settings icon
share icon
Swali

Je, mwanadamu anaweza kuishi bila Mungu?

Jibu


Kinyume na madai ya hawamwamini Mungui na agnostiki katika karne, mwanamu hawezi kuishi bila Mungu. Mwanadamu anaweza kuwa na kuwepo kwa hali ya kufa bila kumjua Mungu, lakini si bila ukweli wa Mungu .

Kama Muumba, Mungu alianzisha maisha ya binadamu. Kusema kwamba mwanadamu anaweza kuwepo mbali na Mungu ni kusema kwamba mwangalizi anaweza kuwepo bila mwanzilishi wa ulinzi au hadithi unaweza kuwepo bila mtoa hadithi. Deni ya uhai wetu ni kwa Mungu ambaye kweye tumeumbwa kwa mfano wake (Mwanzo 1:27). Kuwepo kwetu kunategemea Mungu, kama sisi hukiri kuwepo kwake au la.

Kama mtunzaji, Mungu huendelea kupeana maisha (Zaburi 104:10-32). Yeye ni uzima (Yohana 14:6), na viumbe vyote vimeunganishwa pamoja na mamlaka ya Kristo (Wakolosai 1:17). Hata wale walio mkufuru Mungu hupokea riziki yao kutoka kwake: "Yeye huwaangazia jua lake waovu na wema, huwanyeshea mvua wenye haki na wasio haki" (Mathayo 5:45). Kufikiri kuwa mwanadamu anaweza kuishi bila Mungu ni kudhani kwamba alizeti litaendelea kuishi bila mwanga au ua bila maji.

Kama Mwokozi, Mungu anatoa uzima wa milele kwa wale wanao amini. Katika Kristo kuna maisha, ambayo ni mwanga wa wanadamu (Yohana 1:4). Yesu alikuja ili tuweze kuwa na maisha "na kuwa nayo tele" (Yohana 10:10). Wote ambao wanamwamini wameahadi uzima wa milele na Mungu (Yohana 3:15-16). Kwa mwanadamu kuishi- maisha ya kweli lazima amujue Kristo (Yohana 17:3).

Bila Mungu, mwanadamu ana maisha ya kimwili pekee. Mungu aliwaonya Adamu na Hawa ya kwamba siku wao wangemkataa hakika wangeweza "kufa" (Mwanzo 2:17). Kama tujuavyo, hawakumtii Mungu, lakini hawakufa siku hiyo kimwili, badala yake, walikufa kiroho. Kitu ndani yao kilikufa- maisha ya kiroho waliyokuwa wakijua, ushirika na Mungu, uhuru wa kufurahia kwake, kutokuwa na hatia na usafi wa nafsi zao- na zote zilitoweka.

Adamu, ambaye alikuwa ameumbwa kuishi na kuwa na ushirika na Mungu, alilaaniwa na kuwepo na mwili wa hatia. Chenye Mungu alikusudia kitoke mavumbini hadi utukufu sasa kikawa kienda kutoka hadi vumbini. Kama Adamu, mwanadmu bila Mungu leo hii bado afanya kazi katika kuwepo kwa kidunia. Mtu kama huyo anaweza kuonekana kuwa na furaha, hata hivyo, kuna starehe na furaha kwa kuwa katika maisha haya. Lakini hata hivyo viburudisho na raha haviwezi kupokewa kikamilifu bila uhusiano na Mungu.

Baadhi ya wanao kufuru Mungu huishi maisha ya upotovu na raha. Shughuli zao za mwili zinaonekana kutojali na kuridhisha kuwepo kwao. Biblia inasema kuna kipimo fulani cha furaha unaweza kuwa nayo katika dhambi (Waebrania 11:25). Tatizo ni kwamba ni kwa muda; maisha katika dunia hii ni mafupi (Zaburi 90:3-12). Mapema au baadaye, wanao angamia, kama mwana mpotevu katika mfano, wanaona kwamba furaha ya kidunia ni endelevu (Luka 15:13-15).

Si kila mtu ambaye anamkataa Mungu anatafuta raha tupu, hata hivyo. Kuna watu wengi wasiokoka ambao wanaishi maisha ya nidhamu, kiasi, furaha na ya uridhisho. Biblia inatoa baadhi ya kanuni za maadili ambazo zitafaidisha mwanadamu yeyote katika dunia hii uaminifu, kujizuia, nk. Lakini tena, bila Mungu mwanadamu ana dunia tu pekee. Kupita vizuri njia ya maisha haya sio uhakika kwamba sisi tuko tayari kwa maisha ya baadaye. Angalia mfano wa mkulima tajiri katika Luka 12:16-21 na mfano wa Yesu wa tajiri (lakini kwa maadili sana) kijana katika Mathayo 19:16-23.

Bila Mungu, mwanadamu hajakamilika, hata katika huu mwili unaokufa. Mwanadamu hana amani na mwanadamu mwenzake kwa sababu yeye hana amani yeye mwenyewe. Mwanadamu anahangaika kwa nafsi yake mwenyewe kwa sababu yeye hana amani na Mungu. Kutekeleza azma furaha katika historiaya wamegundua kwamba upotovu wa muda wa maisha wapisha njia ya kukata tamaa zaidi. Hisia sumbufu kwamba "kuna kitu kibaya" ni vigumu kuitupilia mbali. Mfalme Sulemani alijitoa mwenyewe kwa harakati za vyote ambavyo dunia hii inatoa, na alikumbukumbu matokeo yake katika kitabu cha Mhubiri.

Sulemani aligundua kuwa maarifa, katika yenyewe, ni bure (Mhubiri 1:12-18). Akakuta radhi na mali ni ubatili (2:1-11), vitu nivanyo vionekanavyo ni ujinga (2:12-23), na utajiri unapita (Sura ya 6).

Sulemani anahitimisha kwamba maisha ni zawadi kutoka kwa Mungu (3:12-13) na njia ya hekima ya kuishi ni kumcha Mungu: "Hii ndiyo jumla ya maneno yote yamekwisha sikiwa; Mche Mungu, nawe uzishike amri zake, maan kwa jumla dniyo impasayo mtu. Kwa maan Mungu ataleta hukumuni kila kazi, pamoja na kilaneno la siri likiwa jema au likiwa baya"( 12:13-14).

Kwa maneno mengine, kuna maisha zaidi kuliko mwelekeo wa kimwili. Yesu anasisitiza hatua hii wakati Anasema, "Mtu hataishi kwa mkate tu, ila kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu" (Mathayo 4:4). Si mkate (kimwili) lakini neno la Mungu (kiroho) inaendelea kutuweka hai. Ni bure kwetu kujioji wenyewe kwa kutafuta tiba ya taabu zetu zote. Mwanadamu anaweza tu kupata uridhisho wa maisha na ukamilifu wakati anamkubali Mungu.

Bila Mungu , hatima ya mwanadamu ni moto wa Jehanamu. Mwanadamu bila Mungu amekufa kiroho, wakati maisha yake ya kimwili yameisha, anakabiliwa na utengano milele na Mungu. Katika hadithi ya Yesu ya tajiri na Lazaro (Luka 16:19-31), tajiri anaishi maisha ya utamu ya urahisi bila kumuwaza Mungu, huku Lazaro akiteseka katika maisha yake, lakini anamjua Mungu. Ni baada ya vifo vyao kwamba wote wawili kweli walielewa uzito wa uchaguzi wao walifanya katika maisha. Tajiri aligundua akiwa amechelewa, kwamba kuna maana zaidi ya maisha kuliko harakati za mali. Wakati huo huo, Lazaro akifajiwa peponi. Kwa hao wawili, muda mfupi wa maisha yao ya kidunia yalitoweka kwa kulinganisha na hali ya kudumu ya nafsi zao.

Mwanadamu ni kiumbe cha kipekee. Mungu ameweka akili ya milele katika mioyo yetu (Mhubiri 3:11), na kwamba maana ya hatima ya wakati wote inaweza tu kupata utimilifu wake katika Mungu mwenyewe.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, mwanadamu anaweza kuishi bila Mungu?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries