settings icon
share icon
Swali

Je inamaanisha nini kuwa tunapaswa kuwa wepesi wa kusikiliza na si wepesi wa kuongea (Yakobo 1:19)?

Jibu


Yakobo 1:19-20 inasema, “Ndugu zangu wapendwa, fahamuni jambo hili: Kila mtu awe mwepesi wa kusikiliza, lakini asiwe mwepesi wa kusema wala wa kukasirika. Kwa maana hasira ya mwanadamu haitendi haki ya Mungu.” Kuwa “mwepesi wa kusikiliza” inamaanisha kwamba tunajizoeza kusubiri habari nzima kabla ya kutoa maoni. “Mpole wa kusema” ni upande mwingine wa kuwa mwepesi wa kusikiliza. Tunadhibiti maneno yetu na sio kuongea kwa sauti kila kitu kinachokuja katika vichwa vyetu.

Yakobo anaendelea na kuongelea juu ya ulimi: “Kama mtu akidhani ya kuwa anayo dini lakini hauzuii ulimi wake kwa hatamu, hujidanganya moyoni mwake, wala dini yake mtu huyo haifai kitu” (Yakobo 1:26). Baadaye anatuonya kuhusu kuzuia ndimi zetu: “Vivyo hivyo ulimi ni kiungo kidogo sana katika mwili, lakini hujivuna majivuno makuu. Fikirini jinsi moto mdogo unavyoweza kuteketeza msitu mkubwa! Ulimi pia ni moto, ndio ulimwengu wa uovu kati ya viungo vya mwili. Ulimi huutia mwili wote wa mtu unajisi na kuuwasha moto mfumo mzima wa maisha yake, nao wenyewe huchomwa moto wa jehanamu” (Yakobo 3:5-6).

Vinywa vyetu hutuingiza katika shida nyingi. Tunakiri kuamini kitu kimoja, lakini mara nyingi tunasalitiwa na kile hutoka kwa vinywa vyetu. Yesu alisema, “Kwa maana kinywa cha mtu huyanena yale yaliyoujaza moyo wake” (Mathayo 12:34).

Wakati tunajipa nidhamu ili tusikilize zaidi kuliko kuongea, tunaweza kujifunza mengi. Wanaozungumza sana ni wagumu kufundishwa. Wao wanafikri kwamba tayari wanajua kila kitu wanachohitaji kujua, na daima wanatoa maoni yao. Watu wenye hekima wamejifunza kwamba hekima zaidi inaweza patikana kwa kusikiliza, kutizama, na sio kukimbilia kuhukumu. Mithali 10:19 inasema, “Wakati maneno ni mengi, dhambi haikosekani, lakini yeye ambaye huzuia ulimi wake ni mwenye busara.”

Msemo wa zamani uko sawa: “Ni afadhali kubaki kimya na kudhaniwa kuwa mjinga kuliko kufungua mdomo na kuondoa shaka zote.” Ni mahusiano mangapi yameharibika kwa sababu hatukuwa wepesi wa kusikiliza wala wapole kwa kuongoea? Je, ni makosa ngapi yangeepukika kama tungesikiliza badala ya kuongea?

Tunapaswa kuwa waangalifu kuhusu aina ya watu tunaotumia muda mwingi kuwasikiliza. Zaburi 1 inatuonya kuwa tusiwasikilize wapumbavu au waovu. Walakini, kunao watu wengine ambao tunapaswa kuwasikiliza kwa uepesi:
• Wazee kwa sababu ya usoefu wao (Waebrania 13:17).
• Watu wenye busara kwa sababu ya ushauri wao mzuri (Mithali 13:20).
• Watu wanaomcha Mungu kwa sababu wanaweza wakilisha mtazamo wa Mungu katika hali zetu (Zaburi 141:5).
• Mamlaka kwa sababu wanawakilisha sheria (Warumi 13:1).

Wengi wetu si wepesi wa kusikiliza, lakini tunaweza kujifunza kuwa wasikilizaji bora zaidi. Usikilizaji mzuri huwa tendaji. Unahusisha mnenaji. Unaelewa mtazamo wa mnenaji, hata kama hatukubaliani. Wakati watu wanahisi wamesikizwa, wako tayari kusikiliza mtazamo wetu. Kuwa mwepesi wa kusikiliza hakika hufungua milango ya mawasiliano kwa sababu usikilizaji unaonesha heshima, na wakati watu wanahisi kuheshimika, kuna uwezekano kuonyesha heshima hiyo pia na kutusikiliza. Ni muhimu kwetu kuwa wepesi wa kusikiliza na si wepesi wa kuongea. Siku zote Neno la Mungu hutuonyesha njia bora zaidi, na tunapoifuata, tunabarikiwa.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je inamaanisha nini kuwa tunapaswa kuwa wepesi wa kusikiliza na si wepesi wa kuongea (Yakobo 1:19)?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries