settings icon
share icon
Swali

Je, ina maana gani kupenda kama Yesu?

Jibu


Mkristo anapaswa kuwa kama Yesu. Sehemu ya kuwa kama Yesu ni kupenda vile Yesu alivyopenda. Mungu ana lengo la kutufananisha na mfano wa Mwana Wake (Warumi 8:29). Yesu alikuwa mtiifu kwa Baba (Yohana 8:29), Alikuwa mwadilifu kwa kila njia (Waebrania 4:15), na alipenda watu bila ubinafsi (Mathayo 9:36; 14:14). Aliwaamuru wanafunzi Wake wapendane wenyewe jinsi Yeye alivyowapenda (Yohana 13:34). Lakini hilo linawakilisha shida. Yesu alionyesha upendo Wake katika kufa kwa ajili yetu, akisema, “Hakuna aliye na upendo mwingi kuliko huu” (Yohana 15:13). Kwa vile wengi wetu hatuwezi itwa ili tukufe kwa ajili ya mtu, ina maana gani kupenda kama Yesu?

Yohana 3:16 inatuambia maana ya kupenda kama Yesu: “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanaye pekee.” Upendo wa kiungu unatoa bila kujali. Kupenda kama Yesu inamaanisha kushikilia kila kitu tunachomiliki kwa mikono iliyo wasi. Tuko tayari kuachana na pesa, wakati, na mali ili kuwatumikia watu wengine. Tunatambua kwamba kile tunacho ni mkopo kwetu kutoka kwa Baba wa mbinguni na tuna jukumu la jinsi tunavyovitumia (Mathayo 25:14-30). Tunawapa watu kile wanahitaji wakati tuna uwezo wa kufanya hivyo. Wakati tunaona ndugu au dada ako na hitaji, na tuna rasilimali ambayo inaweza kusaidia, tunapaswa kugawa kile tuko nacho na wao (Yakobo 2:14; 1Yohana 3:16-17).

Yesu hakubagua jinsi alivyopenda. Alituonya kwamba ni rahisi kupenda wale walio kama sisi (Luka 6:32-33). Lakini Yesu alipenda hata adui Wake na anatarajia wafuasi Wake kufanya vivyo hivyo (Luka 6:35). Aliponya, akalisha, na kuhudumia wengi ambao walipasa sauti baadaye, “Msulubishe!” (Mathayo 27:20-22). Aliosha miguu ya Yuda Iskariote, akijua kwamba masaa machache Yuda atamsaliti Yeye (Yohana 13:4-5). Alitoa hoja alipohudumia Msamaria aliyechukiwa (Yohana 4), hata kumfanya Msamaria shujaa wa mfano (Luka 10:25-37). Tajiri na masikini, wadogo na wakubwa, waliomcha Mungu na wasiomcha Mungu—watu walikusanyika kumsikia Yesu kwa sababu aliwapenda (Marko 10:1; Mathayo 9:35-36; Luka 18:18).

Kupenda kama Yesu inamaanisha hatuwezi kuchagua jinsi tunavyowajali watu. Yakobo anakemea vikali sana upendeleo kwa msingi wa hali ya kifedha au kijamii: “Bali mkiwapendelea watu, mwafanya dhambi na kuhukumiwa na sheria kuwa wakosaji” (Yakobo 2:9). Tunapaswa kujali kila mwanadamu kwa heshima, tukikumbuka kwamba huyu mtu ni kiumbe maalum, aliyeumbwa kwa mfano wa Mungu (1 Yohana 2:9-10; 4:20-21). Lazima tufanye kazi ya kuondoa mioyo yetu ya ubagusi wa rangi, uroho wa kijamii na kiuchumi, na ubora wa kidini. Hakuna kati ya hayo yanapaswa kuwa katika maisha ya mtu anayetaka kupenda kama Yesu anavyopenda.

Hatupaswii kulinganisha upendo na ridhaa kamili ya kila kitu mtu anafanya. Yesu hakuvumilia dhambi, udanganyifu, au wafuasi wa uongo. Alikuwa na uchungu moja kwa moja na Mafarisayo, viongozi wa dini, na wale waliodai wanampenda Yeye lakini walipenda maisha yao zaidi. Alipokuwa bado anawapenda, Yesu aliwakemea Wafarisayo, akiwaita “Wanafiki!” na “Vipovu wapumbavu!” (Mathayo 23:13, 16). Aliwapa changamoto viongozi wa kidini na kuwaonya, “Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni” (Mathayo 7:21). Aliwashangaza wale waliokuwa na moyo nusu kwa kuwambia, “Mtu aliyetia mkono wake kulima, kisha akaangalia nyuma, hafai kwa ufalme wa Mungu” (Luka 9:62).

Kupenda kama Yesu inamaanisha tunajali vya kutosha kuhusu mioyo ya wengine kwa kuwaambia ukweli. Kiongozi mchanga tajiri alienda kwa Yesu na nia njema, lakini alikosa kuungama (Luka 18:18-25). Alikuwa anataka kile Yesu alikuwa anapeana, lakini hakuwa anamtaka Yesu. Alikuwa anapenda pesa zake zaidi, na Yesu akaonyesha tamaa ya huyo mtu kwa upendo. Hatupendi watu kwa kuwanyima injili ambayo inaweza kuwaokoa. Yesu hakubadilisha ukweli hili kuridhisha “masikio yaliyowasha” ya wasikilizaji Wake (ona 2 Timotheo 4:3). Aliwapenda vya kutosha kwa kuwaonya, kuwapa changamoto, kuwafundisha, na kuwasamehe hadi msalabani (Luka 23:34).

Kusamehe ni njia moja ya kupenda kama Yesu. Tunasemehe wakati tumekosewa (Mathayo 6:14; Waefeso 4:32). Ubinafsi wetu unataka kushikilia jeraha, kuthamini, kuunga mkono, na kuishi nalo. Lakini Yesu alisamehe na anatuambia tusamehe pia (Marko 11:25). Hatuwezi penda mtu ambaye hatuwezi kumsamehe. Yesu hakumbuki dhambi zetu zilizosamehewa juu yetu; badala yake, anatutangaza kuwa safi na kuliorejeshwa (1 Yohana 1:9). Kunaweza kuwa na matokeo ya dhambi zetu, lakini anatupenda kupitia kwa hizo dhambi na anatusaidia kujifunza kutoka kwazo. Tunapomsamehe mtu, tunaweza kumpenda na kumwombea huyo mtu na nia njema kwa sababu tumefanya kile Mungu anatuamuru tufanye (Wakolosai 3:13; Waefeso 4:32).

Yesu aliwambia wanafunzi Wake kwamba njia ya msingi ambayo ulimwengu unaweza kujua wao ni Wake ni kwa kupendana wenyewe kwa wenyewe (Yohana 13:35). Ikiwa tunampenda Yesu, basi tutapenda anachopenda, ambacho ni watu. Na tunapofanya mazoezi ya kupenda jinsi alivyopenda, tunazidi kuwa kama Yeye.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, ina maana gani kupenda kama Yesu?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries