settings icon
share icon
Swali

Je, wanawake katika Biblia walikuwa na chaguo kuhusu yule waliyemwoa?

Jibu


Ndoa nyingi zinazotajwa katika Biblia zilikuwa ndoa za kupangwa ambapo wazazi walihusika katika kuwachagulia watoto wao mwenzi. Taratibu za ndoa za kupanga zilitofautiana sana kutoka kwa familia moja hadi nyingine. Walakini, tamaduni nyingi zimezoea ndoa za mpangilio tangu nyakati za zamani. Kwa mfano, Ibrahimu alimwamuru mtumishi wake kumtafutia mwanawe Isaka mke (Mwanzo 24). Mtumishi huyo alimtafutia Isaka, Rebeka ambaye angeweza kuwa mke, lakini ni wazi kwamba Rebeka alipewa chaguo fulani kuhusu kama angekubali pendekezo hilo (Mistari 57-58).

Yakobo mwana wa Rebeka baadaye alipata mwanamke aliyempenda na akafanya mapatano na baba yake, Labani, ya kufanya kazi miaka saba ndio ampate Raheli katika ndoa (Mwanzo 29). Ingawa ndoa ilipangwa inaonekana kwamba Raheli na Yakobo walifuraia mpango huo.

Tofauti na ndoa za magharibi ambazo mara nyingi hujumuisha kuchumbiana kabla ya ndoa, mila ya kale ya Kiyahudi ilikuwa na zoea la kujizuia zaidi ambalo kwa kawaida lilitia ndani mvuto kati ya mwanamume na mwanamke, mapatano kati ya familia zao mbili, mahari iliyotolewa kwa familia ya mke, na sherehe ya harusi ya siku saba. Desturi ya Kiyahudi ya kuchumbiana ilipunguza uwezekano wa kufanya ngono kabla ya ndoa, na talaka haikutokea mara kwa mara.

Kwa ufupi, ndoa zilizopangwa zilikuwa za kawaida katika nyakati za kale, na Agano la Kale lina mifano kadhaa. Zoezi la ndoa iliyopangwa lilitokana na hisia kali ya familia na uaminifu ambao mara nyingi ulisaidia kutoa ahadi yenye nguvu zaidi kwa agano la ndoa. Hata hivyo, ndoa nyingi katika Biblia zilitegemea mpango rasmi ambapo mwanamume na mwanamke walitamani kuoana.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, wanawake katika Biblia walikuwa na chaguo kuhusu yule waliyemwoa?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries