settings icon
share icon
Swali

Roho Mtakatifu ni mtu?

Jibu


Watu wengi hupata mafundisho ya Roho Mtakatifu kuwa ya kuchanganya. Roho Mtakatifu ni nguvu, mtu, au kitu kingine? Biblia inafundisha nini?

Biblia hutoa njia nyingi za kutusaidia kuelewa kwamba Roho Mtakatifu ni mtu-yaani, Yeye ni mwanadamu, badala ya kitu cha kibinadamu. Kwanza, kila pronouni inayetumiwa inazungumzia Roho kama "yeye" si "ni." Lugha ya Kigiriki ya awali ya Agano Jipya inaelezea kwa kumhakikishia mtu wa Roho Mtakatifu. Neno litumikalo kwa "Roho" (pneuma) lina maana isiyo ya kiume wala kike na ndio liwe na uelewano wa ngeli lazima lichukue nauni isiyo ya kiume wala kike. Hata hivyo, katika hali nyingi, matamshi ya kiume hupatikana (k.m., Yohana 15:26; 16: 13-14). kilugha, hakuna njia nyingine ya kuelewa matamshi ya Agano Jipya kuhusiana na Roho Mtakatifu-Yeye anajulikana kama "Yeye," kama mtu.

Mathayo 28:19 inatufundisha kubatiza kwa jina la Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu. Hii ni kumbukumbu ya pamoja kwa Mungu mmoja wa watatu. Pia, hatupaswi kusikitisha Roho Mtakatifu (Waefeso 4:30). Roho anaweza kutendewa dhambi (Isaya 63:10) na kudanganywa (Matendo 5: 3). Tunapaswa kumtii (Matendo 10: 19-21) na kumheshimu (Zaburi 51:11).

Utu wa Roho Mtakatifu unathibitishwa kwa kazi yake nyingi. Yeye binafsi alikuepo katika uumbaji (Mwanzo 1:2), anawatia nguvu watu wa Mungu (Zekaria 4:6), anawaongoza (Warumi 8:14), anawafariji (Yohana 14:26), anawahukumu (Yohana 16:8), anafundisha (Yohana 16:13), Zuuia dhambi (Isaya 59:19), na anatoa amri (Matendo 8:29). Kila mojawapo ya kazi hizi zinahitaji kuingilia kati kwa mtu badala ya nguvu ya kawaida, kitu au dhana.

Sifa za Roho Mtakatifu pia zinaonyesha utu wake. Roho Mtakatifu ana uzima (Waroma 8: 2), ana nia (1 Wakorintho 12:11), anajua mambo yote (1 Wakorintho 2: 10-11), ni wa milele (Waebrania 9:14), na ako kila mahali (Zaburi 139: 7). Nguvu tu ya kawaida haiwezi kuwa na sifa hizi zote, lakini Roho Mtakatifu ako nayo.

Na utu wa Roho Mtakatifu unathibitishwa na jukumu lake kama Mtu wa tatu wa Uungu. Ni kiumbe pekee tu kilicho sawa na Mungu (Mathayo 28:19) na kina sifa za ujuzi wa, kujua mambo yote, na kuwa kila mahali na kuishi milele kinaweza kuelezwa kama Mungu.

Katika Matendo 5: 3-4, Petro alimtaja Roho Mtakatifu kama Mungu, akisema, "Anania, mbona Shetani ameuingia moyo wako na kukufanya umdanganye Roho Mtakatifu kwa kujiwekea sehemu ya fedha ulizopata kutokana na lile shamba? Kabla ya kuliuza lilikuwa mali yako, baada ya kuliuza, bado hizo fedha zilikuwa zako uzitumie utakavyo. Kwa nini basi, uliamua moyoni mwako kufanya jambo la namna hii? Hukumdanganya mtu; umemdanganya Mungu!" Paulo vile vile alimrejelea Roho Mtakatifu kama Mungu katika Wakorintho wa Pili 3:17-18, akisema, "Bwan ni Roho; na pale alipo Roho wa Bwana ndipo ulip uhuru. Basi, sisi sote ambao nyuso zetu hazikufunikwa, tunaona kama katika kioo, utukufu wa Bwana; tunabadilishwa tufanane Zaidi na huo mfano wake kwa utukufu mwingi Zaidi. Hiyo ni kazi yake Roho wa Bwana."

Roho Mtakatifu ni mtu, kama vile Maandiko yanavyo wazi. Kwa hivyo, Yeye atakuwa na heshima kama Mungu na hutumikia katika umoja kamili na Baba na Mwana kutuongoza katika maisha yetu ya kiroho.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Roho Mtakatifu ni mtu?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries