settings icon
share icon
Swali

Je! Ina maana gani kuwa Yesu ni Mungu pamoja nasi?

Jibu


Kabla ya kuzaliwa kwa Yesu, malaika alimwonekania Yusuf una kumfunulia kuwa mchumba wake, Mariamu, alikuwa na mimba kupitia Roho Mtakatifu (Mathayo 1:20-21). Mariamu alikuwa ajifungue mwana wa kiume, na walikuwa wampee jina Yesu. Halafu Mathayo akinukuu Isaya 7:14, alitoa ufunuo huu wa kutia moyo: "Basi, haya yote yalitukia ili litimie lile neno Bwana alilosema kwa njia ya nabii: "Bikira atachukua mimba, atamzaa mtoto wa kiume, nao watampa jina Imanueli" (maana yake, "Mungu yuko nasi")" (Mathayo 1:22-23).

Miaka mia saba mapema, nabii Isaya aliona uzao wa ubikra wa Masihi aliyeahidiwa. Alitabiri kwamba jina lake litakuwa Imanueli, maana yake "Mungu pamoja nasi." Kwa kurejelea maneno ya Isaya, Mathayo alimtambua Yesu kama Imanueli. Jina Imanueli linadhihirisha muujiza wa utwalizi wa mwili: Yesu ni Mungu pamoja nasi! Mungu alikuwa na watu wake kila wakati-katika mnara wa wingu juua yah ema ya ibada, kwa sauti ya manabii, kwenye sanduku la agano- lakini Mungu hajawahi kamwe kuwepo wazi na watu Wake jinsi alivyokuwa na Mwanawe aliyesaliwa kwa ubikira, Yesu, Masihi wa Israeli.

Katika Agano la Kale, uwepo wa Mungu kwa watu Wake mara nyingi ulikuwa dhahiri wakati utukufu Wake ulijaza hema (Kutoka 25:8; 40:34-35) na hekalu (1 Wafalme 8:10-11). Lakini utukufu huo ulipitwa mbali sana na uwepo wa Mungu-Mwana mwenyewe, Mungu alitwaa mwili, Mungu biniafsi pamoja nasi

Pengine kifungu muhimu zaidi katika Biblia juu Utwalizi wa mwili wa Yesu ni Yohana 1:1-4. Yohana akauli kwamba "naye alikuwa na Mungu, naye alikuwa Mungu. Tangu mwanzo Neno alikuwa na Mungu" (aya ya 1-2). Yesu anatumia neno logos (katika kigiriki), au "Neno," kama rejeleo la wazi la Mungu. Yohana anatangaza katika aya ya 14, "Naye Neno akawa mwanadamu, akakaa kwetu. Nasi tumeuona utukufu wake, utukufu wake yeye aliye Mwana wa pekee wa Baba; amejaa neema na ukweli."

Usiku wa kukamtwa kwake, Yesu alikuwa anawafunza wanafunzi wake. Filipo alikuwa na ombi: "Bwana, tuoneshe Baba, nasi tutatosheka." Hii ilikuwa hamu kamili ya kawaida. Lakini yesu akajibu, "Nimekaa nanyi muda wote huu, nawe Filipo hujanijua? Aliyekwisha niona mimi amemwona Baba" (Yohana 14:8-9). Yesu alikuwa anawaonesha Baba wakati wote. Kwa kweli "Mungu pamoja nasi." Popote Yesu alisungumza, alisungumza neno la Baba. Chochote Yesu alifany, alifanya kadri na vile Baba angetenda.

Mungu akauchukua mwili wa binadamu na damu (1 Timotheo 3:16). Hii ndio maana kutwaa mwili. Mwana wa Mungu kihalisi "alitangamana" nasi kama mmoja wetu; "akaweka hema Yake" katika boma letu (Yohana 1:14). mungu alituonyesha utukufu Wake na kutupa neema yake na kweli. Chini ya Agano la Kale, hema iliwakilisha uwepo wa Mungu, lakini sasa, chini ya Agano Jipya, Yesu Kristo ni Mungu pamoja nasi. Yeye si mfano tu wa Mungu kuwa pamoja nasi; Yesu ni Mungu binafsi kuwa pamoja nasi. Yesu si sehemu ya ufunuo wa Mungu; Yeye aliye pomoja nasi katika ukamilifu wake: "Maana, ndani yake Kristo katika ubinadamu wake, umo ukamilifu wote wa Mungu" (Wakolosai 2:9).

Mungu hujifanya kujulikana kwetu kikamilifu kupitia Yesu Kristo. Anajifunua Yeye mwenyewe kama mwokozi wetu (1 Petro 1:18-19). Yesu ni Mungu Pamoja nasi kama mpatanishi. Wakati mmoja tulikuwa tumetengwa na Mungu kupitia dhambi (Isaya 59:2), lakini wakati Yesu Kristo alikuja, alimleta Mungu kwetu: "Mungu alikuwa ndani ya Kristo, akiupatanisha ulimwengu na nafsi yake, asiwahesabie makosa yao" (2 Wakorintho 5:19; ona pia Warumi 8:3).

Yesu si Mungu Mungu pamoja nasi pekee lakini pia Mungu ndani yetu. Mungu anakuja kuishi ndani yetu kupitia Yesu Kristo wakati tunzaliwa mara ya pili: "Nimesulibiwa pamoja na Kristo; lakini ni hai; wala si mimi tena, bali Kristo yu hai ndani yangu; na uhai nilio nao sasa katika mwili, ninao katika imani ya Mwana wa Mungu, ambaye alinipenda, akajitoa nafsi yake kwa ajili yangu" (Wagalatia 2:20). Roho wa Mungu anaishi ndani yetu, na sisi ni makao yake: "Kwa maana sisi tu hekalu la Mungu aliye hai; kama Mungu alivyosema, ya kwamba, Nitakaa ndani yao, na kati yao nitatembea, nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu'" (2 Wakorintho 6:16).

Yesu si Mungu Pamoja nasi kwa muda mfupi, bali milele yote. Mungu Mwana, hakomi hata wakati mmoja kuwa mtakatifu, aliuchukua hali ya mwili wa mwanadamu na akawa "Mungu pamoja nasi" milele: "mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari" (Mathayo 28:20; pia ona Waebrania 13:5).

Wakati ulipowadia wa Yesu kurudi kwa Babaye, aliwaambia wanafunzi wake, "Nami nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi mwingine, ili akae nanyi hata milele" (Yohana 14:16). Yesu alikuwa anasungumzia Roho Mtakatifu, mtu watu katika Utatu, ambaye ataendelea kuleta uwepo wa Mungu kuishi ndani ya maisha ya waumini. Roho Mtakatifu anatekeleza jukumu la Yesu kama mwalimu, mfunuzi wa kweli, mtia moyo, mfariji, mwombezi, na Mungu pamoja nasi.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Ina maana gani kuwa Yesu ni Mungu pamoja nasi?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries