settings icon
share icon
Swali

Je! Wakristo waliofunga ndoa wanapaswa kuvaa pete za harusi?

Jibu


Biblia haionyeshi kwamba pete za chanda zilitumika kama pete za uchumba au ndoa. Pete ya muhuri ndiyo aina ya kwanza kabisa ya pete inayotajwa katika Biblia. Kwa kweli, mtumishi wa Ibrahimu alipompata Rebeka, alimpa pete ya pua ili kudai kuwa ni bibi-arusi wa Isaka (Mwanzo 24:22)! Tamari alipojigeuza kuwa kahaba ili kushawishi baba-mkwe wake, Yuda, alimwomba muhuri, kamba na fimbo yake kama amana ya ahadi yake ya kumpelekea “mwana-mbuzi kutoka kundini” (Mwanzo 38:17-19). Yeremia anatujulisha kwamba Waisraeli walivaa pete ya muhuri kwenye mkono wa kulia (Yeremia 22:24). Pete ya saini ilitumika kufunga mikataba mbalimbali. Ilikuwa ishara ya mamlaka, heshima, na hadhi ya kijamii (Yakobo 2:2). Farao alimpa Yusufu pete yake ya muhuri kama ishara ya mamlaka (Mwanzo 41:42). Vivyo hivyo, Ahasuero alimpa Hamani muhuri wake ili kutia muhuri amri ya kifalme (Esta 3:10, 12). Mwana mpotevu, aliporudi, alipokea pete kutoka kwa baba yake kama ishara ya heshima na nafasi iliyorejeshwa (Luka 15:22).

Pete za vidole zinazotajwa katika Biblia ni pete za muhuri zinazotumiwa kama ishara za mamlaka na heshima. Warumi wanasifiwa kwa kuanzisha matumizi ya pete ya muhuri kama pete ya uchumba. Wayahudi na Wakristo waliazima desturi hiyo kutoka kwa Warumi. Kwa kuwa sherehe ya uchumba kwa kawaida ilihusisha bwana harusi kutoa kiasi cha pesa au kitu chenye thamani kwa bibi-arusi, ilikuwa badiliko la kawaida kufanya kitu hiki kuwa pete.

Harusi au pete ya ndoa ilianza kutumika katika sherehe za Kikristo katika karne ya 9 Baada ya Kristo (BK). Desturi ya kuvaa pete ya harusi kwenye chanda pete cha mkono wa kushoto ina msingi katika hadithi ya kimapenzi, ingawa si ya kisayansi, ya Kigiriki kwamba mshipa mkubwa unatoka kwenye kidole hiki na kutiririka moja kwa moja hadi kwenye moyo. Hijalishi jinsi na wakati desturi ya pete za harusi ilipoanza, hii leo inaonekana kama ishara ya kujitolea kwa kudumu kwa uhusiano wa ndoa. Kwa hivyo, kwa hakika ina msingi wa kibiblia kwamba ndoa inapaswa kuwa ahadi ya maisha yote (Warumi 7:2). Hii haimaanishi kwamba kuvaa pete ya ndoa ni matakwa kwa Wakristo waliofunga ndoa. Lakini pete za arusi ni ukumbusho mzuri wa agano la ndoa na, kwa kuongezea, agano la Kristo na bibi-arusi Wake-waliokombolewa ambao alikufa kwa ajili yao.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Wakristo waliofunga ndoa wanapaswa kuvaa pete za harusi?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries