settings icon
share icon
Swali

Je, Roho Mtakatifu hufanya nini?

Jibu


Biblia iko wazi kabisa kwamba Roho Mtakatifu anafanya kazi katika ulimwengu wote. Kitabu cha Matendo ambacho pia huitwa "Matendo ya Mitume," kingeweza kuitwa "Matendo ya Roho Mtakatifu kupitia Mitume." Kumekuwa na mabadiliko kadhaa baada ya enzi za kitume-kwa mfano, Roho haongozi Maandiko zaidi-lakini anaendelea kufanya kazi yake ulimwenguni.

Kwanza, Roho Mtakatifu hufanya mambo mengi katika maisha ya waumini. Yeye ndiye Msaidizi wa waumini (Yohana 14:26). Yeye hukaa katika waumini na kuwatia muhuri hata siku ya ukombozi-hii inaonyesha kwamba uwepo wa Roho Mtakatifu ndani ya mwamini ni usiorudika. Yeye hulinda na kuwahakikishia wokovu wale ambao anakaa ndani yao (Waefeso 1:13; 4:30). Roho Mtakatifu husaidia waumini katika maombi (Yuda 1:20) na "huwaombea watu wa Mungu kufuatana na mapenzi ya Mungu" (Warumi 8:26-27).

Roho Mtakatifu huisha upya na kumfanya upya mwamini (Tito 3:5). Wakati wa kuokoka, Roho hubatiza mwamini katika Mwili wa Kristo (Warumi 6:3). Waumini hupokea kuzaliwa upya kwa nguvu ya Roho (Yohana 3:5-8). Roho huwafariji waumini na kushiriki nao na kuwapa furaha katika dhiki nyingi iliyo ulimwenguni (1 Wathesalonike 1:6; 2 Wakorintho 13:14). Roho, katika nguvu yake kuu, hujaza waumini na "furaha yote na amani" wanapomwamini Bwana, na kusababisha waumini "kuzidi kuwa na tumaini" (Warumi 15:13).

Utakaso ni kazi nyingine ya Roho Mtakatifu katika maisha ya mwamini. Roho Mtakatifu hupigana vita dhidi ya tamaa za mwili na huongoza mwamini katika utakatifu (Wagalatia 5:16-18). Kazi za mwili zinadidimia na kazi za Roho Mtakatifu zinakuwa dhahiri (Wagalatia 5:19-26). Waumini wameamriwa "kujazwa na Roho" (Waefeso 5:18), kumaanisha wanapaswa kujitolea kwa udhibiti kamili wa Roho.

Roho Mtakatifu pia hupeana karama. "Vipaji vya kiroho ni vya namna nyingi, lakini Roho avitoaye ni mmoja" (1 Wakorintho 12:4). Karama za Roho za waumini hupeanwa na Roho mtakatifu kama apendavyo mwenyewe (mstari wa 11).

Roho Mtakatifu pia hufanya kazi kati ya wasioamini. Yesu aliahidi kwamba atatuma Roho Mtakatifu "kudhibitishia walimwengu kwamba wamekosea kuhusu dhambi na haki na hukumu" (Yohana 16:8). Roho hushuhudia Kristo (Yohana 15:26), akiwaelekeza watu kwa Bwana. Siku hizi, Roho Mtakatifu pia anazuia dhambi na kupambana na "siri ya kuasi" ulimwenguni. Kitendo hiki kinazuia kuongezeka kwa Mpinga Kristo (2 Wathesalonike 2:6-10).

Roho Mtakatifu ana jukumu lingine muhimu ambayo ni ya kuwapa waumini hekima ndipo waweze kumwelewa Mungu. "Lakini Mungu ametufunulia sisi kwa Roho. Maana Roho huchunguza yote, hata mafumbo ya Mungu.Maana ni nani katika binadamu ayajuaye mambo ya binadamu ila roho ya binadamu iliyo ndani yake? Vivyo hivyo na mambo ya Mungu hakuna ayafahamuye ila Roho wa Mungu" (1 Wakorintho 2:10-11). Kwa kuwa waumini wamepewa karama ya ajabu ya Roho ndani yetu, tunaweza kuelewa mawazo ya Mungu, kama ilivyowekwa wazi katika Maandiko. Roho hutusaidia kuelewa. Hii ni hekima kutoka kwa Mungu, sio hekima kutoka kwa mwanadamu. Hakuna kiwango cha hekima ya binadamu kinachoweza kuchukua nafasi ya mafundisho ya Roho Mtakatifu (1 Wakorintho 2:12-13).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, Roho Mtakatifu hufanya nini?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries