settings icon
share icon
Swali

Ni kwa nini Mungu katika Agano la Kale yu tofauti kuliko Agano Jipya?

Jibu


Ukweli wa ndani kabisa wa swala hili kuna kutoelewa ni nini Agano la kale na Agano Jipya za funua/fichua kuhusu hali ya mungu. Njisi nyingine tunayoweza kuwasiliza wazo hili ni wakati watu wanasema, “Mungu wa Agano la Kale ni Mungu wa ghadhabu ile hali Mungu wa Agano Jipya ni Mungu wa upendo” wazo kwamba Bibilia ni Mungu anazidi kujidhihirisha kwetu kupitia matukio ya kihistoria/kale na kupitia uusiano wake na watu kupitia historia/kale yote inaweza kuchangia kukosa kuelewa ni nini mungu anafanana katika Agano la Kale inavyo linganishwa na Agano Jipya. Ingawa tunaposoma Agano la Kale na Agano Jipya, inabainika kwamba Mungu habadiliki kutoka agano moja hadi lingine na ghadhabu na upendo wake zimefunuliwa katika agano zote.

Kwa mfano katika Agano la Kale yote, Mungu amearifu kuwa “Mungu mwingi wa huruma, mwenye fadhili, si mwepesi wa hasira, mwingi wa rehema na kweili” (Kutoka 34:6; Hesabu 14:18; Kumbu la Torati 4:31; Nehemia 9:17; Zaburi 86:5,15; 108:4; 145:8; Yoeli 2:13). Bali katika Agano Jipya, upendo wa upole wa Mungu na neema zimedhihirishwa zaidi kwa ukamilifu kupitia kwa hoja kwamba, “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele” (Yohana 3:16). Katika Agano la Kale yote, pia twaona Mungu akiwapenda wana wa Israeli sawa na upendo wa baba anaompenda mwanawe. Wakati waliasi Mungu kwa makusudi na kuanza kuabudu miungu, Mungu atawarudi. Bali kila wakati alipowaokoa ikiwa walitupu kwa kuabudu kwao muingu. Kwa mfano, Waebrania 12:6 yatwambia, “Maana yeye ambaye Bwana ampenda, kumrudi, Naye humpiga kila mwana amkubaliye”.

Njia hiyo sawa, katika Agano la Kale lote twaiona hukumu ya Mungu na ghadhabu zikimwagika juu ya dhambi. Vilevile, katika Agano Jipya twaiona “ghadhabu ya Mungu imedhhiirishwa kutoka mbunguni juu ya uasi wote na uovu wa wanadamu waipingao kweli kwa uovu” (Warumi 1:18). Kwa hivyo kwa wazi Mungu is tofauti katika Agano la Kale kuliko alivyo katika Agano Jipya. Mungu kwa hali yake mwenyewe habadiliki. Ingawa tunaweza kuona sehemu ya hali yake moja ikidhihirishwa katika aya zingine zaidi kuliko zingine, Mungu mwenyewe habadiliki.

Tunaposoma na kuichunguza Bibilia, inadhihirika kwamba Mungu ni yule yule katika Agano la Kale na Agano Jipya. Ingawa Bibilia iko na vitabu 66 vilivyo andikiwa katika bara mbili ama tatu, katika lugha tatu tofauti katika muda wa kadri miaka 1500 na takribani waandhishi 40 au zaidi na inabaki kuwa kitabu kimoja kilicho jumulishwa kutoka mwanzo hadi mwisho bila kuhitalafiana. Ndani yake tunamwona Mungu, wa upendo, huruma na haki anayekabiliana na wanadamu wenye dhambi katika hali zote. Kwa kweli Bibilia ni barua ya Mungu ya upendo kwa wanadamu. Upendo wa Mungu kwa viumbe wake, hasa kwa mwanadamu ni wazi katika Bibilia yote. Katika Bibilia yote twauona wito wa upendo na huruma wa Mungu kwa wanadamu kuja kwa uhusiano maalumu naye, si kwa sababu wanastahili, lakini ni kwa sababu ni Mungu wa huruma na neema, mwepesi wa asira na mwingi wa upendo na kweli. Pia tunamwona Mungu mtakatifu na mwadhilifu ambaye ni hakimu wa wale wote wanaoasi na kukataa kumwabudu na kugeukia kuabudu miungu wengine waliojiundia (Warumi mulango wa 1).

Kwa sababu ya utakatifu wa Mungu na tabia (mtindo) yake takatifu, dhambi zote, za zamani, sasa na zijao zitahukumiwa. Bali upendo wa Mungu usio na kikomo ulitoa gharama ya dhambi na kutoa nafasi ya upatanisho ili mwanadamu mwenye dhambi aweze kuepuka ghadabu ya Mungu. Tunauona ukweli huu wa ajabu katika mstari kama 1Yohana 4:10: “Hili ndilo pendo, si kwamba sisi tulimpenda Mungu, bali kwamba yeye alitupenda sisi, akamtuma Mwanawe kuwa patanisho kwa dhambi zetu” katika Agano la Kale Mungu ametoa mpangilio wa tabihu wakati kafara zitatolewa kwa ajili ya dhambi. Ingawa huu mwelekeo wa kafara ulikuwa wa muda ambao ulikuwa unalenga kuja kwa Yesu Kristo ambaye atakufa msalabani ili akamilishe kutolewa kwa tabihu kwa ajili ya dhambi. Mwokozi alikuwa mwaidiwa katika Agano la kale ambaye kwa ukamilifu amedhihirishwa katika Agano Jipya. Katika Agano la Kale amefunikwa, upendo wa mwisho wa Mungu umedhihirishwa, kumtuma Mwanawe Yesu Kristo umeoneshwa kwa njia zake zote za utukufu katika Agano Jipya. Zote, Agano la kale na Agano Jipya zilitolewa “kutuekimisha hata tupate wokovu” (2Timotheo 3:15). Wakati tunachunguza Agano Jipya kwa makini, ni wazi kwamba Mungu “Kwake hakuna kubadilika, wala kivuli cha kugeuka-geuka” (Yakobo 1:17).

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Ni kwa nini Mungu katika Agano la Kale yu tofauti kuliko Agano Jipya?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries