settings icon
share icon
Swali

Je! nyakati za watu wa Mataifa ni gani?

Jibu


Katika Luka 21:24, Yesu anasungumzia matukio ys wakati ujao, hii ikiwa ni pamoja na kuharibiwa kwa Yerusalemu na kurudi kwake. Anasema kwamba “Nao mji wa Yerusalemu utakanyagwa na watu wa Mataifa hadi muda wa hao watu wa Mataifa utimie.” Kifungu hicho hicho kinapatika katika Warumi 11:25, ambacho kinasema, “Ugumu umewapata Israeli kwa sehemu hadi idadi ya watu wa Mataifa watakaoingia itimie.” Je! biblia inatuambia ni nini maana ya kifungu “muda wa watu wa mataifa?

Agano la Kale halina kifungu kamili cha maneno haya, lakini kuna marejeleo ambayo yanaonekana kufanana na haya. Ezekieli 30:3 inatuelekeza kwa “siku ya maangamizi kwa mataifa” imehusishwa na Siku ya Bwana. Mwandamano wa maono ya Danieli unahusu mamlaka ya ulimwengu wa Mataifa na jukumu lao katika mpango wa Mungu kwa dunia. Sanamu ya dhahabu ya Nebukadneza, fedha na shaba, chuma, na udongo (Danieli 2:31-45) inawakilisha falme za Mataifa zinazofuatana ambazo zitatawala hadi Kristo arudi na kuanzisha utawala Wake. Maono ya Danieli ya Minyama mnne (Danieli 7:1-27) vile vile inasumgumzia wafalme wanne au mataifa mane, ambayo watatawala kwa muda hadi Kristo aje kutawala milele. Ono hili la kondoo dume na mbuzi (Danieli 8:1-26) linatoa maelezo ya kina juu ya hawa wafalme wa Mataifa na muda uliohusika katika utawala wao. Katika kila mojawapo ya vifungu hivi, Mataifa yana mamlaka juu ya ulimwengu, hii ikiwa ni pamoja na Wayahudi, kwa muda, lakini hatimaye Mungu atawaangamiza wote na kuanzisha ufalme Wake mara moja. Kila unabii unatamati ukilenga ufalme wa Kristo, kwa hivyo “muda” wa viongozi wa Mataifa itakua miaka ile yote kati ya Ufalme wa Kibabeli wa Nebukadneza na ujio wa utukufu wa Kristo ili aansishe ufalme Wake. Sasa tunaishi katika “nyakati za watu wa Mataifa”, yaani kipindi ambacho Mataifa yametawala.

Tunapokichunguza kitabu cha Ufunuo, tunapata marejeleo sawia kuwa utawala wa Mataifa unaishia pale ujio wa Kristo. Katika Ufunuo 11:2 Yohana anaashiria kwamba Yerusalemu itakuwa chini ya utawala Mataifa, hata kama hekalu litakuwa limerejeshwa. Wanajeshi wa Mnyama wataangamizwa na Bwana katika Ufunuo 19:17-19, pindi kabla utawala wa miaka elfu moja ya Kristo umeanzishwa.

Tukichunguza tena Luka 21:24, tunaona kuwa Yesu alitaja wakati ambapo Yerusalemu itakuwa chini ya utawala na uwezo wa Mataifa. Kutekwa nyara kwa Yerusalemu na Nebukadneza katika mwaka wa 588 BC (Kabla Kristo) ulianza kipindi hicho, na umeendelea hadi wakati wa sasa. Warumi 11:25 inatupa kidokezo cha ni nini lengo la Mungu katika muda wa Mataifa: kuenea kwa Injili ulimwenguni kote. Mpangalio na uvumbuzi wa mamlaka kafiri ya ulimwengu hakika yamesaidia uinjilisti kwa mataifa. Kwa mfano, katika karne ya kwanza ilikua kupia ule msambao wa matumizi ya lugha ya Kigiriki na muundo msingi wa barabara za Kirumi ambazo ziliwezesha watu walioishi mashinani kusikia injili

Dhamira moja ya Warumi 11 ni kwamba, wakati Wayahudi walimkataa Kristo, kwa muda walitengwa na ile baraka yao kuwa na uhusiano na Mungu. Matokeo yake ni, watu wa Mataifa wakapewa injili na wao wakaipokea kwa kufaraha. Ugumu huu wa nyoyo wa muda kwa Waisraeli hakuwezi mzuia Myahudi binafsi kuoka, lakini itazuia taifa nzima katika kumpokea Kristo kama Masiha hadi pale mpango wake umekamilika. Wakati wa muda mwafaka Mungu atalirejesha taifa nzima na watakuja kwa imani ndani yake tena hii ikitamatisha “muda wa Mataifa (Isaya 17:7; 62:11-12).

English

Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! nyakati za watu wa Mataifa ni gani?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries