settings icon
share icon
Swali

Je! Mzaha/kutaniana ni dhambi? Je! Biblia inasema nini kuhusu kufanya mzaha?

Jibu


Utani ni mada ya kuvutia na ni ngumu kuikadiria na kuijadili kama kitu kimoja. Kuzungumza Kibiblia, mzaha wenyewe hauchukuliwi kama dhambi, ingawa katika hali zingine inaweza kuwa hivyo. Mithali 18:21 inatuambia kwamba “Mauti na uzima viko katika uwezo wa ulimi, nao waupendao watakula matunda yake.” Yakobo 3:3-12 inalinganisha ulimi na lijamu katika kinywa cha farasi, usukani wa meli, na moto. Ulimi ni kitu chenye nguvu, na maneno yanaweza kuleta maisha makubwa au madhara makubwa. Kuna mzaha unaojenga. “Moyo wenye furaha ni dawa nzuri, bali roho iliyopondeka hukausha mifupa” (Mithali 17:22). Zaburi zimejaa marejeleo ya kicheko, kinachosababishwa na utani mzuri. Lakini pia kuna njia ya mzaha ambayo ni ya kudhalilisha na kudhuru, na tunahimizwa tusiruhusu “Maneno mabaya yasitoke vinywani mwenu, bali yale yafaayo kwa ajili ya kuwajenga wengine kulingana na mahitaji yao, ili yawafae wale wasikiao” (Waefeso 4:29).

Maneno yetu yanapaswa kumheshimu Mungu kila wakati na kutangaza kwamba tunathamini kile ambacho ameumba. Njia bora ya kujua kama utani wetu unakaribiana na wenye dhambi ni kumtafuta Roho Mtakatifu na kuomba usadikisho wake. Anaweza kutufanya tuwe wasikivu wakati mzaha unafaa na wakati ambapo huenda haufai. Ikiwa kuna shaka yoyote katika akili zetu, au ikiwa dhamiri zetu zinachomwa na mzaha wetu, labda ni bora kuachana nayo. Pia kuna suala la kuwafanya wengine wajikwae, ambalo tunaweza kufanya kwa urahisi kwa mizaha ambayo tunaweza kuhisi haina hatia kabisa, lakini ambayo wengine wanaona kuwa ya kuudhi au ya kuumiza. Uhuru wetu haupaswi kamwe kutumiwa kwa hasara ya dhamiri ya mtu mwingine (Warumi 14:13-17).

Utani wa mara kwa mara na mzaha, ikiwa ni sahihi, labda kwa sehemu kubwa hauna hatia. Lakini kuna wale wanaofanya mzaha mara kwa mara kiasi kwamba hawawezi kusema sentensi bila kuwa na mzaha wa aina fulani. Huo sio mtindo wa maisha unaofaa zaidi kwa Mkristo, hata hivyo kama tunavyoambiwa “tupate kuishi maisha ya kiasi, ya haki na ya utaua katika ulimwengu huu wa sasa” (Tito 2:12). Kama vile ilivyo katika “maeneo yote yasiyo wazi” katika maisha ya Kikristo, kutafuta hekima ya Mungu kuhusu usemi wetu ndiyo njia yenye faida zaidi ya kufuata (Yakobo 1:5).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Mzaha/kutaniana ni dhambi? Je! Biblia inasema nini kuhusu kufanya mzaha?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries