settings icon
share icon
Swali

Je! Mwanamke Mkristo anaweza kuvaa nguo za ndani zinazochochea ngono kwa mumewe?

Jibu


Nguondani za kike ni aina ya mavazi ya wanawake ambayo yanajumuisha nguo za ndani na nguo za kulala usiku. Hata hivyo, kwa kawaida hatufikirii nguo za ndani kuwa na pamoja na nguo za kulała za flana na vazi la joto la mwili. Neno nguondani za kike linaweza kumaanisha virinda, kitani, na ya kuvutia inayovaliwa kwa ajili ya kufurahisha mwenzi wa ngono. Kwa kuwa vipande vingi vya nguo za ndani vimekusudiwa kuamsha mwitikio wa kingono, je, mke Mkristo anapaswa kuvaa nguo hiyo ya ndani kwa ajili ya mume wake?

Tunapozingatia maamuzi ya kindani kati ya mume na mke, ni lazima kila wakati tukumbuke maagizo ya Biblia katika 1 Wakorintho 7:3-5, ambayo huwakumbusha wenzi wa ndoa kwamba miili yao ni ya kila mmoja wao. Mke anapovaa nguo ndani inayovutia mume wake hakika bado ako katika mipaka ya uhuru wa Kikristo, na hakuna ubaya kwa mke kuvaa nguo hiyo ya ndani kwa hiari ili kumfurahisha mume wake.

Walakini, desturi la mke kuvaa nguo za ndani zinazovutia kwa mumewe linaweza kuvuka mipaka. Mume mwenye tamaa na ubininafsi anaweza kusisitiza kwamba mke wake atekeleze majukumu ya kudhalilisha ili kujirudisha mwenyewe na kwa njia zisizopendezana. Kumfanya mke avae kama kahaba, kumlazimisha avae nguo za ndani zinazomshushia hadhi, au kumshinikiza aigize majukumu ambayo yanamfanya akose raha sio sehemu ya maagizo ya Paulo ya kutii. Waume na wake hawapaswi kuona haya kujaribu na kufurahia kujieleza kwa ngono kwa njia yoyote wanayotaka; hata hivyo, wake wengine Wakristo wanahisi kushinikizwa na waume zao kutenda kwa njia fulani katika chumba cha kulala, kwa njia wanazoziona kuwa za kuchukiza. Mume mwenye hekima na upendo hatatumia kamwe utiivu wa mke wake kama kisingizio cha kukiuka dhamiri yake. Ikiwa mke atavaa nguo za ndani zinazochochea ngono, inapaswa kuwa kwa sababu wote wawili, mume na mke wanakubaliana kuhusu hilo (Waefeso 5:21).

Nyakati nyingine mke Mkristo atajitetea kwa kuvaa mavazi yanayoonyesha uchi wa mwili au ya kisherati hadharani kwa kusema, “Mume wangu anaipenda.” Walakini, kile ambacho ni bora nyumbani sio bora huku nje. Ikiwa mume wake sio mwanamume pekee ambaye atakuwa akimwona akiwa amevaa hivyo, basi heshima lazima itawale (1 Timotheo 2:9). Mwanamke anayetamani kumheshimu Bwana kwa mwili wake atavaa na kuenenda katika njia iletayo heshima kwa mume wake na kwa Bwana (Mithali 31:11-12).

Mungu alibuni ngono na kuitaja kuwa tendo la upendo kati ya mwanamume na mwanamke waliooana (Mwanzo 2:22-25). Lakini wanadamu waasi wameondoa utakatifu wake na kuupotosha kwa dhambi za ngono, ambazo baadhi yake zinaonekana katika mitindo fulani ya nguo za ndani. Wenzi wa ndoa Wakristo wanaotaka kudumisha utakatifu wa muungano wao wa ndoa watalinda mioyo yao dhidi ya kudharau kile ambacho Mungu anakiita kizuri. Ikiwa nguo za ndani au vitendo fulani vya ngono vinapinga usafi wa moyo wa mume au mke, chaguo hizo zinahitaji kubadilishwa kama njia ya kueshimiana kwa upendo.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Mwanamke Mkristo anaweza kuvaa nguo za ndani zinazochochea ngono kwa mumewe?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries