settings icon
share icon
Swali

Je! Kuwa tajiri ni dhambi?

Jibu


Biblia inazungumzia sana kuhusu maskini na inaiweka wazi kwamba hatupaswi kupuuza shida zao (Mithali 22:22; Kumbukumbu 15:7; Yakobo 2:5-6). Mungu alipomtuma Mwanawe ulimwenguni, hakumweka katika jumba la kifalme au jumb ala kifahari. Yesu alizaliwa katika famila yenye hali ya duni (Marko 6:3; Yohana 1:46). Biblia ina mifnao ya watu matajiri waliobarikiwa na Mungu, ikiwa ni pamoja na Ibrahimu (Mwanzo 13:2), Yakobo (Mwanzo 30:43), na Sulemani (1 Wafalme 10:23). Lakini, katika hali nyingi sana, Maandiko yanapozungumza kuhusu mali, yanatuonya juu ya hatari za kuwa na mali. Sio dhambi kuwa Tajiri, lakini utajiri huleta majaribu. Dhambi haipo katika kumiliki mali bali katika mitazamo yetu kuhusu utajiri huo na jinsi tunavyoutumia.

Waraka wa Kwanza wa Timotheo 6:9 unasema, “Lakini wale watu wanaotamani kuwa na mali kwa haraka huanguka kwenye majaribu, na wamenaswa na tamaa nyingi za kipumbavu zenye kudhuru, zinazowazamisha watu katika uharibifu na maangamizi.” Mstari wa 10 unaendelea na kusema, “Kwa maana kupenda fedha ndiyo shina moja la maovu ya kila namna. Baadhi ya watu wakitamani fedha, wameiacha imani na kujichoma wenyewe kwa maumivu mengi.” Wengi wamenukuu aya hii kimakosa kusema kwamba pesa ndio chanzo cha maovu yote, lakini hilo si sahihi. Mstari huo unasema kuwa kupenda fedha ndio hutunasa. Sanamu zetu hueleza kile tulicho. Tunapozingatia mafanikio ya dunia, mali, mahusiano, au umaarufu, tunakuwa waabudu sanamu. Wakati malengo yetu ya kidunia yanakuwa ya muhimu zaidi katika maisha yetu, hatuwezi pia kumpendeza Bwana (Warumi 8:8).

Mungu anaweza kuwapa watu wake utajiri wa duniani ambao pia wataugagwa jinsi vile anavyotaka. Wakrito matajiri ambao hawachukulii utajiri kama sanamu ni baraka kwa wengi. Wanaanzisha mashirika, wanachangia kusaidia mayatima na wajane (Yakobo 1:27), na kusaidia makanisa kujiweza kifedha (Malaki 3:10). Bila Wakristo matajiri, wamishonari wengi hawangeweza kutumikia umishenari.

Zakayo alikuwa mtu Tajiri, lakini utajiri wake hakuupa kwa njia isiyofaa na maisha yake yalikuwa na sifa ya uchoyo. Lakini alipokutana na Yesu, Bwana alibadilisha maisha yake. Badiliko la Zakayo liliathiri kila sehemu ya maisha yake, hii ikiwa ni pamoja na jinsi alivyo chukulia pesa: “Leo, wokovu umeingia nyumbani humu, kwa sababu huyu naye ni mwana wa Abrahamu” (Luka 19:8). Kwa kupata wokovu katika Kristo, Zakayo alipata pia kusudi jipya la utajiri wake. Yeye kuwa Tajiri haikuwa dhambi, lakini ingekuwa dhambi kwake kuendelea kulaghai watu au kutumia mali yake kwa malengo ya ubinafsi. Mungu huwapa matajri mali ili wawanufaishe wengine.

Mungu anataka turufarahie yote aliyotupa, ili mradi tusiruhusu zawadi hiyo kuwa mungu. Tunapaswa kuzingatia kila kitu tulicho nacho kama mkopo kutoka kwa Bwana na kumuuliza jinsi anavyotaka tuutumie (Zaburi 50:9-12). Mioyo yetu haipotoshwi na tamaa ya mali, tunaweza kujithibitisha kuwa wasimamizi wazuri wa kile ambacho Mungu ametukabidhi.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Kuwa tajiri ni dhambi?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries