settings icon
share icon
Swali

Mwenendo wa Kikristo una umuhimu katika jinsi ulimwengu usioamini unavyomtazama Kristo?

Jibu


Hii hapa ni jibu rahisi kwa swali la ni jinsi gani tabia ya Mkristo ni muhimu: la muhimu sana! Biblia imejaa vifungu vinvyounganisha tabia ya Mkristo na jinsi ulimwengu unavyomwona Kristo. “Vivyo hivyo, nuru yenu iangaze mbele ya watu, ili wapate kuona matendo yenu mema wamtukuze Baba yenu aliye mbinguni” (Mathanyo 5:16). “Kwa sababu ya huduma ambayo mmejithibitisha wenyewe, watu watamtukuza Mungu kwa ajili ya utiifu ufuatanao na ukiri wenu wa Injili ya Kristo, na kwa ukarimu wenu wa kushiriki pamoja nao na pia wengine wote” (1 Wakorintho 9:13). “Kuweni na mwenendo mzuri mbele ya watu wasiomjua Mungu, ili kama wanawasingizia kuwa watenda mabaya, wayaone matendo yenu mema nao wamtukuze Mungu siku atakapokuja kwetu” (1 Petro 2:12).

Ikiwa tunaweza kulinganisha Ukristo na sinema, matendo yetu mema yanaweza kuonekana kama vidokezo vya sinema. Wakati wasioamini wanapoona upendo ambao Wakristo wanao kati yao na matendo mema wanayoyafanya, wanaweza kuwaza aina yote ya mouvu juu ya Wakristo, lakini hawawezi kukosoa mwenendo wao, ni hii huleta utukufu kwa Mungu. Na hata katika kueneza kwetu injili na kuitetea imani, tunapaswa kufanya hivyo kwa ukarimu na heshima (1 Petro 3:15), na sio kwa hasira na sauti za majivuno.

Ukweli wa mambo ni kwamba injili tayari chukizo kwa ulimwengu usioamini (1 Wakorintho 1:18); Wakristo hawapaswi kuongezea chukizo hilo. Hisia hii inaonekana wazi katika waraka wa kwanza wa Petro. Anawahimiza wasomaji wake kwamba, ikiwa watateswa mikononi mwa watu waovu, iwe kwa sababu wao ni Wakristo na si kwa sababu walikuwa wakitenda dhambi (1 Petro 4:14-16).

Sehemu nyingine nzuri ya Maandiko ambapo jambo hili limewekwa wazi ni katika nyaraka ya Paulo kwa Tito. Katika sura ya pili, Paulo anampa Tito maagizo ya jinsi ya kufundisha kutaniko lake. Katika sehemu tatu tofauti katika mlango huu, anaonyesha jambo tunalozungumzia hapa. Paulo anamsihi Tito awafundishe wanawake wadogo “wawe waaminifu, watakatifu, wakitunza vyema nyumba zao, wema, watiifu kwa waume zao, ili mtu yeyote asije akalikufuru neno la Mungu” (Tito 2:5). Vile vile anamhimiza Tito “Katika kila jambo uwe kielelezo kwa kutenda mema. Katika mafundisho yako uonyeshe uadilifu, utaratibu, na usemi sahihi usio na lawama, ili wanaokupinga watahayari, wakose neno lolote mbaya la kusema juu yetu” (Tito 2:7-8). Na mwisho, Paulo anamwihimiza Tito awaonye watumwa “Wafundishe watumwa kuwatii mabwana zao katika kila jambo, wakijitahidi kuwapendeza wala wasijibizane nao, wala wasiwaibie, bali waonyeshe kuwa wanaweza kuaminika kabisa, ili kwa kila namna wayafanye mafundisho ya Mungu Mwokozi wetu yawe ya kuvutia” (Tito 2:9-10). Katika hivi visa vitatu, Paulo anaonyesha kwamba mwenendo wa Kikristo ni muhimu sio katika kunyamazisha mwenye dhambi tu, bali pia katika kulinda uaminifu wa Neno la Mungu.

Fikiria njia mbadala. Ikiwa mienendo ya Wakristo sio tofauti na ya ulimwengu, hiyo ina faida gani? Ikiwa kweli ulimwengu huku nje unatazama na kuona kuwa hamna tofauti kati yao na Wakristo, kutakuwa na motisha kwao ya kuachana na maisha yao ya kutoamini? Kiasili mwenye dhambi anachukukia mambo ya Mungu (1 Wakorintho 2:14; Warumi 8:7-8). Ikiwa Wakristo wataishi jinsi ulimwengu usioaini unavyoishi, basi tunachofanya ni kukaribisha dharau na mashtaka ya unafiki.

Kwa hakika, hakuna asiyeamini atakayeokolewa kwa matendo mema ya Mkristo; ni lazima wahubiriwe injili. Zaidi ya hayo, sote tunajua kwamba hata katika uwezo wetu sisi tuko katika hatari ya kutenda dhambi. Hata hivyo injili inaweza kupokewa vyema ikiwa imewasilishwa na mtu mnyenyekevu na mpole kuliko mtu asiye na adabu na heshima. Matendo yetu yanaweza kusaidia au kuzuia injili kuenezeka.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Mwenendo wa Kikristo una umuhimu katika jinsi ulimwengu usioamini unavyomtazama Kristo?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries