settings icon
share icon
Swali

Je, ni nini uhusiano kati ya Mungu na wakati?

Jibu


Tunaishi katika ulimwengu wa asili ambao una vipimo vyake vinne vya urefu, upana, utambo, (au kina) na wakati. Hata hivyo, Mungu anakaa katika ufalme mwingine-ufalme wa kiroho- zaidi ya utambuzi wetu wa kimwili. Sio kwamba Mungu hayuko, ni suala la kutokuwa na sheria na vipimo ambavyo vinatawala ulimwengu wetu (Isaya 57:15). Tunajua kwamba "Mungu ni roho" (Yohana 4:24), basi ni nini uhusiano wake na wakati?

Katika Zaburi 90:4, Musa alitumia mfano wa rahisi na wa maana katika kuelezea hali ya kutokuwa na wakati kwa Mungu: "Maana miaka elfu machoni pako ni kama siku ya jana ikiisha kupita, na kama kesha la usiku." Umilele wa Mungu unalinganishwa na muda mfupi wa mwanadamu. Maisha yetu ni mafupi na dhaifu lakini Mungu hadhoofiki au kuwa mdhaifu kwa muda.

Kwa maana kuashiria kwa wakati sio muhimu kwa Mungu kwa kuwa yeye yu juu zaidi ya wakati. Petro, katika 2 Petro 3:8, aliwaonya wasomaji wake wasiruhusu ukweli huu muhimu kuwapita-kwamba mtazamo wa Mungu kuhusu wakati ni tofauti na mtazamo mwanadamu (ona pia Zaburi 102:12,24-27). Bwana hajafungwa na wakati jinsi ambavyo tumefungwa. Yeye ni juu ya nyanja za wakati. Mungu huona milele iliyopita na milele ijayo.Wakati unaopita duniani ni kama kufumba na kufumbua katika mtazamo wa Mungu. Sekunde haina tofauti na kipindi kirefu cha wakati; miaka bilioni inapita kama sekunde machoni pa Mungu wa milele.

Ingawa hatuwezi kuelewa wazo hili la umilele wa Mungu, sisi katika akili zetu zilizo na mwisho tunajaribu kumweka Mungu asiye na mwisho katika ratiba yetu ya wakati. Wale ambao kwa upumbavu wanadai kwamba Mungu afanye kazi kulingana na ratiba yao hupuuza ukweli kwamba Yeye "ndiye aliye juu…aishiye milele" ( Isaya 57:15). Maelezo haya ya Mungu ni tofauti na hali ya binadamu: "Miaka ya kuishi ni sabini, au tukiwa wenye afya, themanini; lakini yote ni shida na taabu!Siku zapita mbio,nasi twatoweka mara" (Zaburi 90:10).

Tena, kwa sababu ya akili zete zenye mwisho, tunaweza kufahamu sehemu tu la wazo la umilele wa Mungu. Na katika kufanya hivyo, tunamweleza kama Mungu asiye na mwanzo wala wisho, wa milele, asiye na mipaka, aishiye milele na kadhalika. Zaburi 90:2 inasema, " Wewe ndiwe Mungu, milele na milele" (ona pia Zaburi 93:2). Yeye amekuwepo kabla ya nyakati zote.

Je, wakati ni nini? Kueleza kwa urahisi, wakati ni muda. Saa zetu huonyesha mabadiliko au, kwa usahihi saa zetu zetu huonyesha madadiliko ambayo huonyesha kupita kwa wakati. Tunaweza kusema basi, wakati lazima uwepo ili kufanikisha mabadiliko, na mabadiliko lazima yawepo kuonyesha wakati uliopita. Kwa maneno mengine, wakati wowote kuna mabadiliko ya aina yoyote, tunajua kuwa wakati umepita. Tunaona haya tunapoishi, tunavyozeeka. Na hatuwezi kuzipata tena dakika ambazo zimepita.

Kwa kuongeza, sayansi ya fizikia inatuambia kuwa wakati ni kitu ambacho hutokana na uwepo wa jambo. Basi, wakati unakuwepo wakati jambo lipo. Lakini Mungu sio jambo; Mungu kwa kweli aliumba jambo. Cha msingi ni kwamba, wakati ulianza pindi mungu alipoumba ulimwengu. Kabla ya hayo, Mungu alikuwepo tu. Kwa kuwa hakukuwa na jambo, na kwa sababu Mungu habadiliki, wakati haukuwepo na kwa hivyo hauna maana, hakuna uhusiano naye.

Na hii inatuleta katika maana ya neno milele. Milele ni neno linalotumika kueleza dhana ya kitu ambacho hakina mwisho na/ au hakina mwanzo. Mungu hana mwanzo au mwisho. Yeye ni juu zaidi ya ulimwengu wa wakati. Umilele sio kitu ambacho kinaweza kuhusishwa kabisa na Mungu. Mungu ni juu zaidi ya umilele.

Maandiko yanaonyesha kwamba Mungu anaishi nje ya mipaka ya wakati jinsi tunavyoijua. Hatima yetu ilipangwa "Kabla ya mwanzo wa nyakati" (2 Timotheo 1:9; Tito 1:2) na "Kabla ya kuweka msingi wa ulimwengu" (Waefeso 1:4; 1 Petro 1:20). "Kwa imani twafahamu ya kuwa ulimwengu uliumbwa kwa neno la Mungu, hata vitu vinavyoonekana havikufanywa kwa vitu vilivyo dhahiri" (Waebrania 11:3). Kwa maneno mengine, ulimwengu tunaoona, kusikia, kuhisi haukuumbwa kutoka kwa kitu kilichokuwepo, lakini ni kutoka kwa chanzo kilicho huru kutoka kwa vipimo tunavyoweza kuona.

"Mungu ni roho" (Yohana 4:24), na vivyo hivyo, Mungu ni wa milele, na yeye ni zaidi ya wakati. Wakati uliubwa na Mungu kama sehemu ya uumbaji wake kwa ajili ya kutekeleza kazi na kusudi lake katika ulimwengu utakaotoweka (ona Petro 3:10-12).

Baada ya kukamilisha shughuli yake ya uumbaji, ikiwemo uumbaji wa wakati, Mungu alihitimisha vipi? "Mungu akaona kila kitu alichokifanya kuwa ni chema kabisa" (Mwanzo 1:31). Kwa kweli, Mungu ni roho katika ulimwengu wa umilele.

Kama waumini, tunayo faraja kubwa tukijua kwamba Mungu, ingawa ni wa milele, yuko katika wakati nasi sasa; sio kwamba hatuwezi kumfikia, lakini yuko nasi wakati huu. Na kwa sababu yuko katika wakati huu, Yeye anaweza kutimiza mahitaji na maombi yetu.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, ni nini uhusiano kati ya Mungu na wakati?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries