roho Mtakatifu akishuka juu ya waumini pa Pentekoste, haikukuwa tukio la utulivu, bali ni nguvu. "Siku ya Pentekoste ilipofika, waumini wote walikuwa wamekusanyika mahali pamoja. Ghafla, sauti ikasikika kutoka angani; sauti iliyokuwa kama ya upepo mkali, ikaijaza ile nyumba yote walimokuwa wamekaa. Kisha, vikatokea vitu vilivyoonekana kama ndimi za moto, vikagawanyika na kutua juu ya kila mmoja wao. Wote wakajazwa Roho Mtakaatifu, wakaanza kusema lugha mbalimbali kadiri Roho alivyowawezesha"(Matendo 2: 1-4). Mara baada ya hapo, wanafunzi waliongea na makutano uliokusanyika Yerusalemu kwa ajili ya Sikukuu ya Pentekoste. Watu hawa walikusanyika kutoka kwa mataifa mbalimbali na kwa hiyo walizungumza lugha nyingi. Fikiria mshangao wao na kushangaa wakati wanafunzi waliwaambia kwa lugha zao wenyewe (mistari 5-12)! Kwa wazi, hii haikuwa kitu ambacho wanafunzi wangeweza kukamilisha kwoa wenyewe bila miezi mingi-au hata miaka-ya kujifunza. Nguvu ya Roho Mtakatifu ilidhihirishwa kwa idadi kubwa ya watu siku hiyo, na kusababisha uongofu wa takiribani watu 3,000 (aya 41).

Wakati wa huduma yake duniani, Yesu alijazwa na Roho Mtakatifu (Luka 4: 1), akiongozwa na Roho (Luka 4:14), na kupewa uwezo wa Roho kufanya miujiza (Mathayo 12:28). Baada ya Yesu kupaa mbinguni, Roho aliwawezesha mitume kufanya miujiza, pia (2 Wakorintho 2:12, Matendo 2:43; 3: 1-7, 9: 39-41). Nguvu ya Roho Mtakatifu ilionekana kati ya waumini wote wa kanisa la kwanza kwa njia ya karama za kiroho kama vile kuzungumza kwa lugha, kutabiri, kufundisha, hekima, na zingine nyingi.

Wote wanaoweka imani yao katika Yesu Kristo papo hapo na daima watakuwa wamejazwa na Roho Mtakatifu (Warumi 8:11). Na, ingawa baadhi ya karama za kiroho zimekoma (k.m., kuzungumza kwa lugha na unabii), Roho Mtakatifu bado anafanya kazi ndani na kupitia kwa waumini kutimiza mapenzi Yake. Nguvu zake zinatuongoza, hutuhukumu, hutufundisha, na hutuwezesha kufanya kazi Yake na kueneza Injili. Uwezo wa Roho Mtakatifu ni karama ya kushangaza ambayo hatupaswi kamwe kuichukulia kimzaa.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Nguvu ya Roho Mtakatifu ni gani?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries