settings icon
share icon
Swali

Je! mvutio kingono wa jinsia moja ni dhambi?

Jibu


Katika Mathayo 5:27-28, Yesu analinganisha tamaa na uzinzi. Hii inaanzisha kanuni ya kibiblia: ikiwa ni dhambi kufanya jambo fulani, pia ni dhambi kutamani kufanya jambo hilo. Biblia inasema waziwazi kwamba ushoga ni dhambi (Walawi 18:22; 20:13; Warumi 1:26-27; 1 Wakorintho 6:9). Kwa hiyo, ni dhambi pia kutamani kufanya vitendo vya ushoga. Je! hii inamaansiha kuwa mvuto wa jinsia moja ni dhambi? Ili kujibu hili, ni lazima tutofautishe kati ya dhambi inayotenda kazi na hali tulivu ya kujaribiwa.

Si dhambi kujaribiwa. Yesu alijaribiwa, lakini hakutenda dhambi (Mathayo 4:1; Waebrania 4:15). Hawa alijaribiwa katika bustani, na kwa hakika lile tunda alilokatazwa alipata kuwa la kupendeza, lakini inaonekana kwamba hakutenda dhambi hadi alipolichukua tunda na kula (Mwanzo 3:6-7). Kupambana na majaribu kunaweza kusababisha dhambi, lakini pambano hilo sio dhambi yenyewe.

Tamaa kwa watu wa jinsia tofauti ni dhambi (Mathayo 5:27-28), lakini kuvutiwa na watu wa jinsia tofauti si dhambi. Ni kawaida na asili kwa wanaume kuvutiwa na wanawake, vile vile na wa kike. Hakuna kamwe kitu kibaya kwa watu kuvutiwa na jinsia tofauti. Inakuwa dhambi ikiwa mvuto huo utageuka kuwa tamaa. Mara tu mvuto huo unapopanuka na kuwa tamaa ya kufanya jambo la uasherati, inakuwa dhambi moyoni.

Ushoga ni tofauti. Tabia ya ushoga katika muktadha wowote ni kitendo ambacho Biblia inakataza. Lakini, kuacha tabia hiyo, je, kuvutiwa na watu wa jinsia yako ni dhambi? Kuzungumza kwa upana, tamaa yoyote ya kitu ambacho Mungu amekataza na ni matokeo ya dhambi, kwa njia hii: dhambi imenea ulimwengu na asili zetu kwamba kile ambacho ni kiovu mara nyingi huonekana kuwa kizuri kwetu. Tumeambukizwa dhambi, na dhambi hutufanya tuwe na mawazo, tamaa na maelekeo yaliyopotoka na yaliyo kombo. Kiasili sisi ni wenye dhambi (Warumi 5:12). Hisia za kuvutiwa na wale wa jinsia kama yako, kwa kila mtu, sio dhambi mara nyingi ambayo iko kazini, bali ni dhambi ya makusudi ambayo imekita mizizi katika asili iliyoanguka. Mvuto kwa jinsia kama ile yako, kwa kiwango fulani, ni dhihirisho la hali ya dhambi.

Mchungaji na mwantheolojia John Piper ana maeneno ya utambuzi kuhusu suala la kuvutiwa na watu wa jinsia yako: “ingekuwa sawa kuseam kwamba tamaa za watu wa jinsia moja ni dhambi kwa maana ya kwamba zimevurugwa na dhambi na ziko kinyume na mapenzi ya Mungu yaliyofunuliwa. Lakini kusababishwa na dhambi na kukita mizizi katika dhambi hakufanyi tamaa ya dhambi kuwa sawa na kutenda dhambi. Kutenda dhambi ni kile kinachotokea wakati uasi dhidi ya Mungu unapojidhihirisha kupitia machafuko yetu” (kutoka kwa mahubiri “Ndoa na idumishwe kwa heshima/Let Marriage Be Held in Honor,” Juni 16, 2012).

Kipindi cha kuvutiwa na jinsia yako kimapenzi, hata kama kinajirudia rudia, kinawekwa vyema kama kishawishi, na si kama dhambi. Ikiwa wakati huo wa ghafla, wa muda mfupi unaruhusiwa kugeuka kuwa kitu kingine zaidi-jaribu la kupita linakuwa nia ya tamaa-basi limekuwa dhambi. Je! ni wakati gani majaribu yanakuwa dhambi ya moyo? Ili kuliuliza kwa njia nyingine, tunaweza kustahimili majaribu kwa muda gani kabla ya kugeuka kuwa mawazo mabaya? Haiwezekani jibu kubainishwa. Tunajua hili: ni lazima sote tugeuzwe kwa kufanywa upya nia zetu (Warumi 12:2) na “tukiteka nyara kila fikira ipate kumtii Kristo” (2 Wakorintho 10:5).

Kwa sababu ya asili ya dhambi ambayo mwanadamu ako nayo, mvuto wa jinsia moja unaweza kuhisika kuwa “kawaida” kwa wengine, lakini ni upuzi kusema kwamba dhambi, ikiwa inakuja “kwa kawaida” inapaswa kukumbatiwa. Je! ni sawa kwa mtu mwenye tabia ya kukasirika kuwakasirikia wengine? Je! ni sawa kwa wazimu wa kuiba vitu kuiba? Je! Ni vyema mume kufanya uzinzi kwa sababu hamu kubwa ya ngono ni sehemu ya hali yake? La hasha. Watu huenda kila wakati hawawezi kujizuia jinsi au vile wanavyo hisi, lakini wanaweza kuzuia kile wanachofanya na hisia hizo (1Petro 1:5-8). Na sisi wote tuna jukumu la kuyapinga majaribu (Waefeso 6:13).

Watoto wa Mungu wanapaswa kufikiri na kutenda tofauti na ulimwengu. Wengi ulimwenguni wanakubali mvuto wa jinsia yao na ushoga kama jambo la kawaida la kijamii, lakini viwango vya maisha vya Mkristo vinapaswa kutoka kwa Biblia, sio hekima ya kawaida (2 Timotheo 3:16-17). Tunaishi ulimwenguni, na kwa hivyo tunapitia majaribu kila siku. Tumeanguka katika asili ya dhambi, na hivyo tunapambana dhidi ya tamaa zisizo za Mungu. Wakristo wengine wanapambana dhidi ya jaribu la kutenda kulingana na mvuto wa jinsia moja. habari njema ni kwamba ushindi unawezekana. “Kwa maana kila aliyezaliwa na Mungu huushinda ulimwengu. Huku ndiko kushinda kuushindako ulimwengu, yaani, hiyo imani yetu” (1 Yohana 5:4).

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! mvutio kingono wa jinsia moja ni dhambi?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries