settings icon
share icon
Swali

Biblia inasema nini kuhusu nafsi kupumzika?

Jibu


"Nafsi kupumzika" ni imani kwamba baada ya mtu kufa, nafsi yake "hulala" mpaka ufufuo na hukumu ya mwisho. Dhana ya "roho kupumzika" si ya kibiblia. Wakati Biblia inaeleza mtu "kulala" katika uhusiano na kifo (Luka 8:52, 1 Wakorintho 15:6), haimaanishi usingizi halisi. Kulala ni njia ya kuelezea kifo kwa sababu mfu anaonekana kuwa amelala. Wakati sisi hufa, sisi hupatana na hukumu ya Mungu (Waebrania 9:27). Kwa waumini, kuwa mbali na mwili ni kuwa pamoja na Bwana (2 Wakorintho 5:6-8; Wafilipi 1:23). Kwa makafiri kifo kinamaanisha adhabu ya milele katika jehanamu (Luka 16:22-23).

Mpaka kufufuka kwa mwisho, hata hivyo, kuna mbinguni ya muda- peponi (Luka 23:43, 2 Wakorintho 12:04) na kuzimuni ya muda-ahera (Ufunuo 1:18; 20:13-14). Kama inavyoweza kuonekana wazi katika Luka 16:19-31, katika peponi wala katika ahera watu hawalali. inanaweza semekana kuwa, mwili wa mtu "unalala" huku nafsi yake ikiwa peponi au kuzimuni. Wakati wa ufufuo, mwili huu "utaamshwa" na kubadilishwa hadi mwili wa milele mtu atamiliki milele, hata kama ni mbinguni au kuzimu. Wale ambao walikuwa katika peponi watapelekwa mbingu mpya na nchi mpya (Ufunuo 21:1). Wale ambao walikuwa katika kuzimu kutupwa katika ziwa la moto (Ufunuo 20:11-15). Hizi ndizo hatima za mwisho na milele ya watu wote ikitegemea ikiwa mtu aliamini katika Yesu Kristo kwa ajili ya wokovu au la.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Biblia inasema nini kuhusu nafsi kupumzika?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries