settings icon
share icon
Swali

Je Mungu ana ucheshi?

Jibu


Pengine ishara bora ya kuonyesha kuwa Mungu huwa na ucheshi ni ile kwamba aliumba mwanadamu kwa mfano wake (Mwanzo 1:27), na hakika watu waneza kuona na kuonyesha ucheshi. "Hisia ya ucheshi" inaweza fafanuliwa kuwa "uwezo wa kuwa na ufahamu wa kitu, kuwa na furaha, au kusema kile ambacho ni cha ucheshi." Kulingana na hii fafanuzi, hivyo Mungu lazima aonyeshe uewezo wa kufahamu, furahia, au kuonyesha kilicho cha ucheshi. Jambo gumu ni kwamba watu wanaona ucheshi huo tofauti, na chenye mwanadamu mwenye dhambi anaelewa kuwa ucheshi hakiwezi kumpendeza Mungu aliye mtakatifu na mkamilifu. Mengi ya yale ulimwengu huita ucheshi sio ucheshi bali ni upumbavu na chungu na hayafai kuwa sehemu yoyote ya maisha ya Mkristo (Wakolosai 3:8). Cheshi zingine hudhihirishwa kwa gharama yaw engine (kuwakejeli badala ya kuwainua), pia hicho ni kitu kilicho kinyume na Neno la Mungu (Wakolosai 4:6; Waefeso 4:29).

Mfano wa ucheshi wa Mungu ni tukio ambalo wana wa Israeli walikuwa wakilitumia sanduku la Agano kama chombo cha bahati wakati walipokuwa vitani, na Wafilisiti walimalizia kulichukua sanduku la hilo na kuliweka katika hekalu zao mbele ya sanamu yao Dagoni. Walikuja katika hekalu yao siku iliyofuata na wakapata Dagoni akiwa amelala kifudifudi mbele ya sanduku la Agano. Wakamsimamisha. asubhi iliyofuatia pia wakampata lakini wakati huu mikono yake na kichwa vilikuwa vimekatwa kama ishara yake kutokuwa na nguvu mbele za Mungu wa sanduku la Agano (1 Samueli 5:1-5). Mungu kumweka Dagoni katika hali ya kunyenyekea kwa sanduku lake la Agano ni taswira ya kejeli.

Tukio hili in mfano wa Mungu akichekelea upumbavu wa wale wanaompinga. "Tazama, ni matusi tu yatokayo mdomoni mwao, maneno yao yanakata kama upanga mkali; tena wanafikiri hakuna anayewasikia. Na Wewe, Bwana, utawacheka, Utawadhihaki mataifa yote" (Zaburi 59:7-8). Zaburi 2 pia yaeleza Mungu akiwacheka wale wote ambao wataasi ufalme wake (aya 4). Ni kama picha ya sarakasi ya mtoto wa chekechea akiwa amekasirishwa na wazazi wake na anatoroka nyumbani…na kutorokea nyumbani mwa majirani. Ijapokuwa kuna hatari ya hili, ingawa taswira ya mtu munyonge na mpumbavu anajaribu kubishana na Mungu Mkuu na ajuaye mambo yote ni mzaha, Mungu hafurahishwi na njia zao na madhara yake, bali anatamani kuwaona wakimgeukia (Ezekieli 33:11; Mathayo 23:37-38).

Mtu hawezi leta ujeshi mbele ya yule ambaye amempoteza mpendwa wake; ujeshi mbaya utakuwa mwovu kwa hali kama hiyo. Vile vile, Mungu anaangazia wale ambao wamepotea na anawatafuta wale ambao watatunza nafsi zao jinsi afanyavyo. Ndio maana maisha yetu (bado tungali na wakati wa kunywa na kucheka) yanapaswa kuwa na busara (kuwa na bidi katika kuyafanya maisha yetu kumfurahisha Kristo) (1Wathesaloniki 5:6, 8; Tito 2:2, 6).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je Mungu ana ucheshi?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries