settings icon
share icon
Swali

Kwa kuwa Mungu sio wa kiume, Je tunapaswa kuacha kutumia pronauni za kiume tunaporejelea Mungu?

Jibu


Tunajua kwamba Mungu ni kiumbe wa kiroho. Kusema kwa mkazo, hana jinsia. Ingawa Mungu amechagua kujifunua Mwenyewe kwa mwanadamu akitumia uume na taswira. Katika Biblia Mungu hajirejelei Mwenyewe akitumia maneno yasioyo na jinsia; Yeye hutumia maneno ya kiume. Jinsi Mungu amechagua kujifunua kwa wanadamu katika lugha ambayo inabainisha jinsia ya kuume, tunaweza kumrejelea katika lugha kama hiyo. Hakuna sababu ya kibiblia ya kutukomesha kutumia jina la kiume kwa kumrejelea Mungu.

Kutoka mwanzo wa Biblia Mungu hujirelea mwenyewe akitumia jina la kiume: "Basi, Mungu akaumba mtu kwa mfano wake; naam, kwa mfano wake Mungu alimuumba. Aliwaumba mwanamume na mwanamke" (Mwanzo 1:27). Tangu mwanzo Mungu amekuwa akijitambulisha kwa jina la kiume. Kiebrania cha kale hakikuwa na nomino ya jinsia, kwa hivyo vitu vyote kimakusudi vilipewa jinsia ya kilugha ya uume na uuke. Hiyo nomino ilikuwa ya makusudi. Katika Agano la Kale, nomino iliyomrejelea Mungu kisarufi ilikuwa ya kiume.

Hali kama hiyo inapatika katika Agano Jipya. Barua (kutoka Matendo hadi Ufunuo) zina takribani aya 900 ambapo neno la kigiriki theos-nomino ya kiume-imetumika kumrejelea Mungu. Ingawa kigiriki cha koine kilikuwa na maneno yasio ya jinsia yoyote, lakini bado Mungu anarejelewa katika jinsia ya kiume.

Fauka ya utungaji wa kisarufi, taswira imetumika katika Biblia pia inathibitisha kwamba Mungu ameamua kujirelea kwa sifa miliki ya kiume. Mafumbo kadhaa na cheo vimetumika kumwelezea Mungu. Kunayo mamia ya marejeleo ya Mungu kama Baba, Mfalme, Bwana. Yesu alitufunza kuomba hasa kwa "Baba" (Luka 11:2). Kunayo marejeleo mengi ya Mungu kama Baba kama vile Kumbukumbu 32:6, Malaki 2:10, na 1Wakorintho 8:6. Mungu anaitwa mfalme wazi (sio malkia) katika maandiko mengi; kwa mfano, Zaburi 24:10, Zaburi 47:2, Isaya 44:6, na 1Timotheo 1:17. Pia anaelezewa kuwa bwana mahali kama Isaya 54:5 na Hosea 2:2, 16 na 19.

Katika sehemu moja tabasamu imetumika kumrejelea akiwafariji watu wake kama vile mama anavyomfariji mwanawe (Isaya 66:13). Hata hapo Mungu hasemi kuwa yeye ni mama, ile hali anawafariji watu wake kama mama. Isaya 49:15 ni aya nyingine ambayo inataja mama katika kumwelezea Mungu, lakini sio hata linganisho; ni tofauti: Mungu huwajali zaidi watu wake kuliko mama mzazi anavyomjali mwanawe.

Ufunuo mkubwa zaidi wa Mungu kwetu ni kupitia kwa Mwana wake, Yesu Kristo (Waebrania 1:2). Katika kutwaa utu, Mwana alikuja ulimwenguni kama mwanaume na sio mwanamke. Yesu kila wakati alimrejelea Mungu kama Baba yake, na sio kama mama yake. Kabla ya kusulubiwa kwake, Yesu aliomba kwa Mungu akimwita, "Baba yangu" (Marko 14:36). Katika Injili pekee, Yesu anamwita Mungu "Baba" zaidi ya mara 100.

Tena, Mungu ni roho; Yeye sio "mume" kwa namna ya mume yeyote huku duniani anaonekana. Mungu hana sifa za kimwili na hana chembe chembe. Yeye yuu zaidi ya jinsia. Kwa wakati huo, Mungu kwa makusudi yake amejifunua Mwenye kwetu akitumia lugha ya kiume. Kila mara Mungu ni "wa kiume" katika Biblia. Tangu Mungu ana tumia nomino ya kiume kujirejelea yeye mwenyewe, anafaa kwendelea kutumia nomino ya kiume, tunapaswa kuendelea kuitumia nomino ya kiume katika kumrejelea Mungu.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Kwa kuwa Mungu sio wa kiume, Je tunapaswa kuacha kutumia pronauni za kiume tunaporejelea Mungu?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries