settings icon
share icon
Swali

Neema ya bure ni nini? Je! Theolojia ya neema ya bure ni gani?

Jibu


Theolojia ya Neema ya Bure kimsingi ni mtazamo wa soteriolojia (kanuni ya wokovu) iliyokuzwa kutoka kwa mizizi ya kimapokokeo ya Wabaptisti. Iliratibiwa na wanatheolojia kama vile Daktari Charles Ryrie na Zane Hodges katika miaka ya 1980, haswa kama jibu kwa theolojia ya Bwana au Wokovu wa Bwana, ambao una mizizi yake katika theolojia ya mabadiliko. Hii leo, Neema ya Bure inazidi kuimarika, ikiungwa mkono na sauti za Kikristo kama vile Tony Evans, Erwin Lutzer, Bruce Wilkinson, Chuo cha kibiblia cha Dallas (Dallas Theological Seminary), na Grace Evangelical Society.

Fundisho la msingi la Theolojia ya Neema ya Bure ni kwamba kuitikia “wito wa kuamini” katika Yesu Kristo kupitia kwa imani pekee ndio kitu kinachohitajika ili upokee uzima wa milele. Imani hii ya msingi na rahisi huleta uhakikisho wa “kuingia” katka ufalme wa Mungu. Kisha, ikiwa mtu anaitikia zaidi “mwito wa kumfuata” Yesu, anakuwa mwanafunzi na kupata utakaso. Mfuasi wa Kristo ana nafasi ya “kurithi” ufalme wa Mungu, ambao ni pamoja na kupokea thawabu hususani na kazi za Mungu ambazo alitimiza huku duniani.

Wanatheolojia wa Neema ya Bure wanaelekeza kenye vifungo kadri ili kuthibitisha tofauti yao ya kuwa na imani iokoayo na kumfuata Kristo, hasa kutoka kwa Injili ya Yohana na Nyaraka za Paulo. Kwa mfano, maelezo ya Yesu kwa mwanamke pale kisimani ya jinsi ya kupokea wokovu- kwamba angelimwomba yeye (Yohana 4:10)-inalinganishwa na meneno ya Yesu kwa wanafunzi dakika chache baadaye- kwamba lazima “kufanya mapenzi ya Mungu ambaye amenituma na kuikamilisha kazi yake” (Yohana 4:34).

Mistari mingine katika Injiliya Yohana inataja tendo la kuamini kuwa linahitajika kwa wokovu, ikiwa ni pamoja na Yohana 3:16 na Yohana 5:24. Na Yohana 6:47 inasema, “yeye anayeamini anao uzima wa milele.” Ukweli kwamba matendo hupelekea mtu kupewa dhawabu mbinguni unaweza oonekana katika vifungu kama Mathayo 5:1-15; 1 Wakorintho 3:11-15; na Waebrania 10:32-36, hasa mstari wa 36 ambao unasema, “Inawapasa kuvumilia ili mkiisha kufanya mapenzi ya Mungu mpate kile alichoahidi.”

Wanatheolojia wengi wa Mageuzi wanashangazwa na madai ya wanatheolojia wa Neema ya Bure, huku wakiwashutumu kwa “uaminifu rahisi” au hata kuwa kinyume na sheria. Kuwa sheria haifai katika wokovu ni imani potovu kwamba Mkristo hayuko chini ya sheria kwa vyovyote vile, iwe ya kibiblia au ya madili, na hivyo anaweza kufanya chochote anachotaka. Ukweli wa mambo ni kwamba theolojia ya Neema ya Bure inaweza kurahisisha kufikia imani ya kupinga sheria. Hata hivyo, mafundisho ya Neema ya Bure sio kuwa yako kinyume na sheria. Wanatheolojia wa Neema ya Bure wanachukulia msimamo wao kuwa wa kibiblia zaidi kuliko ule wa Wokovu wa Bwana, ambao wanauona kuwa theolojia inayotegemea matendo. Kwa mjibu wa wanatheolojia wa Neema ya Bure, Wokovu wa Bwana unashikilia kwamba imani inayookoa inajumuisha “tendo” asili la kukamilisha mabadiliko makubwa ya ndani yanoyoongoza kwa matendo mema.

Hii inaifanya Neema ya Bure kusisitiza uhakikisho wa wokovu, tena kulingana na ahadi ya kimsingi katika Injili ya Yohana, imani hiyo ndiyo inahitajika kwa wokovu. Kwa wanatheolojia wa Neema ya Bure, hili ni suala rahisi, limekwisha amriwa-ikiwa utaamini, utaokolewa. Kwa wanamrengo wa wokovu wa Bwana, uhakikisho wa wokovu unakuja katika kutunza mabadiliko kwa muumini anayekiri imani, kwa mfano, kwamba anatimiza matendo mema. Kila mrengo unauona mwingine kuwa unaelekeza katika upotovu.

Ingawa Theolojia ya Neema ya Bure na Wokovu wa Bwana ni maneno ambayo yamekuzwa hivi karibuni, yanawakilisha wasiwasi ambayo imekuwepo tangu mwanzo wa kanisa. Mwisho wa siku, hamna swali juu ya wokovu wa kimsingi wa wale wanaoshikilia mtazamo wowote ule. Mitazamo yote miwili bado iko katika mipaka ya ukweli. Bado, hii haimaanishi kuwa ni mjadala usio na maana. Imani ya mtu katika jambo hili inaweza kubadilisha maoni yake juu yake mwenyewe, Mungu, na uhakikisho wa wokovu kwa kiwango kikubwa.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Neema ya bure ni nini? Je! Theolojia ya neema ya bure ni gani?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries