settings icon
share icon
Swali

Ni nini maana ya kuwa mwili mmoja katika ndoa?

Jibu


neno "mwili mmoja" linatokana na Mwanzo akaunti ya uumbaji wa Hawa. Mwanzo 2:21-24 inaelezea mchakato wa jinsi Mungu alimuumba Hawa kutoka ubavu uliochukuliwa kutoka upande wa Adamu akiwa amelala. Adamu alitambua kuwa Hawa ni sehemu yake hakika-walikuwa "mwili mmoja." Neno "mwili mmoja" lina maana kwamba kama miili yetu ni chombo kimoja kizima na haiwezi kugawanywa katika vipande na bado iwe mwili mmoja, hivyo ndivyo Mungu alinuia uhusiano wa ndoa uwe. Wao tena sio vitu viwili (watu wawili), lakini sasa kuna chombo kimoja (wanandoa). Kuna idadi ya mambo ya muungano huu mpya.

Mbali na kuingiza hisia, kitengo mpya kinachukua usukani juu ya uhusiano uliopita na ujao (Mwanzo 2:24). Baadhi ya washirika wa ndoa huendelea kuweka uzito mkubwa juu ya mahusiano na wazazi kuliko na mpenzi wao mpya. Hii ni kichocheo kwa ajili ya maafa katika ndoa na ni upotoshaji wa nia ya Mungu ya awali ya "kuachana na kuambatana." Tatizo sawia linaweza kutokea wakati mwanandoa huanza kumkaribia mtoto ili kukidhi mahitaji ya hisia badala ya mpenzi wake.

Kihisia, kiroho, kiakili, kifedha, na katika kila njia nyingine, wanandoa wanapaswa kuwa kitu moja. Hata kama vile sehemu moja ya mwili inajali sehemu zinginezya mwili (tumbo husiaga chakula kwa ajili ya mwili, ubongo unaongoza mwili kwa ajili ya mema ya yote, mikono hufanya kazi kwa ajili ya mwili, nk), hivyo kila mshirika katika ndoa ni mhudumu kwa wengine. Kila mwanaharusi hapaswi kuona fedha kuwa "zake pekee"; bali badala yake kama "zao". Waefeso 5:22-33 na Mithali 31:10-31 inatoa matumizi ya neno "umoja" na jukumu la mume na mke, sawia.

Kimwili, wanakuwa mwili mmoja, na matokeo ya mwili huo mmoja unapatikana katika watoto na muungano wao huzaa; watoto wenye miliki ya maumbile maalum, sawia na muungano wao. Hata katika nyanja ya ngono ya uhusiano wao, mume na mke hawafai kuchukulia miili yao kama yao wenyewe, bali kama mali ya mpenzi wao (1 Wakorintho 7:3-5). Wala wao kuzingatia radhi yao wenyewe, bali kutoa furaha hiyo kwa wenzi wao.

Umoja huu na hamu ya kufaidishana kila mmoja si ya moja kwa moja, hasa baada ya mwanadamu kuanguka katika dhambi. Mume katika Mwanzo 2:24, anambiwa "aambatane" na mke wake. Neno hili lina mawazo mawili ndani yake. Moja ni kuwa "kushikanishwa" na mke wake, picha ya jinsi ambavyo ndoa inapaswa kuwa dhabiti. Sababu nyingine ni "kukaza mbele kwa sababu ya" mke. Hii "kutafuta mke kwa bidii" ni kwenda zaidi ya uchumba na kusababisha ndoa, na inafaa kuendelea katika ndoa. Tabia ya mwili ni "kufanya kile unahisi ni kizuri kwangu" badala ya kufikiria ni nini kitafaidisha mke. Na huu ubinafsi ndio chanzo cha ndoa kuvunjika mara moja pindi tu "fungate imeisha." Badala ya kila mwanandoa kushinda kulalama jinsi mahitaji yake mwenyewe hayafikiwi, yeye anapaswa kundelea kulenga katika kukidhi mahitaji ya mwenziwe.

Inaweza kuwa vizuri kwa watu wawili kuishi pamoja kukidhi mahitaji ya kila mmoja, Mungu ana wito zaidi kwa ndoa. Vile walikuwa wanamtumikia Kristo na maisha yao kabla ya ndoa (Warumi 12:1-2), sasa wao wanapaswa kumtumikia Kristo pamoja kama kitengo kimoja na kulea watoto wao kumtumikia Mungu (1 Wakorintho 7:29-34, Malaki 2: 15; Waefeso 6:4). Priska na Akila, katika Matendo 18, watakuwa mfano mzuri wa hili. Wanandoa wanapotafuta kumtumikia Kristo pamoja, furaha ambayo Roho huleta itajaza ndoa yao (Wagalatia 5:22-23). Katika Bustani ya Edeni, kulikuwa na watu watatu (Adamu, Hawa, na Mungu), na kulikuwa na furaha. Hivyo, kama Mungu ni mkuu katika ndoa hiileo, kuna pia kutakuwa na furaha. Bila Mungu, kama hakuna umoja wa kweli na kamili kamwe haiwezekani.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Ni nini maana ya kuwa mwili mmoja katika ndoa?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries