settings icon
share icon
Swali

Je, Mungu ni mkatili?

Jibu


Kuna watu wasioamini kwamba kuna Mungu, wanaosadiki kuwa hatuna habari za Mungu ambao husema kwamba Mungu anayezungumziwa katika Biblia ni mkatili. Wanavitia tu mioyo yetu ya kibinadamu kwa kusema kuwa Mungu ni mkatili. Neno ukatili inafafanuliwa kuwa "kutojali kabisa au kufurahi katika kusababisha maumivu na mateso." Swali ibuka ni, je, Mungu mkatili? Kwa kuyakinisha, inatulazimisha kuruhuhusu kwamba Mungu hajali kuhusu maumivu na mateso au anafurahia kuona viumbe vyake vikiteseka.

Wale wasioamini kwamba kuna Mungu, ambao hudai kuwa Mungu ni mkatili wana mzigo mkubwa wa kudhibitisha maneno hayo. Wanadai kujua matendo ya Mungu na pia wanadai kujua kikamilifu hali ambayo alifanya vitendo hivyo, na vile vile motisha wake. Zaidi ya hayo, wanadai kujua akili ya Mungu, huku wakimpa mtazamo wa kutojali au raha ya kuudhi ili kumfafanua kama mkatili. Kwa kweli, hii ni zaidi ya wakosoaji kuonyesha kwamba hawawezi kujua akili ya Mungu. "Maana mawazo yangu si mawazo yenu, wala njia zenu si njia zangu; asema Bwana.Kwa maana kama vile mbingu zilivyo juu sana kuliko nchi, kadhalika njia zangu zi juu sana kuliko njia zenu, na mawazo yangu kuliko mawazo yenu" (Isaya55:8-9).

Hamna shaka kwamba kwa wakati Mwingine Mungu huruhusu na kusababisha maumivu na mateso, lakini wema wa Mungu hauwezi kutiliwa shaka kwa sababu anafanya jambo amabalo linaonekana kuwa katili kwetu. Hatuwezi kudai kujua fikra zake katika kila hali lakini tunajua sababu kadhaa za vitendo ambavyo vinavyoonekana kuwa katili kwetu, haswa ikiwa hatujui ama hatujali kujua kuhusu hali ya vitendo hivyo.

1. Kutoa adhabu ya haki: Ikiwa adhabu ni ya haki, inaweza semekana kuwa ni ya kikatili? Kile ambacho wakosoaji mara nyingi hawaelewi ni kwamba upendo wa Mungu haupungui wakati anapoleta adhabu kwa watu. Mungu ana uwezo wa kutoa adhabu kwa kundi la watu waovu ili kuokoa wale ambao wamejitolea kwake. Kutotoa adhabu ya makosa ingekua jambo la kikatili na kungeonyesha ukatili kwa wale wasio na hatia. Wakati Mungu alisababisha Bahari Nyekundu kufunga, na kuzamisha jeshi lote la Farao, Yeye alikuwa akiadhibu uasi wa Farao ili kuwaokoa watu wake aliowachagua kutoka kwa kuuawa na kuangamia (Kutoka 14). Makosa ambayo hayaadhibiwi bila shaka husababisha dhambi kubwa ambayo haifaidi mtu yeyote na huharibu fanaka ya kila mtu. Hata wakati Mungu aliwaambia Waisraeli kuwaangamiza kabisa maadui wa Mungu, wakiwepo wanawake na watoto, alijua kwamba kuwaruhusu waishi kungesababisha kuwepo kwa vizazi vijavyo vilivyojitolea kwa ibada ya sanamu -ikiwa ni pamoja na visa vya watoto kutolewa kama sadaka katika madhabau ya miungu wa uongo.

2. Kuleta faida kubwa zaidi: Maumivu na mateso ambayo huleta faida zaidi wakati mwingine hayawezi kuletwa kwa njia nyingine. Biblia inatuambia kwamba majaribu na mambo magumu husababisha Wakristo walio na nguvu, bora na tunapaswa "kuhesabu kuwa ni ya furaha tupu" (Yakobo1:2) wakati tunapokabiliana nayo. Mungu huyaleta haya kwa faida kwetu, ili kutusafisha kama dhahabu katika moto wa mateso. Mtume Paulo alichukulia mateso-kichapo, kupigwa kwa mawe, kuharibika kwa meli,njaa, baridi, kufungwa gerezani- kama njia ya kuhakikishwa kwamba atawahi kujua udhaifu wake, kuwa angekumbuka kila wakati kwamba nguvu iliyofanya kazi ndani yake ilitoka kwa Mungu, na sio yeye mwenyewe, na kamwe hatadanganyika kutegemea uwezo wake mwenyewe (2 Wakirintho 1:8-10; 4:7-12). Haki ya Mungu inadhibitishwa dhidi ya wasioamini wakati anawafanya wapate maumivu ma mateso. Yeye anaonyesha huruma yake kwao kwa kuwaonya mara kwa mara juu ya matokeo ya dhambi. Wakati wanapoleta msiba juu yao kwa njia ya uasi wao, inakuwa ni adhabu sio ukatili. Waasi wananapoendelea kumtikisa Mungu ngumi zao kwa muda, jinsi yeye anavyoruhurusu inaonyesha rehema zake na saburi yake, wala sio ukatili.

3. Ili kujipa utukufu: Mungu anatukuka kupitia dhihirisho la sifa zake. Sote tunakubali kuwa Yeye anaonekana mzuri kwetu wakati anaonyesha upendo na rehema yake, lakini kwa kuwa kila sifa ni takatifu na kamilifu, hata dhihirisho la ghadhabu na hasira yake humletea utukufu. Na hiyo ndiyo lengo kuu-utukufu wake, sio wetu. Akili zetu ndogo haziwezi kumwaza, na pia kumhoji Mungu.

Mambo haya yote yanayosababisha maumivu na mateso yanastahili, ni ya haki na ni halali. Kinyume na madai ya wakosoaji, kuna sababu nzuri za Mungu kuruhusu uovu na mateso katika ulimwengu huu. Kumwamini Mungu licha ya kutojua sababu hizi sio imani potovu. Badala yake, tunamwamini na vitu ambavyo hatuzielewi kwa sababu tunaona uaminifu wake katika matendo ambayo tunayaelewa.

Tunaposoma Biblia kwa uangalifu , badala ya kumwaona Mungu akitenda kwa ukatili, tunamuona Yeye akitenda kwa ajili ya upendo wake kwetu. Kwa mfano, kitabu cha Ayubu mara nyingi huonyeshwa kama mfano wa matendo ya Mungu ya kuhuzunisha dhidi ya mtu asiye na hatia. Kitabu hicho kinatangaza kwamba Ayubu hakuwa na hatia kwa mateso yaliyo mpata, jambo ambalo linaonekana kupendelea madai ya wasioamini kuwepo kwa Mungu. Lakini kudai kwamba inadhibitisha kuwa Mungu ni mwenye kuhuzunisha inaonyesha kuelewa kwa juujuu kwa kitabu cha Ayubu.

Katika Mashariki ya Karibu wakati wa mababu, Imani ya kawaida ilikuwa kwamba Mungu kila wakati aliwabariki waadilifu na kuleta mateso kwa wasio waadilifu. Kitabu cha Ayubu kinabishana dhidi ya theoloja hiyo. Hadithi hiyo inaonyesha kwamba maoni ya mwanadamu kuhusu haki ya Mungu yanahitaji kurekebishwa. Tunahitaji kuelewa kwamba Mungu hazuiliwi kutumia mateso kama njia ya kulipiza kisasi. Anayatumia mateso pia kutenga watu kutoka kwa vitu vya dunia ambavyo vinawashawishi. Kwa kuongeza, Ayubu analeta watu karibu katika kufahamu kazi ya Mungu ya upatanisho msalabani. Ikiwa mwanadamu angeendela kifikiri kwamba Mungu hangemruhusu mtu asiye na hatia kuteseka, basi tutakuwa tumekosa mpango wa Mungu wa kuukomboa ulimwengu. Kwa maana Mungu aliruhusu mateso ya Mtu asiye na hatia (Yesu Kristo) ili kuleta wokovu wake. Kwa hivyo kitabu hiki cha Ayubu kinachangia pakubwa katika historia ya ukombozi.

Kwa mukhutasari, wakosoaji wana kazi ngumu ya kudhibitisha kwamba vitendo vya Mungu vinaonyesha ukatili. Kwa muktadha, vifungu vya biblia ambavyo vinaonekana kumwonyesha Mungu kama mkatili kwa kweli havifanyi kitu kama hicho. Kwa kweli, kwa ufahamu mzuri wa maandiko, tunaona kwamba matendo ya Mungu daima yanachochewa na hulka yake takatifu na kamilifu.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, Mungu ni mkatili?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries