settings icon
share icon
Swali

Ni kwa nini Mungu ni Mungu wa wivu?

Jibu


Ni muhimu kuelewa jinsi neno “wivu” limetumika. Matumizi yake katika Kutoka 20:5 katika kuelezea Mungu ni tofauti na jinsi limetumika kuelezea dhambi ya wivu (Wagalatia 5:20). Wakati sisi tunalitumia neno “wivu”, tunalitumia kuwa na maana ya tama ya kitu cha mtu ambacho hatuna. Mtu anaweza kuwa na wivu au kumwonea ngoyo mtu mwingine kwa sababu yeye ana gari zuri au nyumba (miliki). Au mtu anaweza kuwa na wivu au tamani mtu mwingine kwa sababu ya baadhi ya uwezo au ujuzi huyo mtu mwingine anao (kama vile uwezo wa riadha). Mfano mwingine ni ule kwamba mtu mmoja anaweza kuwa na wivu au tamaa ya mwingine kwa sababu ya urembo wake.

Katika Kutoka 20:05, siyo kwamba Mungu ana wivu au tamaa kwa sababu mtu ana kitu ambacho anahitaji. Kutoka 20:4-5 inasema, “Usijifanyie sanamu kwa ajili yako mwenyewe kwa mfano wowote mbinguni wala duniani au katika chini ya maji. Wala kujiinamisha mbele yao au ibada yao, kwa kuwa mimi, Bwana, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu ...” Onyo ni kwamba Mungu ni wa wivu wakati mtu anatoa kitu kwa mwingine ambacho ni haki kwake.

Katika mistari hii, Mungu anazungumza juu ya watu wanaotengeneza sanamu na kuziinamia kwa kuziabudu badala ya kumpa Mungu ibada anayostahili peke yake. Mungu anamiliki ibada na huduma ambayo ni yake. Ni dhambi (kama Mungu anavyosema katika amri hii) kuabudu au kutumikia kitu kingine chochote zaidi ya Mungu. Ni dhambi wakati tunatamani, au kuonea kinyongo, au tunapo kuwa na wivu kwa mtu kwa sababu yeye ana kitu ambacho hatuna. Ni matumizi mbalimbali ya neno “wivu” wakati Mungu anasema yeye ni wivu. Kile kinacho mtia wivu ni mali yake; ibada na huduma ni mali yake peke yake, na zinastahili kutolewa kwake Mungu pekee.

Labda mfano wa vitendo utatusaidia kuelewa tofauti ilioko katika majina hayo. Kama mume anamwona mume mwingine anampapasa mkewe kimapenzi, yeye ana haki ya kuwa na wivu, kwa sababu ni yeye tu ana haki ya kumpapasa mke wake. Aina hii ya wivu si dhambi. Badala yake, ni sahihi kabisa. Kuwa na wivu kwa kitu ambacho Mungu anatangaza kuwa mali yenu ni nzuri na sahihi. Wivu ni dhambi wakati una hamu ya kitu ambacho si mali yenu. Ibada, sifa, heshima na utukufu ni mali ya Mungu peke yake, kwa sababu yeye pekee ndiye anastahili. Kwa hivyo, Mungu ana uhuru wa kuwa na wivu wakati ibada, sifa, heshima, au utukufu zinatolewa sanamu. Hii ni hasa ndio wivu Mtume Paulo anaelezea katika 2 Wakorintho 11:2,”Mimi nimeona wivu kwa ajili yenu na ni wivu wa Mungu.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Ni kwa nini Mungu ni Mungu wa wivu?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries