settings icon
share icon
Swali

Mimi ni nani katika Kristo?

Jibu


Kwa mujibu wa 2 Wakorintho 5:17 , "Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Krisot amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama! Yamekuwa mapya." Kuna maneno mawili ambayo neno “mpya” limetafsiriwa katika Biblia. Kwanza , Neos , linahusu jambo ambalo limekwisha uumbwa, lakini tayari kunao mengine mengi yapo kama hilo. Neno limetafsiriwa "mpya" katika aya hii ni neno kainos, ambalo lina maana ya "kitu ambacho kimeundwa na tofauti na kitu kingine chochote katika kimewai kuwepo." Katika Kristo, sisi tumefanywa kuwa kiumbe kipya kabisa , kama Mungu aliumba mbingu na dunia awali -Yeye aliumba kutoka utubu, vivyo hivyo alituumba na sisi. Yeye hasafishi nafsi yetu ya zamani pekee; Yeye hufanya upya kiumbe chote. Wakati sisi tuko katika Kristo, sisi ni " washirika wa hali ya uungu " (2 Petro 1:4). Mungu mwenyewe, katika utu wa Roho wake Mtakatifu, anaweka makazi katika mioyo yetu. Sisi tuko katika Kristo na Yeye yu ndani yetu.

Katika Kristo, sisi tumefanywa wpya, uhuishwa, na kuzaliwa mara ya pili, na kiumbe hiki kipya ni nia ya kiroho, ambapo asili ya zamani ni nia ya mwili. Asili mpya ya ushirika na Mungu inaonyesha kutii mapenzi yake, na ni kujitoa kwa utumishi wake. Haya ni matendo ambayo asili ya zamani haina uwezo wa kufanya au kuwa. Asili ya zamani imekufa kwa mambo ya roho na haiwezi kujifufua yenyewe. Ni " wafu katika makosa na dhambi" (Waefeso 2:1) na inaweza tu kufanywa hai na kuamka kwa uamsho usio wa kawaida, ambayo hufanyika wakati sisi huja kwa Kristo na tumejazwa naye. Kristo hutupa sisi asili mpya kabisa na takatifu na maisha yasiyo na uaribifu. Maisha yetu ya kale, awali tukiwa wafu kwa Mungu kwa sababu ya dhambi, imezikwa , na sisi tumefufuliwa "kutembea maisha katika mapya ya uzima" pamoja naye (Warumi 6:4).

Kama sisi ni wa Kristo, sisi tumeunganishwa pamoja naye na hatumo tena watumwa wa dhambi (Warumi 6:5-6); sisi tumefanywa hai pamoja naye (Waefeso 2:5 ); sisi tumebadilishwa kw sura yake (Warumi 8:29); sisi tu huru kutokana na hukumu na hatutembei kwa jinsi ya mwili, bali mambo ya Roho (Warumi 8:1); na sisi ni sehemu ya mwili wa Kristo na waumini wengine (Warumi 12:5). Muumini sasa ana moyo mpya ( Ezekiel 11:19) na amebarikiwa "kwa kila baraka za kiroho katika sehemu ya mbinguni katika Kristo Yesu" (Waefeso 1:3).

Tunaweza kushangaa ni kwa nini hatuishi njia ambazo zimeelezwa, ingawa tumeyatoa maisha yetu kwa Kristo na tumepata uhakikisho kwa wokovu wetu. Hii ni kwa sababu asili yetu mpya inaishi katika miili yetu ya zamani ya kimwili, na hizi mbili zi katika vita kwa zenyewe. Asili ya zamani imekufa, bali asili mpya bado ina vita na wa zamani "hema" ambayo inakaa. Uovu na dhambi bado zipo, lakini muumini sasa anauona kwa mtazamo mpya na haumdhibiti tena vile hapo awali ulikuwa. Katika Kristo, sisi sasa tuko na uchaguzi wa kukataa dhambi, ambapo asili ya zamani haiwezi. Sasa tuna uchaguzi aidha wa kulisha asili mpya kwa njia ya neno , maombi, na utii, au kulisha nyama, kwa kupuuza mambo hayo.

Wakati sisi tuko katika Kristo, " sisi tu zaidi ya washindi kupitia Yeye aliyetupenda " ( Warumi 8:37) na tunaweza kufurahi katika Mwokozi wetu, ambayehufanya mambo yote yanawezekana (Wafilipi 4:13). Katika Kristo sisi tumependwa, tumesamehewa, na tu salama. Katika Kristo sisi tumenyakuliwa, fanywa haki, kukombolewa, kupatanishwa, na kuchaguliwa. Katika Kristo sisi ni washindi , kujazwa na furaha na amani , na nafasi ya maana ya kweli katika maisha. Kristo ni Mwokozi wa ajabu namna gani!

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Mimi ni nani katika Kristo?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries