settings icon
share icon
Swali

Je! Mwanadamu aliyeunganishwa atakuwa na roho?

Jibu


Matarajio ya kuunda binadamu kwa ajili ya uzazi huibua maswali mengi ya kiadili, maadili na kitabibu. Pia inagusia maswali ya kina y kitheolojia. Labda hamna la msingi zaidi kuliko hili: je! mwanadamu aliyeumbwa kisayansi atakuwa na roho?

Kwa wengine, jibu linaonekana kuwa wazi. Kwa wengine wanazo sababu za kustaajabu. Wengine huenda hatua kwamba wanadai kuwa uumbaji wa mwanadamu kisayansi ni jambo ambalo haliwezekani kwa sababu hakuna roho ambayo inaweza kuumbwa! Jinsi mtu anavyoliona suala hili hutegemea kanuni kuu, sana sana karibu na mtazamo wake wa jinsi nafsi inaumbwa. Kama ilivyo kwa masuala mengine ambayo sio ya wokovu, Biblia haitupi jibu la moja kwa moja. Katika hali hizo hatupaswi kuamini hilo bali kuwa waangalifu.

Kwa kusema hayo yote na kwa kulingana na vidokezo kadhaa vya kiroho, kisayansi, na vitendo, inaonekana kuwa jibu sahihi la ikiwa wanadamu walioumbwa kutokana na sayansi watakuwa na roho “hakika ni naam.”

Wakristo wana maoni kinzano kuhusu jinsi nafsi zisizo na mwili zinavyoumbwa. Kunao uungwaji wa kibiblia mara mbili wa suala hili, ijulikanayo (nafsi) bunifu na lile la kuwa nafsi ya watoto wachanga iliumbwa kutoka kwa wazazi wao katika utungaji mimba. La kwanza linasema kuwa Mungu anaumba nafsi wakati wa utungaji mimba wa mtoto. Mtazamo wa pili unasema utungaji wa mimba kupitia ngono ambao ni kupitia kwa wazazi huumba nafsi. Wengine wanaamini kuwepo kwa nafsi kabla ya chochote, sio mtazamo ulio sahihi kibiblia na kamwe hautaangaziwa hapa.

Kabla ya tulichunguze suala hili zaidi, ni muhimu kuweka masharti fulani. Hapa neno binadamu linarejelea mwanachama wa kibayolojia wa ukoo safu wa kisasa: nyenzo na chembechembe ya maumbile. Mtu hurejelea mtu aliyekamilika: akili, mwili, nafsi, na roho, kwa kusizitiza kipengele cha kiroho. Mwanadamu wa chembechembe kisayansi na mapaja MZ zinarejelea wanadamu waliumbwa kupitia kwa mchakato ulioelezewa hapa chini.

Katika uhamisho wa kinyukilia wa chemchechembe umbaji, kiini (kutuo cha mawasiliano) cha mayai ambayo haijarutubishwa huondolewa. Inabadilishwa na kiini cha mfadhili wa kiini kwenye kimechukuliwa kutoka kwa viumbe vinavyotumika kutengeneza kiumbe kingine. Hii seli mpya ambayo imetengezwa na kuchachawishwa na kuanza kuongezeka. Hii husababisha kiumbe chenye chembechembe (DNA) inayofanana na ile ya mfadhili. Katika uhamisho huu wa sayansi, ukuaji unafanyika katika masingira ya maabara na kutengeza viungu vya mwili. Katika uzao wa kawaida, ukuaji unafanyika katika tumbo la mama mrithi na unaweza kusababisha kuzaliwa kwa kiumbe kinachamfanana mfadhili wa mbegu.

Kuzungumza kibayolojia, tayari kuna kitu ambacho ni sawia na binadamu kinaishi. Mapacha wanaofanana, au mapacha wasiofanana (mapacha wa MZ), wao ni matokeo ya mchakato huu wa asili: manii moja na yai zinaungana na kutoa kiini kimoja cha kiini kilichotungishwa, na kuitwa kiumbe kichanga. Kisha hiki kiumbe kichanga hujigagwa sehemu mbili au viinitete tofauti zaidi, ambavyo vinakua kwa kujitegemea. Mapacha wa MZ kwa madhumuni yote ya vitendo ni kiini cha kila moja ya seli zenyewe.

Kwa maneno mengine, kibayolojia (kinasaba) wanadamu walioumbika kimaabala bado wapo. Utaratibu wa uumbaji wao ni tofauti sana na ule wa kutumia chembechembe kimsingi katika maabara, lakini matokeo ya mwisho ni yale yale. Hili ni jambo kuu la kukumbuka wakati wa kuchunguza mitazamo tofauti ikiwa kama nafsi za kimaabara zina roho au la. Msimamo wa mtu lazima uwe thabiti na utumike kwa uhamisha asili wa chembechembe kama vile mapacha wa MZ na wale amboa hatimaye wanaweza zaliwa kwa njia ya uzazi asili.

Mtazamo wa wale wanaoamini uumbaji kwa urahisi unathibitisha kwamba watu walioumbwa nche ya uzao wa asili wana roho, kuwa Mungu amejihuzisha moja kwa moja katika uumbaji wa kila nafsi kwa wakati ufaao. Pengine Mungu huijaza nafsi kwa kiumbe kichanga kilichotungishwa, kikiumba nafsi zaidi iwapo ikiwa kiumbe hicho kitajigagwa. Biblia haiko wazi, lakini kwa ajili ya suala hili, maelezo hayana umuhimu wowote. Kulingana na uumbaji wa roho, namna ya kuumba mwili wa kawaida hauna uhusiano na kujazwa kwake kwa nafsi. Ili kubuniwa, kuundwa, au vingenevyo, mtazamo wa uumbaji unasema kuwa Mungu ndiye anaumba nafsi, na hakuna sababu za kimaandiko au za kiroho za kufikiri kwamba hangefanya hivyo pamoja na wanadamu wote.

Wale wa mtazamo wa azazi ya asili, unaleta matatizo mengi. Kulingana na wana mtazamo wa azazi ya asili zote mwili roho vinarithiwa kutoka kwa wazazi. Hasa, inashikilia kwamba asili ya dhambi ya mtu hurithiwa kutoka kwa Adamu kupitia kwa baba yake. Hii inamaanisha kwamba pindi tu manii na yai huungana kuumba chembechembe za mwanadamu, vile vile nafsi pia imeumbwa. Lakini, katika kutumia seli za mwili, “wazazi” hawaitajiki na mtu mmoja tu anachangia chembe za urithi ambazo zinazidishwa. Hamna “utungaji” bali ni kuzidisha chembe zilizoko.

Hii inaibua maswali mengi kuhusu maambukizi ya nafsi kulingana na mtazamo kuwa nafsi huambukiswa kutoka kwa wazazi katika utungaji. Kwa mfano, mtu wa maambukizi hangekuwa na “baba” au “mama” katika maana ya kawaida. Matokeo ni kuwa binadamu angekuwa na DNA kutoka kwa mfadhili mmoja tu. Kwa maumbile, “baba” ambaye chembe yake ilitumika na baba mfadhili, na “mama” ambaye chembe yake imetumika nia mama mfadhili. Lakini kwa mjibu wa utungaji, kiumbe mwenyewe hawezi kuwa na wazazi kama hao. Ikiwa muunganiko wa kibayolojia wa kiini cha wazazi ndio huunda nafsi, ni wapi nafsi ya mshirika inaweza kutoka?

Njia hiyo hiyo ya kuhoji, ijapokuwa ni ya mtazamo wa uzazi asili, inapaswa kuzingatia nyakati zote dhana ya asili ya dhambi inayorithiwa kutoka kwa baba. Wa mtazamo wa azazi asili wanashikilia, kwa mfano, kwamba ilikua ukosefu wa baba wa kibinadamu ambao ulisababisha Yesu kuzaliwa bila asili ya dhambi. Ikiwa mtu mshirika akikosa baba halisi wa kibinadamu, je! asili ya dhambi ingenakiliwa kupitia DNA ya mshirika huyo? Kusema kweli, urithi wa asili ya dhambi ni swali tofauti na kupata nafsi na huibua mambo mengine mengi yaliyo na uwezekano wa kujadiliwa. Jambo ni kwamba, kama mtazamo wa azazi asili unashikilia kuwa nafsi na asili ya dhambi hupitishwa wakati wa utungaji mimba, na lazima iwe kwa hali zote (au isiwe) hivyo wakati wa kuwa na mtu mshirika.

Kumbuka, bila shaka, mtazamo wa mtu juu ya suala hili lazima uzingatie ushirika asili, kama vile mapacha fanana. Wakati wa utungaji mimba, kuna kiumbe kichanga kimoja. Baadaye, kunaweza kuwa na viwili, bila utungaji mimba zaidi kufanyika. Chache mno (ikiwa zipp) za mtazamo wa azazi asili zinapendekeza kwamba ni aina moja tu kati ya mapacha wawili au watatu ambao wana roho, au kwamba wanashiriki nafsi moja, kwa hivyo kuna haja ya kuwa na njia thabiti ya kutoa elezo kwa ajili ya nafsi kugagwanyika ambayo hushughulikia wanadamu wote waliumbwa kwa njia ya asili, ambayo inaweza kulinganishwa na mchakato wa kuumba kwa kutumia sayansi.

Kwa ufupi, mtazamo wa kurithi nafsi kutoka kwa wazazi unaacha nafasi ya kuhoji kuwa ikiwa manadamu wa ushirika (kimaabara) atakuwa na nafsi au la, ikiwa inatafusiriwa kumaanisha kuwa nafsi zinaumbwa kwa utungaji wa kibayolojia wenyewe. Kudai kuwa Mungu ndiye anayeamua wakati wa kuiweka nafsi, basi hautakuwa mtazamo wa nafsi kurithiwa kutoka kwa wazazi hadi kwa mtoto, bali ule wa ubunifu. Kwa kumjibu, yule anayeshikilia mtazamo wa nafsi kurithishwa mtoto na wazazi anaeza sema kwamba uumbaji wa nafsi ni kitu kinachotokea wakati mwanadamu- wa aina yeyote-anaumbwa, kwa njia yoyote ya kimwili. Iwe au isiwe kuwa hili linafaa kuchunguzwa kwa kina sana na kujadiliwa na kuachwa kwa mjadala tofauti.

Kwa njia inayoonekana, Wakristo wachache watapendekeza kwamba jinsi mtu alivyotungika inaweza kumuathiri mtu kiroho au kimaadili. Kwa mfano, madai ya kawaida kwamba uavyaji mimba unafaa kuruhusiwa “katika kisa cha ubakaji au kujamiana kwa maharimu” inamaanisha kwamba watu waliotungika chini ya hali kama hizo sio watu, sio binadamu kamili, watu wasio na faida au wasio na dhamani, ikilinganishwa na wale watu waliotukinga kwa njia “sahihi.” Huo ni mjadala wa kimaadili kuliko theolojia, lakini msimamo wetu lazima uwe thabiti. Ikiwa masingira ya utungwaji (au ukosefu wa utungwaji) unaathiri ikiwa kuwa mtu ana nafsi au la, basi maadili ya mtu au thamani ya kiroho kwa hikika ziko ili zinyakuliwe. Wakristo wanapaswa kuzingatia kwa makini msimamo wao kuhusu suala hili.

Hakuna jubu gumu na la haraka kwa swali la ikiwa mwanadamu aliyeumbwa ana nafsi au la. Baada ya kusema hayo, tafsiri nyingi za Biblia, na maana ya jumla ya theolojia, itapendekeza kuwa mwanadamu wa ushirika kwa kweli atakuwa na nafsi. Ni rahisi kuunda mfumo wa kitheolojia ambapo hawatakuwa na nafsi. Bado Wakristo wengi watapa mfumo huo ukijikanganya wenyewe na hauhitajiki.

Kukosa ufahamu kamili, tunawajibika kuwachukulia wanadamu wote kuwa watu kamili, walio na thamani na sio kwa manufaa pekee ambayo Mungu amewaweka katika uumbaji Wake (Zaburi 104:24) bali kwa upendo ambao Yeye anatarajia tuonyeshane (Yakobo 2:8). Hiyo ni pamoja na wanadamu walioumbwa kimaabara, iwe au isiewe kuwa mtu yu hai.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Mwanadamu aliyeunganishwa atakuwa na roho?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries